Mkuu wa JKT nchini Meja Jenerali Charles Mbuge wamefanya
ziara ya siku moja mkoani Simiyu kwa lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji
wa miradi inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi hilo SUMA JKT.
Akikagua miradi hiyo jana Julai 03, 2020 Meja Jenerali Mbuge
amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kuongeza kasi katika utekeleza ili miradi
hiyo iweze kukamilika kwa wakati.
“Nataka site (maeneo ya kazi) zichangamke, hakikisheni mnaongeza
watenda kazi wakiwemo mafundi na vibarua; tafuteni mashine zenye uwezo wa
kufyatua tofali nyingi kwa wakati mmoja ili kazi iende kwa kasi na
viwango," alisema Mbuge.
Aidha, Brigedia Jenerali Mbuge amewaagiza viongozi wote
wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi bila
kusimamiwa huku akisisitiza kuwa atafuatilia utekelezaji wa maagizo yote
aliyoyatoa kwa viongozi wa JKT ambao ni wasimamizi wa miradi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali ya
Mkoa inatambua kazi nzuri inayofanywa na SUMA JKT mkoani hapa, huku akibainisha
kuwa anatarajia kuona matokeo zaidi baada ya ziara ya Mkuu wa JKT kutokana na
maelekezo aliyotoa kwa wasaidizi wake ambayo mengine amehusika moja kwa moja
kuwa sehemu kubwa ya utatuzi wa changamoto kwenye miradi hiyo.
"Ziara hii imekuwa ziara darasa na sisi kama viongozi
tumejifunza mengi kwako Mkuu wa JKT hasa katika suala la kufanya maamuzi;
tunategemea kuona matokeo baada ya ziara hii kutokana na maelekezo
uliyoyatoa," alisema Mtaka.
Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah
amesema Serikali ya Mkoa na taasisi za Umma zilizopo inaunga mkono SUMA JKT huku
akiomba zaidi ya shilingi milioni 700 zilizolipwa kwa ajili ya kuendeleza
ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu zitumike kufanya kazi hiyo ili kutoa
nafasi kwa Katibu Tawala Mkoa kupewa fedha nyingine na lengo la kukamilisha
jengo hilo Desemba 2020 litimie.
Msimamizi Mkuu wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa, Kapteni Fabian Buberwa
ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa JKT na kusisitiza
kuaysimamia kwa kadri alivyoelekeza.
SUMA JKT katika Mkoa wa Simiyu inatekeleza ujenzi wa miradi
mbalimbali ikiwemo ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa, Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa , ujenzi wa jengo la wizara ya kilimo
katika uwanja wa nanenane Nyakabindi, ujenzi wa kiwanda cha chaki na kiwanda
cha vifungashio.
MWISHO.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge (wa tatu kulia) akitoa maelekezo kwa
wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya wizara ya kilimo katika Viwanja vya
nanenane Nyakabindi Bariadi, katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi
wa miradi inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge (wa tatu kulia) akitoa maelekezo kwa
wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu Nyaumata mjini
Bariadi, katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi
inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Sehemu ya
jengo al ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu inayoendelea kujengwa katika eneo la Nyaumata
Mjini Bariadi.
sehemu ya jengo la ofisi ya wizara ya kilimo inayojengwa na SUMA JKT katika
Viwanja vya nanenane Nyakabindi Bariadi.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa
mkoa na JKT wakati wa ziara ya Mkuu wa JKT nchini Brigedia Jenerali Charles
Mbuge( kulia) mkoani hapa kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi
inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge akizungumza na viongozi wa mkoa wa
Simiyu mara baada ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa miradi inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini
Bariadi.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge akiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa
wa Simiyu akitoka eneo la Nyaumata mahali panapojengwa Jengo la ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi
inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa JKT nchini Brigedia Jenerali
Charles Mbuge wakitoa maelekezo katika eneo la ujenzi wa jengo la wodi ya
wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi
wa miradi inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa
mradi wa ujenzi wa Wodi ya wazazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
Nyaumata mjini Bariadi, katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
miradi inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa
mradi wa ujenzi wa ofisi ya wizara ya kilimo katika Viwanja vya nanenane Nyakabindi
Bariadi, katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi
inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge akiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa
wa Simiyu akitoka eneo la Nyaumata mahali panapojengwa Jengo la Wizara ya
kilimo linalojengwa katika viwanja vya nanenane Nyakabindi Bariadi, wakati wa
ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi inayotekelezwa na SUMA JKT
aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu
Tawala Msaidizi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Mashaka
Luhamba anayeshughulikia sehemu ya miundombinu akichangia hoja katika kikao cha
Mkuu wa JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge na viongozi mbalimbali wa
mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi
inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge akitoa maelekezo katika eneo la
ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi inayotekelezwa na
SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa
JKT nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge (katikati) akitoa maelekezo kwa
wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya wizara ya kilimo katika Viwanja vya
nanenane Nyakabindi Bariadi, katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi
wa miradi inayotekelezwa na SUMA JKT aliyoifanya Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment