Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Kighoma Malima ametoa wito wananchi wa mikoa ya
Simiyu, Mara, Shinyanga na maeneo mengine nchini kafika katika maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu
katika Kanda ya Ziwa Mashariki inayoundwa na mikoa ya Simiyu, Mara na
Shinyanga ili wajionee maonesho yenye
kiwango.
Mhe.
Malima ameyasema hayo Juni 27, 2020 katika
kikao cha maandalizi ya Maonesho hayo ambayo yatafanyika kitaifa katika kanda
hiyo kwa mara ya tatu mfululizo kilichofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa
nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
“Ingawa
maandalizi yetu yaliathiriwa na changamoto ya Corona bado tuna uhakikia wa
kufanya vizuri kwani tumepita kuangalia maendeleo ya vipando, vipando viko
katika hali nzuri na tunaamini kuwa maonesho haya yatakwenda vizuri kama ilivyo
kawaida yetu, hivyo tunawakaribisha wananchi wote kushiriki maonesho haya
ambayo yatakuwa ya viwango,” alisema Malima.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack amesema Kanda ya Ziwa Mashariki itafanya
vizuri katika maonesho ya kitaifa mwaka 2020 kuliko miaka miwili ya mwanzo, kwa kuwa pamoja na changamoto
zilizojitokeza katika maandalizi kumekuwa na mwamko mkubwa wa ushiriki wa wadau
katika maonesho haya.
Katika
hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema wadau
mbalimbali zikiwemo taasisi binafsi na za Umma, wananchi wakiwemo wajasiriamali
na wafanyabiashara wameonesha mwitikio mkubwa na wanaendelea na maandalizi
ambapo alibainisha kuwa katika maonesho ya nanenane mwaka huu washiriki
takribani 500 wanatarajiwa kushiriki.
Aidha
Bi. Mmbaga ametoa wito kwa wananchi wote nchini hususani wa mikoa ya Simiyu, Mara
na Shinyanga kuitumia vizuri fursa ya kuwa maonesho haya ya Kitaifa kufanyika
katika kanda ya ziwa Mashariki na wajitokeze kwa wingi katika maonesho haya ili
waweze kupata kuona mambo mbalimbali yatakayosaidia kuongeza tija kwenye maeneo
yao ya uzalishaji.
Maonesho
ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema “KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI
CHAGUA VIONGOZI BORA 2020.”
Baadhi ya viongozi na
wataalam wakitembelea vipando mbalimbali
vya mazao vilivyoandaliwa kwaa jili ya maonesho ya nanenane kabla ya
kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika
kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa hiyo mitatu ambayo yatafanyika kwa
mara ya tatu mfululizo sasa katika
Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.
0 comments:
Post a Comment