Shirikisho la Walimu wanamazingira mkoa wa Simiyu wametoa msaada wa vifaa vya kunawia mikono ikiwa ni sehemu ya uungaji mkono juhudi za serikali mkoani hapa katika kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Vifaa hvyo ambavyo vyenye thamani ya shilingi 167,000/= vimepokelewa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Julai 03, 2020.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa naiaba ya walimu hao Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Mwalimu Aron Kiunsi amesema wameguswa kutoa msaada huo kwa viongozi wa mkoa ili wao waweze kupelekea vifaa hivyo kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi ikiwa ni pamoja na shule ambazo kwa sasa zimefunguliwa na wanafunzi wana uhitaji wa vifaa hivyo.
Akipokea vifaa hivyo Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah amewashukuru walimu hao kwa kujitolea kuunga mkono nguvu ya mkoa katika tahadhari dhidi ya Corona, huku akiendelea kutoa wito kwa wadau wengine kutoa msaada wa vifaa hivyo katika maeneo yenye uhitaji mkubwa ikiwa ni pamoja na shule.
“Ninawashukuru sana walimu kwa kutambua mahitaji tuliyo nayo katika kuchulua tahadhari ya Virusi vya Corona na kujitolea sehemu ya vipato vyao kununua vifaa hivi kuunga nguvu ya mkoa, sisi kama watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa tutahakikisha kuwa vifaa hivi vitapelekwa katika baadhi ya shule za msingi na sekondari ambako kuna uhitaji mkubwa,” alisema Weginah.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema anawashukuru walimu kwa kuendela kuwa wadau muhimu katika sekta ya elimu kwanza kupitia ufundishaji na pili kupitia uchangiaji huku akieleza kuwa mchango wa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kuwakinga na maradhi mbalimbali ikiwemo maambukizi ya Corona na kusababisha wanafunzi kusoma wakiwa salama.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Khamis Kulemba amesema idara ya afya mkoa iko bega kwa began a walimu hao kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakuwa salama ambapo ameseitiziza kuwa itasimamia kuhakikisha tahadhari zote dhidi ya ugonjwa wa COVID 19 zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na unawaji mikono kwa maji tiririka na sabuni.
“Walimu, viongozi na jamii yote kwa ujumla twendeni tukalinde afya za watoto wetu na kulinda haki hizo ni kuhakikisha zile tahadhari zote zinafuatwa wakati wote wanapokuwa shuleni; msaada mliotoa leo ni mfano wa kuigwa kwa mtu mmoja mmoja, mashirika na taasisi mbalimbali, niwahakikishie tu kuwa tuko pamoja nanyi kuhakikisha Corona ndani ya Simiyu inatokomezwa kabisa,” alisema Dkt. Kulemba.
Naye Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Simiyu Bw.Mayunga George amewapongeza walimu hao kwa msaada walioutoa kwa ajili ya kuwasaidia watoto kusoma kwa usalama zaidi, huku akiwapongeza pia kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuwafundisha watoto na kuufanya mkoa kuwa katika nafasi nzuri katika ufaulu ambapo amebainisha kuwa ufudishaji wao unaifanya kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya tano katika elimu kupitia elimu bila malipo ionekane.
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na walimu wanamazingira
mkoa wa Simiyu ofisini kwake mara baada ya walimu hao kukabidhi vifaa vya kunawia mikono ili kuchukua
tahadhari ya maambukizi ya Corona hususani katika shule mbalimbali, Julai 03, 2020 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment