Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Mhe. Adam Kighoma Malima ametoa wito wananchi wa mikoa ya Simiyu, Mara,
Shinyanga na maeneo mengine nchini kafika katika maonesho ya Nanenane Kitaifa
mwaka 2020 yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu katika
Kanda ya Ziwa Mashariki inayoundwa na mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ili wajionee maonesho yenye kiwango.
Mhe. Malima ameyasema
hayo Juni 27, 2020 katika kikao cha
maandalizi ya Maonesho hayo ambayo yatafanyika kitaifa katika kanda hiyo kwa
mara ya tatu mfululizo kilichofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa nyakabindi
Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
“Ingawa maandalizi yetu
yaliathiriwa na changamoto ya Corona bado tuna uhakikia wa kufanya vizuri kwani
tumepita kuangalia maendeleo ya vipando, vipando viko katika hali nzuri na
tunaamini kuwa maonesho haya yatakwenda vizuri kama ilivyo kawaida yetu, hivyo
tunawakaribisha wananchi wote kushiriki maonesho haya ambayo yatakuwa ya
viwango,” alisema Malima.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Mhe. Zainab Telack amesema Kanda ya Ziwa Mashariki itafanya vizuri
katika maonesho ya kitaifa mwaka 2020 kuliko miaka miwili ya mwanzo, kwa kuwa pamoja na changamoto
zilizojitokeza katika maandalizi kumekuwa na mwamko mkubwa wa ushiriki wa wadau
katika maonesho haya.
Katika hatua nyingine
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema wadau mbalimbali
zikiwemo taasisi binafsi na za Umma, wananchi wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara
wameonesha mwitikio mkubwa na wanaendelea na maandalizi ambapo alibainisha kuwa
katika maonesho ya nanenane mwaka huu washiriki takribani 500 wanatarajiwa
kushiriki.
Aidha Bi. Mmbaga ametoa
wito kwa wananchi wote nchini hususani wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga
kuitumia vizuri fursa ya kuwa maonesho haya ya Kitaifa kufanyika katika kanda
ya ziwa Mashariki na wajitokeze kwa wingi katika maonesho haya ili waweze
kupata kuona mambo mbalimbali yatakayosaidia kuongeza tija kwenye maeneo yao ya
uzalishaji
Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2020 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema “KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020.”
MWISHO
Baadhi ya viongozi na
wataalam wakitembelea vipando mbalimbali
vya mazao vilivyoandaliwa kwaa jili ya maonesho ya nanenane kabla ya
kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika
kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa hiyo mitatu ambayo yatafanyika kwa
mara ya tatu mfululizo sasa katika
Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.Baadhi ya viongozi na wataalam wakitembelea vipando mbalimbali vya mazao vilivyoandaliwa kwaa jili ya maonesho ya nanenane kabla ya kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa hiyo mitatu ambayo yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo sasa katika Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akizungumza na viongozi na wataalam kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambayo yatafanyika katika Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na viongozi na wataalam kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika kanda ya ziwa mashariki inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambayo yatafanyika katika Uwanja wa NaneNane Nyakabindi jana uwanjani hapo.
AANGALIA BAADHI
YA PICHA ZA VIONGOZI KATIKA KIKAO CHA MAANDALIZI YA NANENANE, PICHA ZAO
WAKITEMBELEA VIPANDO, PICHA ZA VIPANDO, MAJENGO NA UJENZI WA MAHEMA
0 comments:
Post a Comment