Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI imekabidhi masanduku 10 kutoka
Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi kwa Mkoa wa Simiyu ili yatumike kwa ajili
ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na
UKIMWI.
Akikabidhi masanduku hayo Mkurugenzi wa TACAIDS Dkt. Leonard
Maboko amesema karibuni Wafadhili wamepunguza kwa kiasi kikubwa ufadhili katika
masuala ya Ukimwi ni  vema zikatumika  fedha zetu wenyewe (wadau wa ndani)  badala ya kutegemea Wafadhili
“ Ili Kuchangia fedha hizo Mfuko  umebuni Masanduku ambayo
Wanainchi wanaweza kutoa michango kwa Fedha taslim, tumeleta masanduku haya 10
ikiwa ni maagizo ya Waziri wa nchi ofisi ya Waziri  Mkuu Kazi, Vijana,Ajira
na Wenye  Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ambaye alikuwa mgeni rasmi
akimwakilisha  Mhe. Kassim Majaliwa  Waziri Mkuu,wakati wa maadhimisho
ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza 2019”
“ Katika maadhimisho hayo kila mkoa uliagizwa kuwa na  
masanduku hayo na kuhamasisha wananchi kuchangia jitihada hizi, Siku ya Ukimwi
Duniani 2020 kila mkoa utatakiwa kutoa taarifa kuwa umechangia Serikali kiasi
gani kupitia Mfuko wa Udhamini wa  kudhibiti Ukimwi, alisema Dkt. Maboko.
Aidha, Dkt. Maboko amesema michango hiyo inaweza 
kuwakilishwa kwa kuchangia Moja kwa moja au kupitia AIrtel Money +255 684
909090 au kwa Viongozi kuchukua masanduku na kuhamasisha wananchi kuchangia
katika ziara na matukio mbalimbali ambayo wao wanayaongoza huku akibainisha
kuwa mpaka sasa fuko umeshaipatia Serikali kiasi cha shilingi 660.
Katika hatua nyingine Dkt. Maboko amefafanua kuwa katika fedha
zote zinazokusanywa  katika mfuko huu, asilimia 60 hutumika kwenye ununuzi
wa dawa/vitendanishi,  asilimia 25
hutumika   kwenye kinga na asilimia 15 kwenye shughuli za bodi na
Utawala.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu, Mhandisi.Mashaka
Luhamba ameshukuru TACAIDS kwa kutimiza ahadi ya kuleta masanduku hayo kama
walivyoahidi kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa huku akiwahakikishia TACAIDS kuwa mkoa
utatumia kila fursa kuhakikisha kuwa unawahamasisha Wananchi wa  Simiyu
kuchangia katika Mfuko huu.
Akieleza hali ya maambukizi ya VVU/UKIMWI katika Mkoa wa Simiyu,
Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Simiyu, Dkt.Khamis  Kulemba amesema kutokana
na utafiti wa Mwaka  2016-2017 ushamiri wa maambuziki ya VVU Mkoani Simiyu
umefikia kiwango cha  3.9%  ambayo ni chini ya  4.7% ikiwa
ni  kiwango cha  kitaifa
“ Tunaendelea na kazi ya kuzuia maambukizi mapya kwa kuwezesha asilimia
90 watu wanatambua hali za afya zao,  asilimia 90% ya  wagonjwa  wanatumia
dawa na asilimia 90 nyingine kushusha kiwango cha virusi vya UKIMWI katika damu
ya Mgonjwa ( Viral suppression)
Dkt. Kulemba ameongeza kuwa Mkoani Simiyu asilimia 91 ya watu
wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU na
kiwango cha maambukizi katika damu zao kimeshuka, huku akitoa wito kwa wananchi
kuchangia mfuko wa kudhibiti UKIMWI kwani vita dhidi ya VVU/UKIMWI ni ya kila
mmoja katika jamii.
Mfuko wa Udhamini wa kudhibiti ukimwi  ulianzishwa
Mwaka  2015, Kusudi la Mfuko huu ni  kuchangia fedha kwa ajili
ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.
MWISHO
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS),  Dkt. Leonard Maboko(kushoto) akimkabidhi moja
ya sanduku Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi.Mashaka Luhamba yaliyotolewa na
TACAIDS kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha
huduma za VVU na UKIMWI.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi.Mashaka Luhamba (kushoto) akimkabidhi
Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Simiyu, Dkt.Khamis  Kulemba moja ya masanduku yaliyotolewa
na TACAIDS kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha
huduma za VVU na UKIMWI.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi.Mashaka Luhamba  akizungumza kabla ya kupokea masanduku yaliyotolewa
na TACAIDS kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kuboresha
huduma za VVU na UKIMWI kutoka TACAIDS.
 
 
0 comments:
Post a Comment