Wednesday, April 14, 2021

WASTAAFU WAWAASA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUJITUMA

        Watumishi waliostaafu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wamewaasa watumishi wa Umma kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na kujituma ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri na kumaliza salama safari yao ya utumishi wa Umma. 

Rai hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti katika hafla ya kuwaaga iliyoandaliwa na Katibu Tawala wa Mkoa ambayo iliyofanyika Aprili 13, 2021 Mjini Bariadi.

“Nawasihi Watumishi wenzangu mfanye kazi kwa kujituma na muwe makini katika utendaji kazi wenu ili mtoe huduma inayotakiwa kwa watu mnaowahudumia,” alisema Dkt. Mugune Maeka ambaye alistaafu utumishi wa Umma akiwa Daktari msaidizi Mkuu

“Ninawashukuru kwa ushirikiano mlionionesha siku zote nilizofanya kazi nanyi, nawaomba watumishi mtimize wajibu wenu na muwe na subira mnapokutana na changamoto mbalimbali katika utumishi wao,” alisema Gamitwe Mahaza ambaye amestaafu utumishi wa Umma akiwa Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na uzalishaji 

“Ninawashukuru sana viongozi wetu kuona umuhimu wa kutuaga baada ya kukoma kwa utumishi wetu, niwaombe watumishi mfanye kazi kwa utii na uaminifu ili muweze kumaliza vema safari yenu ya Utumishi wa Umma,” alisema Joseph Milando ambaye amestaafu watumishi wa umma akiwa Mlinzi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu, Bw. Ekwabi Mujungu amewapongeza wastaafu hao kwa utumishi wao uliotukuka kwa kuwa wakati wakiwa watumishi hawajawahi kuwa rekodi yoyote ya utovu wa nidhamu wala tuhuma zozote na kuwataka watumishi wengine kuiga mfano wao. 

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Donatus Weginah amewashukuru wastaafu hao kwa kuwa na mchango mkubwa katika kufikia ndoto ya mkoa huku akiwapongeza kwa kuwa watumishi wa mfano wenye utumishi uliotukuka. 

Wastaafu hao ni pamoja na Bw. Rauden Mwamwaja ambaye amekuwa mtumishi wa Umma kwa miaka 38 amestaafu akiwa dereva mwandamizi, Dkt. Mugune Maeka amekuwa mtumishi wa Umma kwa miaka 37 amestaafu akiwa Daktari Mkuu msaidizi, Dkt. Gamitwe Mahaza ametumikia Umma kwa miaka 36 amestaafu akiwa Katibu Tawala msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, Bw. Joseph Milando ametumika miaka 21 kama mlinzi na Bw. Leonard Malulu ambaye amefanya kazi kwa miaka 34 na amestaafu akiwa Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi. 

Katika hafla hiyo kila mstaafu alikabidhiwa cheti cha utumishi uliotukuka pamoja na fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000/=), zawadi ambazo zimetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa kwa lengo la kuwapongeza na kutambua mchango wao wakati wa utumishi wao.

MWISHO

Bw. Rauden Mwamwaja (kulia) ambaye amekuwa mtumishi wa Umma kwa miaka 38 amestaafu akiwa dereva mwandamizi, akipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Donatus Weginah akizungumza na watumishi katika hafla ya kuwaaga wastaafu iliyofanyika Aprili 13, 2021 Mjini Bariadi.

Bw. Joseph Milando ametumika miaka 21 kama mlinzi (wa pili kulia) aakipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah (wa pili kushoto) katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Dkt. Mugune Maeka (katikati) ambaye amekuwa mtumishi wa Umma kwa miaka 37 amestaafu akiwa Daktari Mkuu msaidizi, akipokea  zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Dkt. Gamitwe Mahaza(wa pili kushoto) ambaye  ametumikia Umma kwa miaka 36 amestaafu akiwa Katibu Tawala msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, akipokea  zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Bw. Leonard Malulu ambaye amefanya kazi kwa miaka 34 na amestaafu akiwa Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, akipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Bw. Leonard Malulu ambaye amefanya kazi kwa miaka 34 na amestaafu akiwa Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, akipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Bw. Leonard Malulu ambaye amefanya kazi kwa miaka 34 na amestaafu akiwa Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, akipokea cheti cha utumishi uliotukuka na zawadi ya shilingi 1,000,000/= kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.

Bw. Joseph Milando ametumika miaka 21 kama mlinzi(Mstaafu) aliyesimama, akizungumza katika katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi.
Baadhi ya watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiwa katika hafla ya kuwapongeza wastaafu, Aprili 13, Mjini Bariadi

TAZAMA PICHA MBALIMBALI KATIKA HAFLA YA KUWAPONGEZA WASTAAFU ILIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA MKUU WA MKOA, APRILI 13, 2021 MJINI BARIADI.



















0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!