Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri sita za
Mkoa wa Simiyu zimetoa shilingi 138,030,500/= kwa vikundi 122 vya wanawake kama
mikopo kutoka katika asilimia nne ya mapato ya ndani ya halmashauri, kwa ajili
ya kuwapatia mitaji ya kuanzisha na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
Hayo
yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kupitia hotuba
yake iliyosomwa kwa naiba yake na Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Bi, Manahamisi Kawega wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani
Machi 08, 2021 ambayo kimkoa yamefanyika Wilayani Maswa.
“Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, imetoa shilingi 10,000,000/= kwa vikundi 25, Halmashauri wilaya
ya Bariadi shilingi 48,000,000/= vikundi 37, Busega shilingi 16,000,000/=kwa
vikundi 16, Itilima shilingi 12,000,000/= vikundi 12, Maswa shilingi
39,200,000/= vikundi 18 na Meatu shilingi 12,830,500 kwa vikundi 14,” alisema.
Aidha,
Mmbaga amewaagiza Wakurugenzi wa Mamalaka za Serikali za Mitaa kuendelea
kutenga na kupeleka fedha asilimia nne kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi
vya wanawake kwani haina riba kuliko mikopo kutoka taasisi nyingine za kifedha.
Vile
vile Mmbaga amesema kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka 2021 “ Wanawake katika
Uongozi:Chachu ya kufikia Dunia yenye Usawa” itumike kuwawezesha wanawake
kwenye nafasi za uongozi katika mkoa wa Simiyu kwa kuwa jamii bado haijatambua
umuhimu wa kumuwezesha mwanamke nafasi za uongozi tunapoelekea kwenye Dunia ya
usawa.
Naye
Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba ametoa wito kwa viongozi
wanawake kufanya kazi kulingana na matarajio ya wanawake huku akisisitiza
wahakikishe wanatafuta ufumbuzi wa changamoto za wanawake.
Mkuu
wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera amewataka wanawake kujiamini na kujitokeza katika fursa mbalimbali za uongozi
katika jamii kwa kuwa viongozi wanawake ni wachache, hivyo kila fursa
inapopatikana wasisite kujitokeza ili kuwe na viongozi wengi wanawake katika
kuelekea dunia yenye usawa.
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Kimkoa
yaliambatana na maonesho ya shughuli za wanawake wajasiriamali, uchangiaji
damu, kutoa misaada kwa wagonjwa ambapo chama cha Wafanyakazi wa Afya na
Serikali (TUGHE) walitoa msaada wa mashuka 30 kwenye wodi ya wazazi katika
Hospitali ya Wilaya ya Maswa.
MWISHO
Mwanasheria kutoka
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(wa pili kushoto) ambaye
alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni
rasmi , akimsikiliza mjasiriamali mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea
mabanda ya maonesho Machi 08, 2021.
Baadhi ya watumishi
wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiwa wamebeba bango kwenye maandamano
ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo
nane Machi 08, 2021.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe. Tano Mwera akitoa salamu
kwa wanawake wa mkoa wa Simiyu wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani
ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08,
2021. Mwenyekiti wa UWT Mkoa
wa Simiyu,Mama Mariam Manyangu Mwera
akitoa salamu kwa wanawake wa mkoa wa Simiyu wakati maadhimisho ya siku
ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane
wilayani Maswa Machi 08, 2021.Baadhi ya watumishi
wanawake kutoka Ofisi mbalimbali za Mkoa wa Simiyu wakiwa wamebeba bango lenye
ujumbe maalum kwenye maandamano ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa
yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi 08, 2021.
Wanafunzi kutoka Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakiimba wimbo wenye ujumbe maalum katika
maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 08, 2021 ambayo kimkoa
yamefanyika katika Uwanja wa Nugzonane wilayani Maswa. Baadhi ya wanawake
wakikimbia mbio za magunia ikiwa ni sehemu ya burudani katika maadhimisho ya
siku ya wanawake Duniani Machi 08, 2021 ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja
wa Nugzonane wilayani Maswa.
Baadhi
ya viongozi na wanawake wa mkoa wa Simiyu wakicheza wimbo maalum ulioimbwa na baadhi ya walimu wa kike katika
maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 08, 2021 ambayo kimkoa
yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mwanasheria kutoka
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(wa pili kulia) ambaye
alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni
rasmi , akimsikiliza mdau katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
yaliyofanyika kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea mabanda
ya maonesho Machi 08, 2021.
Vijana wa sarakasi
wakitoa burudani wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa
yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021. Kutoka kulia, Katibu
Tawala wa Wilaya ya Maswa Bi. Agnes
Alex, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega wakiteta
jambo wakati maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika
katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021,(wa tatu kushoto) ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu Bi. Haula
Kachwamba. Baadhi ya wanawake
wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati maadhimisho ya siku ya wanawake
Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa
Machi 08, 2021. Baadhi ya wanawake
wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati maadhimisho ya siku ya wanawake
Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa
Machi 08, 2021. Baadhi ya wanawake
wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati maadhimisho ya siku ya wanawake
Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa
Machi 08, 2021.
Mwanasheria kutoka
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(wa pili kushoto) ambaye
alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni
rasmi , akimsikiliza mjasiriamali mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea
mabanda ya maonesho Machi 08, 2021. Mwanasheria kutoka
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(katikati) ambaye alimwakilisha
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni rasmi , akiangalia
baadhi ya bidhaa za wajasiriamali mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea
mabanda ya mMwanasheria kutoka
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega(wa pili kushoto) ambaye
alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni
rasmi , akimsikiliza mjasiriamali mwanamke katika maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane Wilayani Maswa alipotembelea
mabanda ya maonesho Machi 08, 2021.
Mwanasheria kutoka
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mwanahamisi Kawega ambaye alimwakilisha Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga kama Mgeni rasmi , akizungumza na mwanamke
katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa Uwanja wa Nguzo nane
Wilayani Maswa alipotembelea mabanda ya maonesho Machi 08, 2021.
Baadhi ya watumishi
wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiwa kwenye maandamano ya siku ya
wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi
08, 2021. Katibu Tawala wa Wilaya
ya Maswa,Bi. Agnes Alex akitoa salamu kwa wanawake wa mkoa wa Simiyu wakati
maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja
wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021.
Baadhi ya watumishi wanawake kutoka Ofisi mbalimbali za Mkoa wa Simiyu wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe maalum kwenye maandamano ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi 08, 2021.
Mwanasheria wa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa akitoa taarifa ya chimbuko la Siku ya wanawake wakati
maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja
wa Nguzonane wilayani Maswa Machi 08, 2021. Baadhi ya watumishi wanawake kutoka Ofisi mbalimbali za Mkoa wa Simiyu wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe maalum kwenye maandamano ya siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Machi 08, 2021.
0 comments:
Post a Comment