Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa
miezi miwili kuanzia sasa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Itilima kukamilisha ujenzi wa mabweni katika shule ya sekondari Bariadi, Nyasosi na
Itilima ili wanafunzi waliokusudiwa kukaa katika mabweni hapo wapate huduma
tarajiwa kwa wakati.
Silinde ametoa agizo hilo wakati alipotembelea shule
hizo wakati wa ziara yake Machi 05, 2021 Mkoani Simiyu yenye lengo la kukagua
ujenzi wa majengo ya miundombinu ya elimu ikiwemo mabweni, mabwalo na vyumba
vya madarasa.
Amesema Serikali haitatoa fedha nyingine kukamilisha
mabweni, mabwalo na madarasa ambayo bado hayajakamilika na haitakubali yabaki
magofu hivyo ni jukumu la Halmashauri
husika kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo hayo ili wanafunzi
waliokusudiwa kutumia wapate haki yao.
“Nimeridhishwa na kiwango cha ujenzi wa madarasa na
thamani ya fedha inaonekana ninawapongeza sana, kuhusu mabweni mhakikishe
yanakamilika na ninaahidi kurudi tena hapa mwezi Mei kuja kukagua kuona namna
mlivyotekeleza, yasipokamilika ninawaambia wazi nitawavua madaraka wakuu wa
shule na maafisa Elimu sekondari,” alisema Silinde.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima,
Bi.Elizabeth Gumbo ameahidi kukamilisha ujenzi wa bweni shule ya sekondari Itilima
ifikapo Aprili 30, 2021 huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi,
Bw. James John akiahidi kukamilisha bweni la Shule ya sekondari Nyasosi tarehe
hiyo hiyo na Mkurugenzi wa Mji wa Bariadi,Melkizedeck Humbe ameahidi
kukamilisha ujenzi Mei 15, 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi amesema
shule ya Sekondari Itilima ilipokea shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujnezi wa
bweni ambapo amebainsha kuwa baadhi ya sababu zilizopelekea mradi huo
kutokamilika kwa fedha hiyo ni pamoja na aina ya udongo uliopo katika eneo la
Ujenzi kuhitaji msingi mrefu na imara uliotumia fedha nyingi tofauti na
makadirio pamoja na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.
Pamoja na changamoto hizo Kilangi amesema Serikali
wilayani humo itahakikisha Bweni la Shule ya Sekondari Itilima linakamilika kwa
wakati ili kuwawezesha wanafunzi kupata huduma iliyokusudiwa kwao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amewaagiza wataalam
wa Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Bariadi kuhakikisha wanakamilisha
majengo yote yaliyoletewa fedha na serikali huku akimhakikishia Naibu Waziri
kuwa mabweni ya Bariadi sekondari na Nyasosi sekondari yatakamilika kwa wakati.
Katika hatua nyingine Kiswaga amewataka Wakurugenzi
wa Halmashauri za wilaya hiyo kumpelekea taarufa ya fedha zote za miradi zinazoingia
ili kamati ya ulinzi na usalama iweze kujua na kuweka utaratibu wa kuzisimamia
na kuhakikisha zinatekeleza miradi kulingana na maelekezo ya Serikali.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi akitoa
ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde
(mwenye skafu) wakati alipotembelea Shule ya Sekondari Itilima ili kujionea
maendeleo ya Ujnezi wa bweni shuleni hapo wakati wa ziara ya naibu Waziri huyo
Machi 05, 2021 mkoani Simiyu yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa
miundombinu ya elimu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David
Silinde(kulia) akielekea kukagua jengo la bweni katika Shule ya sekondari
Bariadi wilayani Bariadi wakati wa ziara yake Machi 05, 2021 mkoani Simiyu
yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akiwasilisha
taarifa ya Mkoa kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David
(kulia) wakati wa ziara yake Machi 05, 2021 mkoani Simiyu yenye lengo la
kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David
Silinde akizungumza na viongozi na baadhi ya watendaji wa Wilaya ya Itilima
wakati wa ziara yake Machi 05, 2021 mkoani Simiyu yenye lengo la kukagua
maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David
Silinde (mwenye suti nyeusi) akikagua ujenzi wa Bweni linaloendelea kujengwa
katika shule ya sekondari Nyasosi wilayani Bariadi kupitia fedha za mradi wa
lipa kulingana na matokeo (EP4R), wakati wa ziara yake Machi 05, 2021 mkoani
Simiyu yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu.
0 comments:
Post a Comment