Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde ameridhishwa na namna mradi wa ujenzi wa bwalo, vyumba viwili vya madarasa, maabara na matundu ya vyoo ulivyotekelezwa kwa viwango katika Shule ya Sekondari Anthony Mtaka iliyopo kata ya Lamadi wilayani Busega Mkoani Simiyu.
Silinde
ameyasema hayo leo Machi 06, 2021 shuleni hapo alipotembelea mradi huo wakati
wa ziara akikamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu yenye lengo la
kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo mabweni, mambwalo,
madarasa na matundu ya vyoo.
“Nimeisikiliza
hii ripoti iliyosomwa na Mkuu wetu wa shule, nimekagua madarasa, maabara
nimekagua na bwalo la chakula kwa kweli mmejenga kwa viwango vinavyoridhisha
kikubwa zaidi mmekuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali, kwa kazi iliyofanyika hapa hiyo milioni 42
iliyosomwa hapa kama bakaa mnaweza mkaitumia kukamilisha madarasa mengine
yaliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi,” alisema.
Ameongeza
kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imedhamiria kudhibiti mapato na matumizi ya fedha
za Serikali huku akiwataka watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa
wazalendo na waadilifu katika usimamizi wa fedha za serikali na kuhakikisha
wanapopewa fedha kwa aajili ya utekeelzaji wa miradi watekeleze kwa mujibu wa
maelekezo wanayopewa.
Aidha,
Silinde amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuboresha miundombinu ya
elimu kwa ajili ya kuboresha mazingira ya utoaji elimu kwa watoto wa Kitanzania
na ndiyo maana sasa hivi imejikita katika ujenzi wa mabweni bora, madarasa
bora, mabwalo bora, maabara za kisasa na matundu ya vyoo bora na kuahidi
kuwaondoa kwenye nafasi zao wale wote wenye nia ya kuikwamisha serikali.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Busega, Mhe. Simon Songe ameishukuru Serikali kwa fedha
ilizotoa kwa jili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu wilayani Busega
na kuahidi kuendelea kuzisimamia fedha hizo ili ziweze kutimiza azma ya
serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Songe
ameongeza kuwa wilaya ya Busega ina mahitaji ya shule 44 za sekondari zilizopo
zikiwa 20 na ambazo zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni zikiwa nne, hivyo
ameomba Serikali itakapoombwa fehda kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za
wananchi katika ujenzi wa shule hizo itoe kipaumbele kwa wilaya hiyo ili
kufikia lengo la kuwa na shule 44 za sekondari.
Kwa
upande wao wanafunzi wa shule ya sekondari Anthony Mtaka wanaishukuru serikali
kwa kuwajengea madarsa, bwalo na maabara jambo ambalo wamekiri kuwa litachangia
katika kuboresha mazingira yao ya kujifunzia.
“Tunaishukuru
serikali kutujengea maabara ambayo itatusaidia sana kufanya mazoezi ya vitendo
hususani kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi lakini na madarasa tuliyongewa
tunashukuru pia maana yamepunguza msongamano darasani,” alisema George Daud
kiranja Mkuu Anthony Mtaka sekondari.
“Pamoja
na kutujenge madarasa maabara na vyoo mimi ninaishukuru serikali kwa kutujengea
bwalo ambalo tutalitumia kwa matumizi mbalimbali zaidi ya kulia chakula,
tutalitumia kufanyia mikutano na midahalo; hili litakuwa mkombozi maana
tulikuwa tunafanyia vikao vyetu na midahalo chini ya miti,” alisema Sarah
Mathias mwanafunzi shule ya sekondari Anthony Mtaka.
Awali
akiwasilisha taarifa Mkuu wa Shule ya Sekondari Anthony Mtaka, Mwl. Joseph
Kazimoto amesema fedha zilizopokelewa ni shilingi 196, 600,000/= kwa lengo la
ujenzi wa bwalo, vyumba viwili ya madarasa, maabara na matundu sita ya vyoo na
mara baada ya kukamilisha kazi hizo fedha iliyobaki ni jumla ya shilingi
42,894,100/= .
MWISHO
Baadhi ya wanafunzi wa
Shule ya Sekondari Anthony Mtaka iliyopo Kata ya Lamadi wilayani Busega
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde
akizungumza alipozungumza nao shuleni
hapo wakati wa ziara yake wilayani humo Machi 06, 2021 iliyokuwa na lengo la
kukagua miundombinu ya elimu.
Sehemu ya jengo la Maabara
inayojengwa katika shule inayotarajiwa kukamilika na kusajiliwa kwa jina la Mkuu
wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Venance
Mabeyo iliyopo katika kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega.
Mbunge wa Jimbo la
Busega, Mhe. Simon Songe akizungumza na
baadhi ya viongozi na watendaji wa Wilaya ya Busega pamoja na watumishi na
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Anthony Mtaka wakati wa ziara ya Naibu Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde (mwenye skafu kulia)
wilayani humo Machi 06, 2021 iliyokuwa na lengo la kukagua miundombinu ya
elimu.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde ( mwenye skafu) akielekea kukagua
miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya elimu mara baada ya kuwasili shule
ya sekondari Anthony Mtaka wakati wa ziara yake wilayani humo Machi 06, 2021
iliyokuwa na lengo la kukagua miundombinu ya elimu.
0 comments:
Post a Comment