Monday, August 15, 2016

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUWAHIMIZA WAUMINI KUFANYA KAZI



 Na Stella Kalinga
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya Dini kutumia nafasi zao katika kuwahimiza watu wafanye kazi kwa bidii ili kuendeana na Kauli Mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU.

Kiswaga ametoa wito huo katika ufunguzi wa Mkutano wa Neno la Mungu mjini Bariadi, ulioandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kwa kushirikiana na Huduma ya New Life in Christ ya Jijini Dar es Salaam.

Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Kiswaga amesema Viongozi wa dini wana nafasi za kubwa kuwahamasisha waumini kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Mhe. Rais wetu John Pombe Magufuli ameshatoa maelekezo kuwa watu wote wafanye kazi, tena wafanye kazi kwa nguvu zao zote, katika imani hiyo hiyo Mkuu wa Mkoa wetu anasema ana imani kubwa kuwa viongozi wa dini wataendelea kuwahimiza waumini wao wafanye kazi. Ombi lake kwenu Muendelee kumuombea Rais wetu ili aweze kuliongoza Taifa hili na kutekeleza majukumu yake kwa Amani na Utulivu” 

Kiswaga amesema pamoja na kuwahimiza wananchi kufanya kazi Serikali inatambua mchango mkubwa wa Viongozi wa dini katika kupunguza Imani potofu, mauaji ya vikongwe, mauaji ya albino na kutatua migogro ndani ya familia na jamii kwa ujumla, hivyo huchangia kupunguza vitendo viovu katika jamii. 

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Wilaya amewatahadharisha wananchi na wakazi wa Bariadi kutojiingiza katika masuala ya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na kutojichukulia sheria mikononi kwa kuwaua vikongwe, kujiingiza katika maandamano yasiyo na kibali cha Serikali na akawataka kutii na kuheshimu sheria za nchi.

Aidha, Kiswaga amewataka wakazi wa Bariadi na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kufanya usafi katika maeneo yao ya kazi, biashara na makazi ili kuuweka Mkoa wa Simiyu katika hali ya Usafi.

Kwa upande wake  Askofu wa K.K.K.T Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala amesema Kanisa linaunga mkono Juhudi za Serikali za kuwafanya Watanzania waishi kwa amani kwa kuwapelekea injili, ili waendelee kuwa na uhuru wa kuabudu. 

Mkutano huo wenye kauli Mbiu ya SIMIYU KWA YESU ulifunguliwa rasmi jana katika Mji wa Bariadi na utaendelea pia katika vituo vingine 27 katika wilaya zote tano za Mkoa wa Simiyu hadi tarehe 21/08/2016.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Injili Mjini Bariadi, ulioandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kwa kushirikiana na Huduma ya New Life In Christ ya jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)

Askofu wa  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akizungumza na Wakazi wa Mjini Bariadi (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Injili, ulioandaliwa na Kanisa hilo  kwa kushirikiana na Huduma ya New Life In Christ ya jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)
Mkuu wa Jimbo la Bariadi, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mch. Harold Mkaro akizungumza na Wakazi wa Mjini Bariadi (hawapo pichani)wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Injili, ulioandaliwa na Kanisa hilo  kwa kushirikiana na Huduma ya New Life In Christ ya jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa pili kulia) akizungumza jambao na Viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Injili Mjini Bariadi, ulioandaliwa na Kanisa hilo kwa kushirikiana na Huduma ya New Life In Christ ya jijini Dar es Salaam, (kulia)(Mkuu wa Jimbo la Bariadi, Mch. Harold Mkaro  (Kushoto) Askofu wa Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala, (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)
Mwinjilisti Teddy Steven akihubiri katika Mkutano wa Injili Mjini Bariadi( (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)
Baadhi ya Wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) kutoka katika Sharika mbalimbali za Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga (hayupo pichani)akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka katika Ufunguzi wa Mkutano wa Injili, Mjini Bariadi  ulioandaliwa na Kanisa hilo kwa kushirikiana na  Huduma ya New Life In Christ ya Jijini Da es Salaam.
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Bariadi wakishangilia jambo wakatiwa ufunguzi wa Mkutano wa Injili ulioandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kwa kushirikiana na Huduma ya New Life In Christ ya jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!