Tuesday, August 23, 2016

RC SIMIYU AWATAKA VIJANA KUACHANA NA SIASA ZISIZO NA TIJA NA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MAENDELEO

Na Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  amewataka vijana wa Mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kutambua na kuchangamkia fursa za uchumi na maendeleo badala ya kujiingiza katika masuala ya siasa zisizo na tija. 
 
Mkuu huyo wa Mkoa amesema hayo katika ufunguzi wa semina ya Vijana Wajasiriamali iliyolenga kuwasaidia kutambua fursa za biashara na uchumi inayondeshwa na CLUODS Media Group kwa kushirikiana na Wataalam mbalimbali, ikiwa na Kauli Mbiu ya “FURSA 2016-Ongeza Thamani” ambayo imeshirikisha vikundi vya vijana kutoka wilaya zote tano za mkoa huo.

Mtaka amesema Serikali Mkoani humo itawachukulia hatua Wanasiasa wote watakaotaka kuwafanya vijana wa Mkoa huo kuandamana Septemba Mosi, 2016 na badala yake Serikali inawataka vijana hao kujikita katika fursa zilizopo Mkoani humo,  kwa kuwa inayo dira na malengo ya kuwasaidia vijana kujikwamua kutoka katika umaskini.

 “ Ni vizuri uwaache wanasiasa wanaotaka kufanya majaribio na Serikali watoke wao na familia zao, kwa sababu hizo nyumba wanazokaa za viyoyozi hukai wewe, kwenye magari ya viyoyozi wanayotembelea hutembelei wewe, usiwe fursa ya Wanasiasa waganga njaa”, alisema Mtaka.

Mtaka amesema azma ya Serikali katika Mkoa wa Simiyu ni kuwa kila wilaya izalishe zao moja ambalo litaitambulisha wilaya husika yaani (one product one district) ambapo alieleza kuwa, Wizara yenye dhamana na Vijana imeshatoa zaidi ya shilingi 69,000,000 kwa ajili ya Vijana wa Meatu na Maswa, hivyo akawataka  kabla ya  tarehe 14 Oktoba, 2016 Vijana wa Wilaya ya Meatu waanze kuzalisha  maziwa ya ng’ombe asilia, Vijana wa wilaya ya Maswa waanze kuzalisha chaki ambazo zitatumika katika shule za Mkoa huo mikoa mingine nchini.

Katika Tanzania ya Viwanda Serikali mkoani Simiyu imedhamiria Mkoa huo kwenye sekta ya Viwanda uwe Mkoa unaozalisha mahitaji madogo mdogo ya wananchi kama vile pamba inyotumika hospitali kufungia na kusafishia vidonda, pamba za masikioni badala ya kuagiza vitu hivyo kutoka nje ya nchi, kwa kuwa Mkoa wa Simiyu unazalisha takribani asilimia 55 ya pamba nchini

Aidha, Mtaka amesema Serikali imejipanga kuongeza uzalishaji wa pamba bora kutoka tani milioni 70 mwaka 2015/2016 hadi kufikia tani 200  mwaka 2017/2018 kwa kuwa imeweka mipango ya kuwawezesha Maafisa Ugani ngazi zote ili wawape msaada wa kitaalam wakulima walime kilimo bora chenye tija.

Akizungumza katika semina hiyo mmoja wa wawezesheshaji, Charles Ndugu amesema ili wafanyabiashara na wajasiriamali waweze kuzitangaza bidhaa na huduma wanazozitoa wajikite katika kutoa huduma bora kwa wateja,udhibiti ubora wa huduma/bidhaa, biashara zao ziwe na mwendelezo katika utoaji wa huduma na pia bidha zao ziwe na muonekano mzuri kwa wateja.

Nae Hassan Ngoma amewataka vijana wajasiriamali kutofanya biashara kwa mazoea na badala yake watafute taarifa na maarifa sahihi juu ya fursa mbalimbali za biashara wanazozifanya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds, Ruge Mtahaba amesema wao kama Clouds wamenzisha semina za namna hii wakishirikiana na Wataalam mbalimbali, kwa lengo la kuwasaidia vijana na wananchi wote kwa ujumla katika kuanzisha mawazo, kuyalea, kuyakuza na kufika mahali pa kupanuka kuwa biashara na akatoawito kwa vijana kuachana na dhana ya kusoma kwa lengo la kutaka kuajiriwa badala yake wasome wakiwa na malengo ya kujiajiri.

CLOUDS Media Group  kupitia “FURSA 2016-Ongeza Thamani” itatembelea mikoa 22 na Simiyu ni Mkoa wa tatu tangu ilipoanza kwa mwaka 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akizungumza na vijana wajasiriamali wa Mkoa huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wajasiriamali iliyofanyika Mjini Bariadi ambayo  iliyoandaliwa na Clouds Media wakishirikiana na Wataalam wengine ikiwa na Kauli mbiu FURSA 2016-Ongeza Thamani”, (kulia) Mrisho Mpoto akifuatiwa na Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media, Ruge Mtahaba (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)


:Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media, Ruge Mtahaba(wa tatu kushoto) wakiteta jambo wakati wa semina ya  Wajasiriamali iliyofanyika Mjini Bariadi ambayo  iliandaliwa na Clouds Media wakishirikiana na Wataalam wengine ikiwa na Kauli mbiu FURSA 2016-Ongeza Thamani”, ( wa kwanza kushoto ) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu),

Mwezeshaji na Mfanyabiashara Hassan Ngoma akitoa mada katika Semina ya Fursa iliyotolewa na Clouds Media kwa kushirikiana na Wataalam wengine kwa vijana na wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) ambayo imefanyika Mjini Bariadi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu).

Mwezeshaji na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Ruge Mtahaba akitoa mada katika Semina ya Fursa iliyotolewa na Clouds Media kwa kushirikiana na Wataalam wengine kwa vijana na wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) ambayo imefanyika Mjini Bariadi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu).

Mwezeshaji na Msanii Mrisho Mpoto (kushoto) akitoa mada katika Semina ya Fursa iliyotolewa na Clouds Media kwa kushirikiana na Wataalam wengine kwa vijana na wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) ambayo imefanyika Mjini Bariadi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu).

Baadhi na Viongozi na Washiriki wa Semina ya Fursa iliyotolewa na Clouds Media kwa kushirikiana na Wataalam wengine kwa vijana na wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu ambayo imefanyika Mjini Bariadi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu).

Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Fursa iliyotolewa na Clouds Media kwa kushirikiana na Wataalam wengine kwa vijana na wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu ambayo imefanyika Mjini Bariadi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu).
Mwezeshaji na Msanii wa kizazi kipya Nick wa Pili akitoa mada katika Semina ya Fursa iliyotolewa na Clouds Media kwa kushirikiana na Wataalam wengine kwa vijana na wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu ambayo imefanyika Mjini Bariadi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu).

: Mwezeshaji Charles Ndugu akitoa mada katika Semina ya Fursa iliyotolewa na Clouds Media kwa kushirikiana na Wataalam wengine kwa vijana na wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu ambayo imefanyika Mjini Bariadi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu).

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga(katikati) akizungumza na Wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa huo, kufungua semina iliyoandaliwa na Clouds Media, (kutoka kushoto), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga, Hassan Ngoma Mwezeshaji katika Semina ya Fursa.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu).

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!