Washiriki wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kikao |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila akizungumza na Washiriki wa kikao cha kuwapongeza Wanabariadi kwa kupata leseni ya Kuchimba Madini Washiriki wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amempongeza Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Kapange na Wakurugenzi Bw.Khalid Mwalami na Adrian Jungu kwa kazi kubwa ambayo wameendelea kuifanya katika sekta ya madini.
Rc.Kafulila ametoa pongezi hizo kwenye kikao cha kukabidhi leseni ya kuchimba Madini kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Bariadi mji na Bariadi vijijini, hafla iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya Bariadi.
" Nakupongeza Mkuu wa Wilaya, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bariadi mji na Bariadi vijijini , kwani Halmashauri ya Bariaji Vijijini ilikuwa dhoofu sana katika makusanyo kiasi cha kufikiria kuifuta. Lakini ndani ya miezi 6 imetoka nafasi za mkiani mpaka nafasi ya 15 kati ya halmashauri185 huku halmashauri ya mji ikishika nafasi ya 13".Amesema Kafulila.
0 comments:
Post a Comment