Mhe.Kafulila,amempongeza mjasiliamali Frank Malima, ambaye ndiye mmiliki wa kiwanda cha kuchambua na kusafisha dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akiwa ameambatana na Viongozi wengine wa Mkoa mara alipotembelea kiwanda cha kuchambua na kusafisha dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED kilichopo Mkoani Simiyu, hivi karibuni.
Akizungumzia Bw.Frank Malima, Mhe. Kafulila alieleza kuwa Bw. Malima ni mubobezi wa masuala ya madini, maarifa ambayo ameyapata nje ya nchi ikiwemo Afrika ya Kusini.
Akimshukuru, Mkuu wa Mkoa, Bw.Malima ameahidi kuwapatia kinamama mashine aina ya
BALL MILL,mashine ambayo itaongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 5 kwa
mwezi mpaka tani 100 kwa mwezi, hii ikiwa ni matumizi ya mashine moja.
Kiwanda cha kuchambua na kusafisha dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED kina uwezo wa kusafisha kilo 15-20 za dhahabu kwa siku.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kafulila pamoja na viongozi wengine katika kiwanda cha kuchambua na kusafisha dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED- Bariadi. |
0 comments:
Post a Comment