Thursday, November 18, 2021

UZINDUZI WA UGAWAJI PIKIPIKI KITAIFA KWA MAAFISA UGANI KATIKA MIKOA INAYOZALISHA MAZAO KIMKAKATI, WAFANYIKA MKOANI SIMIYU.

Akizungumza,Mkurugenzi mkuu Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga alitoa shukrani kwa Waziri wa kilimo Mhe. Adolf Mkenda kwa kukubali kuhudhuria zoezi la ugawaji wa pikipiki. 

Pongezi kwa mkoa wa Simiyu kwa kuzalisha zaidi ya asilimia 61 ya pamba yote nchini msimu huu wa kilimo.Tatizo la msingi katika sekta ya kilimo ni kupungukiwa maarifa kwa sababu ya wataalamu kutowezeshwa ipasavyo.

Mkakati wa Wizara ni kuimarisha huduma za ughani. Maafisa ughani wote watakuwa na pikipiki kwa sababu ni vigumu kwa afisa ugani mmoja asiye na usafiri kutembelea kata nzima.Hivyo leo wataalam watapewa vitendea kazi ili waweze kuwafikia wakulima.Wakulima wafuate kanuni za kilimo.Lengo la zoezi la leo ni kuhakikisha mkulima anaboreshewa kielimu. Maafisa ughani wasitumie pikipiki kama biashara.Halmashauri zinapaswa kusimamia vizuri zoezi la kilimo cha pamba ili kuongeza mapato 


Dr. Sophia Kashenge Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Mbegu za Kilimo,Tanzania, alitoa pongezi na shukrani kwa Wizara ya Kilimo kwa kutoa kipaumbele kikubwa kwa kazi ambazo zilikuwa hazipewi kipaumbele. Kazi ya Wakala wa mbegu za Kilimo ni kuhakikisha mbegu zinazogunduliwa na mtafiti zinamfikia mkulima na kuzizalisha kwa wingi ili zifike kwa mkulima kuendana na uhitaji.

Wakala wanafanya kazi kupitia mashamba kumi na nne ya mbegu ya serikali. Ombi letu kwa Serikali, ni kutuongeza mashamba kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu.

Mkoa wa Simiyu umepokea mbegu za alizeti tani 114 ambapo tani 60 zimepelekwa Halmashauri ya Wilaya ya itilima, tani 34 Meatu na tani 20 Maswa kwa ajili ya kilimo cha alizeti.Aidha, Wakala wa mbegu za kilimo wameanzisha duka la mbegu mkoa wa Si 

Akizungumza,Balozi wa Pamba Bw. Agrey Mwanri alitoa Shukrani kwa Wizara/Serikali kwa maamuzi ya kukubali mbegu zitolewe kwa mkopo. Hili ni jambo la busara kwani Wakulima watakatwa mikopo hiyo wakati wakiuza mazao yao.

Shukrani kwa Waziri Prof. Adolf Mkenda kwa kuja kutoa pikipiki. Tahadhari kwa Maafisa Ugani mnapaswa kutumia pikipiki kwa kazi iliyokusudiwa pekee. 

Nitumie fursa hii kuwashauri wakuu wa Wilaya/Mikoa kusimamia matumizi sahihi ya pikipiki hizo na kuhakikisha zinafanya kazi iliyo kusudiwa.

Kuleta vitendea kazi ambavyo watumishi wataenda kivitumia na kurahisisha kazi ya kilimo ni ukomavu wa kisiasa. 

Kila mkulima wa Pamba akimaliza kuvuna Pamba ahakikishe anatoa masalia yote ili kuhakikisha msimu mpya unapoanza yasiwepo mabaki na masalia yote ya pamba ili kukabiliana na wadudu waharibifu. 

Zoezi la kutoa masalia halijafanyika katika utimilifu kwani baadhi ya wakulima hawajatoa hivyo naomba Serikali kuwachukulia hatua. 

 M/kiti CCM Mkoa wa Simiyu Bi.Shemsa Mohamed alieleza lengo letu ni kuhakikisha Simiyu inakwenda kuwa kinara wa uzalishaji wa Pamba na kilimo cha biashara. Ombi la wakulima ni kupunguziwa makato ya (Amcos, Union, Bodi ya Pamba) pamoja na ongezeko la bei ya mbegu usiokuwa na utaratibu mzuri. 

Maafisa Ugani wanapaswa kutumia pikipiki kwa kazi ambayo Serikali imemtuma pamoja na kuhakikisha wakulima wanapata tija na kuongeza uzalishaji wa Pamba.

Amcos hazinufaishi wakulima. Pamba ni zao linalotegemewa na wakulima kuwainua ki uchumi hivyo  Amcos ziwe na utaratibu ambao mkulima atanufaika moja kwa moja.

Katibu mkuu wizara ya kilimo- Bw. Andrea Masawe,alisema ugawaji wa Pikipiki ni hatua ya utekelezaji wa kile Serikali ilichoahidi ikiwa ni kipaumbele cha tatu cha mkakati wa kuongeza tija ya kilimo nchini.

Nina imani kubwa kuwa uwekezaji uliofanyika una kwenda kuboresha huduma za ugani ili mkulima apate elimu ya uhakika ya kanuni bora za kilimo.

Maafisa ugani 258 kutoka mikoa 3 na 1018 kutoka mikoa 18, wamepata mafunzo. Mkoa wa Simiyu una maafisa ugani 134 ambao wamepata mafunzo hayo.

Tunategemea kutakuwa na mashamba darasa mawili kwa kila afisa ugani na shamba darasa moja la mfano. Uzinduzi huu ni sehemu kidogo ya zoezi kubwa la kugawa vitendea kazi kwa wakulima.Wizara imeimarisha taasisi kutoa ushirikiano kwa taasisi zake katika utendaji wa kazi.Mkoa wa simiyu umepokea pikipiki 86. 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila alieleza, Mkoa wa Simiyu ni mkoa wa kilimo. Asilimia 92 ya mkoa ni vijiji na wakazi wake ni Wakulima. 

Niwahakikishie kuwa Afisa Ugani yeyote atakayetumia Pikipiki kufanya bodaboda hatakuwa mtumishi wa Serikali katika mkoa wa Simiyu. 

Mkoa umetengeneza vikosi katika ngazi zote hivyo pikipiki hizi zitakwenda kusaidia hasa ngazi ya kijiji na kata ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa Pamba.

Utekelezaji wa azimio la Meatu la uzalishaji wa Pamba, Wizara ikiunga mkono mkakati huu itaongeza uzalishaji wa Pamba nchini. Mkoa utahakikisha watumishi ambao sio waadiilifu katika vyama vya Ushirika, Ushirika unawaondoa.Lengo la kuchukua hatua kali ni sababu ya kilio cha muda mrefu cha wakulima kudhurumiwa haki zao kwa sababu utaratibu unakiukwa huku sheria ikimbana mkulima auze katika ushirika. 

Mkoa una Amcos zaidi ya 300 hivyo mkoa unaomba kupatiwa mafunzo kwa watumishi wa Amcosi ili kuondoa mapungufu yaliyopo ambapo watumishi wanaonekana sio waadilifu kwa sababu ya kukosa maarifa.Wizara iendelee kuwezesha mikakati ya kuinua kilimo cha Pamba ambapo kwa sasa halmashauri zinabeba mzigo wa kuwezesha mikakati hiyo. 

Mkoa wa Simiyu umeteuliwa kuwa mkoa ambao unazalisha mafuta kwa kiwango kikubwa .Hivyo naoimba Wizara kuwezesha mikakati ya kuhakikisha mkoa unafikia malengo ya kuongeza uzalishaji. Mkoa utatumia shule kama mashamba darasa katika kuzalisha alizeti na kila shule itakuwa na mshamba darasa ya Alizeti pamoja na Pamba. Mkoa unahamasisha vilimo mbalimbali vya biashara kwenye kila wilaya.

Matumaini yetu ni kuwa mkoa wa Simiyu utaendelea kuwa karibu na Wizara kwa sababu m 92% ni wakulima na ni mkoa wa mfano katika kilimo. 

Akizungumza, Waziri wa kilimo Mhe.Prof. Adolf Mkenda, alisema kugawa pikipiki ni zoezi la kurudisha hadhi ya maafisa ugani. Nimpongeze mkuu wa Mkoa kwa jitihada za kuhakikisha anaongeza tija kwenye kilimo katika Mkoa wa Simiyu.Kama hatutawathamini Madaico na Maafisa ugani hatutafikia kile kilichoagizwa na ilani ya chama cha mapinduzi 

Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mkulima anapata kilo zaidi ya 1000 kwa ekari kwenye zao la Pamba.Tija ikiwa ndogo wanapata shida kwenye uzallishaji wa malighafi katika viwanda. Lengo kubwa la kilimo ni kupunguza bei ya mazao katika nchi yetu na kuongeza kipato cha wakulima. Hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha inamuwezesha mkulima kuzalisha mazao mengi zaidi ili hata kama bei ya mazao itakuwa ndogo mkulima bado atapata faida. Tunataka hata Bei ya mazao ikishuka lakini kipato cha mkulima kiongezeke.Hii inawekana kwa kuongeza tija ya kilimo. 

Changamoto kubwa kwenye kilimo ni tija. Baada ya utafiti wa kilimo bora na kupata mbegu bora za pamba kwa sasa tunaendelea na kuboresha kazi za ugani. Afisa ugani anajukumu la kupeleka matokeo ya utafiti kwa wakulima na kufundisha matumizi ya mbegu bora. Maafisa ugani wanajukumu la kuwafundisha wakulima mabadiliko ya hali ya hewa ili waweze kulima mazao yanayokabiliana na ukame. 

 Hatuwezi kupuuza huduma za ugani tukabaki salama Hakuna maafisa ugani wa kutosha, nchi ina maafisa ugani 6704 sawa na asilimia 32.6 uhitaji ukiwa ni maafisa ugani 20538. Hakuna Vitendea kazi vya kutosha kwa wasimamizi wa shughuli za ugani na ushirika (Daico) hawana vitendea kazi kama magari na hakuna bajeti ya kuwawezeaha kuendesha shughuli za ugani katika ngazi zilizo chini yao. Kuwapatia mafunzo maafisa ugani ili kurejesha kilimo cha kisasa . 

 Makusanyo ya mapato ya Halmashauri nyingi yanategemea kilimo, licha ya kuwa wasimamizi wa kilimo hawapewi kipaumbele cha mahitaji yao katika kuwawezesha kufanya kazi yao. Halmashauri hutenga fedha kwa ajili ya maafisa ugani, Wizara itatoa mafuta kwa msimu huu wa kilimo pamoja na vipuli baada ya msimu huu wa kilimo Halmashauri zitaendelea na zoezi hilo. 

 Niahidi; Maafisa ugani kufufua mashamba darasa pamoja kupatiwa mafuzo rejea. Maafisa ugani kwa mikoa mitatu kununuliwa simu janja kwa ajili ya kujaza taarifa za wakulima wanapo watembelea wakulima kutatua changamoto za wakulima Bodi zote za mazao zitanunua pikipiki kwa ajili ya kuboresha huduma za ugani. Maafisa ugani wanapaswa kutunza pikipiki vizuri. Wakulima wazingatie kung'oa mabaki ili kumaliza magonjwa ya pamba. Ambaye hajang'oa masalia atachukuliwa hatua za kisheria. 

Mwisho.

Waziri wa Kilimo Mhe.Prof. Adolf Mkenda akifanya uzinduzi wa Kitaifa wa Ugawaji Pikipiki kwa Maafisa ugani katika mikoa inayozalisha Mazao ya Kimkakati,

Picha za baadhi ya pikipiki zilizogawiwa kwa maafisa Ugani, jumla ya pikipiki 86 ziligaiwa kwa maafisa Ugani.


Picha za Viongozi baada ya uzinduzi wa ugawaji Pikipiki

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca  Kayombo akijaribu Pikipiki zilizogawiwa kwa maafisa uganiWakuu wa Wilaya za Dodoma wakipokea mbegu na mafuta ya alizeti kutoka kwenye duka la Wakala la mbegu, duka ambalo limefunguliwa Mkoani Simiyu.Mbegu hizo zilitolewa na Waziri wa kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!