Wednesday, November 17, 2021

MKOA WA SIMIYU KUWA KATI YA MIKOA MITANO ITAKAYONUFAIKA NA MRADI WANNE WA TASAF (TPRP IV) .

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuzindua Utekelezaji wa awamu ya Nne ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Tanzania (TPRP IV), na Viongozi na watedaji wa Mkoa wa Simiyu, Mkurugenzi Mtendaji wa TASA,  Bw.Ladislaus Mwamanga,alisema kuwa lengo la kikao kazi hicho ni kuzungumza na Viongozi na watendaji wa Mkoa wa Simiyu juu wa utekelezaji wa awamu ya nne ya mradi wa kupunguza Umaskini Tanzania ambapo pamoja na hayo mada mbalimbali kuhusu utaratibu wa kutuma fedha, majukumu  ya wadau wa ngazi zote yatawasilishwa.

 Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa mitano nchini Tanzania itakayonufaika na mradi wa (TPRP IV) ambao kwa ujumla wake utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 50 Milioni. Mkoa Wa Simiyu unategemea kunufaika kwa takribani Tsh. 24.3Bln.

 Meneja miradi TASAF Bw. Paul Kijazi akiwasilisha mada alieleza kuwa TASAF imekuwa ikifanya miradi mbalimbali ya kupunguza umaskini nchini Tanzania ulifanyika. Mradi wa nne wa TASAF utahusisha mikoa 5 na wilaya 33.Mradi huo utakuwa na thamani ya USd. 50 mln. Aidha Bw.Kijazi alieleza kuwa miradi ya aina tatu ndio itakayotekelezwa ikiwa ni pamoja na;Miradi ya Jamii, miradi ya kuongeza kipato na miradi ya kutoa ajira ya muda kwa kaya za walengwa.Tathimini za miradi hiyo zitakuwa zikifanyika kila baada ya miezi sita ya kwanza baada ya mradi kuanza. 

 Aidha Bi.Sekela Mwakatumbula aliwasilisha mada kuhusu utaratibu wa kutuma Fedha iliwasilishwa ambapo TASAF waliwaeleza viongozi na wadau kuwa TASAF hutuma fedha kwa wakati na kuhakikisha kuwa mradi unatekelezwa kwa kipindi kilichopangwa.Fedha inayotolewa kwa mradi inatakiwa itumike kwa mradi husika na si vingenevyo, ni vyema wanakijiji wakahusishwa katika miradi kwani wafadhili hupenda kuzungumza na wanakijiji wenyewe. Asilimia 88 ya fedha hutolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi,asilimia 1 ya fedha huenda kwa Katibu Tawala, ambazo hutumika kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji, aidha viongozi walishauriwa kutembelea miradi wakiwa na wataalam. Asilimia 8.5% ya fedha hizo hupelekwa Halmashauri, 3.5% hutolewa mapema kwa ajili ya kuibua na kutathimini miradi,na 5% huwasilishwa baadae. Asilimia 1.5 hutumwa katika kata kwa ajili ya usimamizi wa utekelezaji wa miradi.Baada ya kupokea fedha hizo ni muhimu barua na stakabadhi zikatumwa kwa wakati. 

 Bw. Abdulmariki Shaaban aliwaeleza Viongozi na Wataalamu walielezewa majukumu yao mbalimbali ikiwa ni pamoja na majukumu ya TASAF Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Bw. Donatus Weggina aliwafahamisha Viongozi wa TASAF na wataalam kutoka Simiyu kuwa kama Mkoa tutazingatia taratibu zote, tutahakikisha taarifa za kila robo mwaka zinatolewa kwa wakati na kwa usahihi .Aliwaasa viongozi wanapokwenda kwenye utekelezaji wawe na ushirikiano na umoja.

 Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo aliushukuru uongozi wa TASAF na hasa Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia mkoa wa Simiyu kuwa miongoni mwa mikoa mitano itakayonifaika na (TPRP IV) na kupokea kiasi cha takribani Tsh. 24.3bln zitakazotumika kwa kipindi cha mika mitano. Bi.Kayombo aliipongeza TASAF kwa kuongeza posho ya watenda kazi kuanzia Tsh. 2500/= hadi Tsh.3000/= kwa siku.Aidha Katibu Tawala huyo aliwapongeza watoa mada kwa kuwasilisha mada nzuri.Aliwaahidi TASAF kuwa, akiwa mtemndaji mkuu atahakikisha kuwa fedha na miradi inatakelezwa , inasimamiwa na kukamilishwa ipasavyo.#

Mwisho.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF -Bw.Ladislaus Mwamanga akizungungunza wakati wa kikao  kikao kazi cha kuzindua Utekelezaji wa awamu ya Nne ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Tanzania (TPRPIV)


Picha ya pamoja ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na TASAF



Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo, akizungumza na Viongozi na wadau mbalimbali waliohudhuria  kikao kazi cha kuzindua Utekelezaji wa awamu ya Nne ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Tanzania (TPRP IV),katika ukumbi wa Bariadi Conference- Bariadi Simiyu.




Baadhi ya Wadau walioshiriki  kikao kazi cha kuzindua Utekelezaji wa awamu ya Nne ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Tanzania (TPRP IV)

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!