Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.David Kafulila amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange, Mkurugenzi wa Bariadi Bw.Khalid Mwalami na timu yake pamoja na viongozi wa shule alizozikagua kwa usimamizi mahiri.
Mhe Kafulila alitoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambapo zaidi ya asilimia 90 ya majengo yake yamefikia hatua ya kupauliwa.
Akiwa ameridhishwa na kazi hiyo,Mhe. Kafulila amepongeza kasi ya Ujenzi wa madarasa katika Wilaya ya hiyo na kusema, Wilaya hiyo ni mfano wa kuigwa na wilaya zingine zote.
Aidha Mkuu wa Mkoa amempongeza na kumtolea mfano Mkuu wa shule ya sekondari Mbiti, Bi. Salome Bulenge, ambaye pamoja na changamoto zingine, shule yake ndio ya kwanza kufikia hatua ya upauaji.
Ikiwa ishara ya kuonyesha kwamba ujenzi umefikia hatua ya kupaua, wakiwa katika shule ya Sekondari Mwamlapa ,Mhe.Kafulila akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Kapange walinyanyua bati na kumkabidhi fundi ujenzi .
Mhe. David Kafulila akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Lupakisyo Kapange wakijadili jambo |
Rc. Kafulika akiwa na Dc. Kapange wakinyanyua bati ikiwa ni ishara ya kuonyesha ujenzi umefikia hatua ya Upauaji |
0 comments:
Post a Comment