Saturday, November 20, 2021

"Tokeni Maofisini Nendeni Site Mkaangalie Hali ya Ujenzi" - RC. KAFULILA


Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu Mhe. David Kafulila akitembelea Miradi ya Ujenzi wa Shule za Miradi ya Uviko-19Mkuu wa Mkoa Mhe. Kafulila akikagua kiasi cha Zege 

Mkuu wa Mkoa Akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya Itilima Mhe. Faiza SuleimanMkuu wa Mkoa akiwa ameambataka na viongozi mbalimbali wakikagua miradi ya Ujenzi wa Shule za 
Uviko-19, Wilayani Itilima hivi karibuni


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila, amewataka viongozi wa Wilaya ya Itilima  pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kuongeza ufuatiliaji katika ujenzi wa madarasa  ya Uviko-19 kwani Wilaya hiyo bado ipo nyuma kwa kiwango kikubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mhe.Kafulila ameyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya miradi ya ujenzi wa madarasa kwa kutumia fedha za Uviko-19, wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa hayo hivi karibuni. 

“Mpaka sasa mlitakiwa muwe mmefikia asilimia zaidi ya 50, lakini mpo asilimia 20, hii kasi ni ndogo sana, ongezeni kasi tokeni maofisini nendeni site mkaangalie hali ikoje kama kuna matatizo mtatue. Mkuu wa Wilaya unatakiwa kuanzisha mkakati wa kujenga usiku na mchana, tafuteni taa, kila sehemu ambapo wanajenga waambieni wajenge usiku na mchana. Waalimu na Wasimamizi, simamieni kwa umakini na haraka ili hayo majengo yajengwe kwa kiwango bora, thamani ya pesa iwepo lakini pia  msiache kuchukua hatua kwa wabadhilifu..”Amesisitiza Mhe. Kafulila.

Akitoa taarifa kuhusu kuchelewa kwa miradi hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Faiza Suleiman ameeleza kuwa sababu ya kuchelewa kwa ujenzi wa miradi hiyo imetokana na kuchelewa kupata  vifaa ikiwa pamoja na vifaa kuchelewa kufika kwenye maeneo husika kutokana na changamoto ya barabara.Aidha Mhe.Faiza alieleza kuwa ujenzi wa miradi hiyo umefikia asilimia 20 na upo usawa wa msingi katika maeneo yote. 

Mwisho

 

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!