Ku
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na Wadau wa Sekta ya afya
Katibu Tawala Bi. Prisca Kayombo akiwatambulisha Viongozi Mbalimbali waliofuatana na mkuu wa mkoa
Wadau wa sekta ya afya wakijiandaa na kikao kazi
Wadau wakisikiliza mada wakati wa Kikao kazi
Kufuatia taarifa ya tathimini kuonesha usimamizi duni sekta ya Afya, RC Kafulila amelekeza kuandaliwa mikataba ya usimamizi kati ya RMO na DMOs, RAS na DEDs na yeye mwenyewe RCs a DCs ili kuhakikisha wilaya na halmashauri zinasimamia sekta ya afya kikamilifu.
Maelekezo hayo ameyatoa kufuatia tathimini ya usimamizi wa sekta ya afya kuonyesha kuwa kwa muda mrefu usimamizi wa Kamati za Afya Wilaya ( CHMT) ni dhaifu, wakurugenzi na wakuu wa wilaya hawajawa na msukumo wa kutosha kuhakikisha usimamizi.
Aidha Mhe. Kafulila ameagiza KUVUNJWA kwa Kamati za usimamizi wa huduma ya Afya (CHMT) itakayoshindwa kusimamia sekta ya afya katika halmashauri husika. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo kufuatia taarifa ya tathimini ya robo mwaka kuonyesha kuwa CHMT zote mkoani Simiyu kwa kipindi kirefu zimekuwa na usimamizi dhaifu hata kusababisha vifo kizembe.
0 comments:
Post a Comment