Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amewataka Wakandarasi na Local fundi wa miradi ya maji mkoa wa Simiyu kutekeleza miradi ya maji kwa uadilifu na wakati. Mhe. Kafulila ameyasema hayo wakati wa hafla ya kusaini mikataba 24 kati ya RUWASA na wakandarasi na RUWASA na Local Fundi.
Akizungumza katika hafla hiyo meneja wa RUWASA- Simiyu Eng. Mariam Majala amesema kuwa baada ya kuanzishwa kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini,mkoa wa Simiyu unaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji 53 katika Wilaya za Busega, Meatu, Maswa, Itilima na Bariadi, aidha kati ya miradi 53, miradi 31 ni mipya, miradi 10 ya upanuzi, miradi 9 ya ukarabati na miradi 3 ya ukamilishaji. Eng Mariam ameeleza kuwa miradi yoye hiyo 53 inatekelezwa kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account).
Akieleza kuhusu usainishaji wa mikataba mipya 24, Eng.Mariamu ameeleza kuwa "Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) leo tunatarajia kutia saini ya mikataba 24 kati ya 36 yenye gharama ya Tsh. 6.9bln. Mikataba 12 ni ya Wakandarasi na mikataba 12 ni ya Local fund. Aidha mikataba ya miradi 4 inatarajiwa kusainiwa na RUWASA makao makuu na mikataba ya miradi 8 itasainiwa katika awamu ya pili mara baada ya taratibu za ununuzi kukamilika". Meneja RUWASA Simiyu amebainisha kuwa mikataba yote iliyosainiwa 22/12/2021 itafanya kazi kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari, 2022 hadi June 2022. Baada ya kukamilika kwa miradi hiyo Mkoa wa Simiyu unatarajia kuongeza vituo vya kuchotea maji 143 ambavyo vitahudumia wananchi wapatao 35,750 na kufanya idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama kwa maeneo ya vijijini mkoani humo kufikia 1,185,035 sawa na asilimia 73.6.
Akizungumza, changamoto zinazowakabili Watanzania,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, ameeleza kuwa utafiti uliofanywa 2008 kupitia kura za maoni,ulionyesha kuwa kati ya matatizo makunbwa manne yanayowasumbua Watanzania, tatizo la pili lilikuwa maji, wakati tatizo la nne likiwa rushwa.Hii inaonyesha kuwa suala la maji ni suala ni suala muhimu sana. Hivyo uamuzi wa kuanzisha RUWASA ulikuwa uamuzi sahihi.
Mkoa wa Simiyu una idadi ya watu wapatao 1.9ml, kati ya hao ni watu 1.14 mln sawa na 67.22% ndio wanaopata maji safi na salama. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 ongezeko la upatikanaji wa maji ni lita 1,833,400 sawa na 6.4%. Ni imani yangu kuwa kwa kusaini hii mikataba ya miradi 24 yenye thamani ya 6.9bln.Upatikanaji wa maji katika mkoa wa Simiyu utaongezeka kutoka 67.22% kufikia 73.6%.Lengo letu ni kufikia 85%.Hali hii inaonyesha waziwazi kuwa fedha za maji sio tatizo bali utekelezaji ndio mgogoro.
"Wito wangu kwa wakandarasi na Local Fundi, tekelezeni miradi hii kwa uadilifu na kwa wakati.Kwani kwa kufanya kazi kwa wakati au hata chini ya wakati na kwa ubora mtakuwa mmejitangaza zaidi. Halmashauri taarifa kuhusu masuala ya maji, umeme, Pamba,ni taarifa muhimu kwenye vikao na ziwe zinatolewa kwenye kila kikao cha madiwani. Madiwani wanatakiwa kuwa nazo, na hii itaongeza umaarufu wa RUWASA". Amesisitiza Mhe.Kafulila.
Maji ni kitu muhimu sana katika mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu.Miaka miwili iliyopita upatikanaji wa maji Mkoani Simiyu ulikuwa 40.5%, Kufikia June 2022 upatikanaji wa maji Simiyu utakuwa 73.6%. Hii inaonyesha wazi kuwa tunaweza tukafika zaidi ya 90%. Pongezi kwa kazi nzuri mnayofanya RUWASA. Hongera Meneja RUWASA kwa uwazi. Hii inaongoza uwajibikaji. Ni imani yangu kuwa upatikanaji wa watoa huduma ulizangatia mchakato,sheria, kanuni na taratibu.Hivyo nendeni mkapige kazi na kazi iwe kwenye moyo na kiganja chako.
Kwenye hii Tsh.6.9bln,toeni hata misaada kwa jamii (CSR) kwani nyie ni wawekezaji. Mkalipe Kodi zote mnazotakiwa kulipa kwa mujibu wa sheria hii ni pamoja na Service levy,malipo ya service levy yalipwe kwa Halmashauri husika.Ushuru ni vitu ambayo vipo kisheria na vilipwe. Simiyu ni yetu pamoja hivyo ni lazima tuijenge.Nawakumbusha wajibu wenu na muende mkatende, kafanyeni kazi.Lengo ni moja kumtua mama ndoo kichwani.
Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed, aliwapongeza RUWASA kwa kazi nzuri na kuwakumbusha wakandarasi na Local Fundi kuwa kazi waliyopewa ni ya miezi 6 tu."Kama Chama tutaanza kukagua miradi yote mwezi 3.Miradi hii ikamilike kwa wakati. Ni matarajio yetu kuwa kama ahadi iliyotolewa kwenye Ilani ya chama kuwa ili ifikapo 2025, 85% ya watu wote kutumia maji safi na salama itimie
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Njalu Silanga, amesema, kikao hiki kimehusisha Waheshimiwa wabunge, viongozi wote wa Chama na Serikali, hivyo makandarasi kumbukeni kwamba mmesaini mikataba mbele yetu na tunatarajia mtafanya kazi vizuri, tutawapa ushirikiano, hatuhitaji malalamiko, tunataka kazi ifanyike.
Aidha, Mbunge wa Meatu Mhe. Leah Komanya, alitoa shukrani kwa tukio hili la usainishaji mikataba kwani ni la mara ya kwanza na kubwa zaidi yote mikataba 24 kusainiwa Mara moja. Mhe.Komanya aliwafahamisha washiriki wa hafla hiyo kuwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais alianzisha kampeni ya kumtua mwanamke ndoo kichwani, kampeni ambayo akiwa Rais ameitekeleza kwa kuagiza 20% fedha za UVIKO-19 ziende kwenye miradi ya maji.Mhe Komanya amewataka wananchi wote kulinda miundo mbinu na vyanzo vya maji
Wakizungumza, Wakuu wa Wilaya ya Maswa, Itilima na Busega waliishukuru RUWASA kwa huduma ya maji inayopatikana katika halmashauri zao, na kueleza kuwa kuna baadhi ya maeneo upatikanaji wa maji ni wa 65% tu, na hivyo ni matumaini yao kuwa kwa usainishaji huu wa mikataba 24 ya maji kati ya RUWASA na Wakandarasi pamoja RUWASA na Local Fundi,upatikanaji wa maji utaongezeka na utekelezaji wa miradi hiyo utafanyika kwa mujibu wa ratiba, huku wakizingatia ubora, kwani kiasi cha fedha zilizoelekezwa kwenye miradi hiyo si ndogo.Wakuu wa Wilaya hizo waliwahakikishia wakandarasi na Local Fundi kuwa wako pamoja nao na kuwahakikishia ushirikiano wao.
Mwisho
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na washiriki wa hafla ya kusaini mikata 24 ya RUWASA,.Kulia KUU ya Mkoa na baadi ya wafanyakazi wa RUWASA Simiyu |
Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akichangia jambo |
Mwenyekiti wa chama cgha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed akisisituiza jambo wakati wa hafla ya kusaini mikataba 24 ya RUWASA |
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria akichangia hoja |
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faiza Seleman alichangia hoja kulia kwake,ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge |
Wakandarasi na Local Fundi wakisikiliza yanayojiri wakati wa hafla ya kuaini mikataba 24 ya RUWASA |
0 comments:
Post a Comment