Tuesday, December 28, 2021

RC KAFULILA ALIA NA KAMPUNI YA UJENZI YA CHICCO .

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila akizungumza wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika leo Katika Ukumbi wa Bariadi Conference Centre, mjini Bariadi- Simiyu. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, akieleza kutokuridhishwa kwake na wakandarasi na hivyo kuagiza kufutwa kwa zabuni zilizotolewa kwa kampuni 7
Aliyesimama ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akichangia jambo, Kushoto Mbunge wa Vijana Mkoa wa Simiyu Mhe.Lucy Sabu. Kulia Mbunge wa Maswa Mashariki Mhe. Stanlaus Nyongo.

Aliyesimama Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo, akichangia hoja , aliyekaa kulia Mbunge wa Meatu, Mhe.Leah Komanya

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa,Eng.John Mkumbo, akitoa  taarifa ya Mtandao wa Barabara na jinsi ujenzi wa barabara unavyoendelea mkoani Simiyu, kwenye kikao cha barabara kichofanyika leo mjini Bariadi

MKUU wa Mkoa wa Simiyu,David Kafulila ameonyesha kutoridhishwa na kitendo cha Kampuni ya ujenzi wa barabara ya CHICCO ya nchini China kupewa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya lami ya Mchepuko(By Pass)ya Km 11 ya mjini Maswa.

Akizungumza leo kwenye kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi,amesema kuwa atawasiliana na Waziri wa ujenzi na Uchukuzi, Mhe.Prof. Makame Mbarawa kupata maelezo kuhusu uhalali wa kampuni ya Ukandarasi wa Barabara CHICCO kupewa kandarasi ya ujenzi huo.

Amesema kampuni hiyo awali  ilipewa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Km 57 kutoka Mwighumbi hadi Maswa kwa gharama ya Sh Bilioni 75 lakini wakajenga chini ya kiwango na kutakiwa kuirudia upya kipande cha barabara chenye urefu  wa Kilomita 15.Mwisho.

 RC.Kafulila alibaini kujengwa kwa kiwango cha chini barabara hiyo mara baada ya kutembelea ujenzi huo Mwezi Juni mwaka huu na kuagiza maeneo yote ambayo ujenzi haukukidhi viwango kurudiwa na hadi sasa mkandarasi anaendelea na kazi ambayo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!