Thursday, August 24, 2017

WAKURUGENZI WATAKIWA KUSIMAMIA IDARA YA ARDHI KUHAKIKISHA INAPIMA MAENEO NA KUTOA HATI

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula  amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Simiyu  kuwasimamia watumishi wa Idara ya Ardhi na kuhakikisha wanapima maeneo  na kutoa hati miliki kwa wananchi.

Mhe.Mabula ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu ambayo imelenga kufuatilia utekelezaji wa maelekezo mbalimbali aliyoyatoa wakati wa ziara yake Novemba 2017, mwenendo wa ukusanyaji wa kodi za ardhi na  kukagua Jengo la Kanda ya Ardhi Simiyu itakayohudumia Mikoa ya Simiyu,Shinyanga na Mara,

“Mtumishi aliyeajiriwa kama surveyor (mpima ardhi) hana sababu za kukaa ofisini kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 9:30 alasiri wakati kazi zake nyingi ziko uwandani; Mwisho atajikuta amepima viwanja 58 mwaka mzima, maana yake ni kwamba atakuwa hajajua wajibu wake, wakurugenzi badilikeni katika kuwasimamia watumishi wa sekta ya ardhi” amesema Mabula

Amesema ikiwa Watumishi wa Idara ya Ardhi wakitimiza wajibu wao Ardhi ikapimwa, wananchi wakapewa hati miliki ya maeneo yao ya viwanja na mashamba;  migogoro itapungua, Serikali itakusanya maduhuli kupitia kodi ya Ardhi na uendelezaji wa miji utafanyika katika mpango mzuri

Pamoja na kupima maeneo na kutoa hati miliki, Mhe.Naibu Waziri amesema Idara ya Ardhi inapaswa kuhakikisha wananchi waliomilikishwa maeneo wanajenga kwa kuzingatia sheria Namba 8 ya mwaka 2007 ya Mipango Miji, ili kuepukana na ujenzi holela unaopelekea kuwa na miji isiyopangwa.

Aidha, Mhe.Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, amesisitiza maeneo yote ya Taasisi za Serikali yapimwe na kutolewa hati miliki ili kuyalinda na uvamizi.

Sanjali na hilo, Mhe.Naibu Waziri amewataka wataalam wa Ardhi kukusanya maduhuli ya Serikali yatokanayo na kodi za ardhi kwa kutumia mifumo ya Kielektroniki iliyowekwa katika kufuatilia na kuhakikisha wananchi wote wanaostahli kulipa kodi ya ardhi wanalipa kwa wakati.

Naibu Waziri ameelekeza Kamati za Halmashauri zinazosimamia Ardhi zihakikishe zinaifanya agenda ya Makusanyo ya maduhuli kuwa ya kudumu katika vikao vyao vya kila robo, ili kila wanapokutana itolewe taarifa ya hali ya makusanyo, wananchi waliopewa notisi na wale wanaotakiwa kupelekwa katika mabaraza ya Ardhi ya Wilaya kwa kushindwa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.

Akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya Bariadi Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Festo Kiswaga amesema Halmashauri zote mbili zinazounda Wilaya ya Bariadi zinaendelea na kuhamasisha wananchi kupima maeneo yao na kupata hati miliki ili kuongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya Ardhi, ambapo Halmashauri ya Wilaya Bariadi pekee kwa mwaka 2017/2018 inatarajia kupima viwanja 2400 katika Vituo vya Kibiashara vya Nkololo,Dutwa na Ngulyati.

Naye Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo amesema Mtalaam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amefika Mkoani Simiyu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji wa kodi za Ardhi,  kwa watumishi wa Halmashauri zote ambao utawawezesha kutengeneza ankara (bill) ya makusanyo ya kodi na tozo zote.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshukuru Wizara ya Ardhi kwa kuona Umuhimu wa kuanzisha Kanda ya Ardhi ya Simiyu na akaomba Wizara ifanye utaratibu wa kumleta Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Maswa kutokana na aliyekuwepo kasimamishwa kazi, hali iliyopelekea mashauri mengi kutofanyiwa kazi.

Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses amesema kuanzia mwezi Septemba 2017 atakuwepo Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Maswa  ambaye atasikiliza kesi, ambapo pia ameleeza kuwa Wizara ina mpango wa kuanzisha mabaraza mawili ya Ardhi na Nyumba katika Wilaya ya Bariadi na Busega ambayo yataanzishwa muda wowote baada ya kupatikana majengo kwa ajili ya Ofisi.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) yuko katika ziara ya siku mbili Mkoani Simiyu ambapo akiwa Mjini Bariadi amefanya kikao na  Viongozi, wataalam wa Ardhi na Watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Mji Bariadi na Halmashauri ya Wilaya Bariadi kilichofanyika Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili kushoto)akizungumza na viongozi, watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Bariadi(kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) kuhusu jengo lililoandaliwa kwa ajili ya Ofisi ya Ardhi Kanda ya Simiyu ambayo inatarajia kuanza kazi hivi karibuni, ambayo itahudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)azungumze na Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Bariadi(hawapo pichani) kabla ya kuanza ziara yake Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)azungumze na Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Bariadi(hawapo pichani) kabla ya kuanza ziara yake Mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akiwaasilisha taarifa ya Wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto)wakati akiwa katika Ziara ya siku Mbili Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akichangia hoja katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb), viongozi, watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi, kilichofayika mjini Bariadi  wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo  Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akichangia hoja katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb), viongozi, watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi, kilichofayika mjini Bariadi  wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo  Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) wakati alipotembelea Ofisi ya Idara ya Ardhi ya Halamashauri hiyo kujionea namna inavyokusanya mapato yatokanayo na Ardhi, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao mjini Bariadi.
Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao mjini Bariadi.
Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)  kuhusu eneo la uwanja wa ndege wa Kidulya lililokuwa limevamiwa na mwananchi mmoja na namna Serikali ilivyolishughulikia, wakati alipolitembelea eneo hilo akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Melkizedek Humbe(kulia) akimweleza  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)  hatua zilizochukuliwa na Halmashauri dhidi ya mwananchi aliyevamia eneo la uwanja wa ndege Kidulya, wakati alipolitembelea eneo hilo akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji, Ndg.Speratus Boniphace akichangia hoja katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi, kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo Mkoani Simiyu.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Ardhi Mkoa na Wilaya na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea eneo la Uwanja wa Ndege wa Kidulya Mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Mtaalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg. Martha Zongo hoja katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi, kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Msaidizi ehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Sekretarieti ya Mkoawa Simiyu(ambaye alimwakilisha Katibu Tawala Mkoa) akiwatambulisha viongozi na watumishi mbalimbali walioshiriki katika ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bariadi na baadhi ya wataalam wa Ofisi ya Ardhi Kanda ya Ziwa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji Bariadi, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja wakuu wa idara wa Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Bariadi, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!