Askofu Mkuu wa Kanisa
la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin
Lekundayo ameongoza viongozi na mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada
maalum ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na
kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi la Mtaa wa Ntuzu lililopo Bariadi mjini
ambapo Waumini wa kanisa hilo pamoja na
wengine kutoka mkoa wa Mwanza na Mara wamewakilisha waumini wengine hapa
nchini, ambapo ibada hiyo imehudhuriwa pia na viogozi wa Chama na Serikali
akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye amemwakilisha Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
“Nilikuwa naangalia takwimu za hali ya janga la
Corona ilivyo duniani leo asubuhi (Desemba 05, 2020) hadi sasa zinaonesha watu
66,281,000 wamepatwa na Corona, waliokufa mpaka sasa 1,525,294 ikiwa ulikuwa
umechukulia kiurahisi, hizi takwimu zikuamshe kwamba Mungu ametupendelea sana
Tanzania tunamshukuru sana Mungu kwa niaba ya wenzetu,” alisema Dkt. Lekundayo.
Awali akitoa mahubiri kabla ya maombi hayo pamoja
na kuwasihi waumini kumshukuru Mungu kuwapitisha katika janga la Corona, Askofu
Lekundayo pia ametoa wito kwa waumini kuendelea kumshukuru Mungu pia kwa namna
ambavyo amelipitisha Taifa katika Uchaguzi Mkuu, huku akisisitiza umuhimu wa
kufanya jambo ambalo litabaki kumbukumbu yao juu ya neema ya Mungu katika
masuala hayo.
Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga amesema Tanzania kupitishwa katika Janga la Corona haikuwa bahati bali
ni neema ya Mungu, hivyo akawashukuru viongozi wa Dini kwa kuliombea Taifa kwa
juhudi na Mungu akajibu.
Aidha, Kiswaga amesema Serikali inaendelea
kuheshimu mchango wa kanisa na itaendelea kushirikiana nalo katika majukumu
yake ya kitume na kimaendeleo, huku akitoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea
kuliombea Taifa na viongozi wake ili waweze kufanya kazi kwa manufaa na ustawi
wa Watanzania.
“Katika neno la Mungu kuna habari ya wale
wakoma kumi ambao waliponywa na Bwana Yesu lakini aliyerudi kushukuru ni mmoja
tu, ninaamini maombi haya ya shukrani yaendelea kuiponya nchi yetu na majanga
ambayo yanaonekana kwa macho na ambayo hayaonekani,” alisema Kiswaga.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Samweli
Kiboye amesema kuna baadhi ya watu
waliobeza Mhe Rais alivyotangaza
kumtanguliza Mungu kwa kutangaza siku tatu za kuliombea Taifa ili
aliponye Taifa na Janga la Corona lakini
baada ya kuona matokeo ya maombi naamini wameona kuwa maamuzi yake yalikuwa
sahihi.
MWISHO
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akihubiri katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha
Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika
Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo
hapa nchini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo, viongozi wa Serikali na
viongozi wa Chama, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha
Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa
amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika
Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo
hapa nchini.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato
wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la
Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini,
iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba
05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa
kanisa hilo hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David Makoye akiongoza maombi katika ibada ya
kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi
Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la
Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin
Lekundayo(kushoto), iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Kwaya kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi ikiimba
katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja
na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu
Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania,
Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa
la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa
nchini.
Kwaya kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Sabasaba Musoma
mkoani Mara ikiimba katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika
Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa
nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo
Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba
05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa
kanisa hilo hapa nchini.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato
wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la
Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini,
iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba
05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa
kanisa hilo hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kushoto)
akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David Makoye, katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa
katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa
nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo
Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba
05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa
kanisa hilo hapa nchini.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato
wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la
Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini,
iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba
05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa
kanisa hilo hapa nchini.
Kutoka kushoto Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa
Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt. Mch. Godwin Lekundayo,
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Katibu Mkuu wa Kanisa la
Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David
Makoye wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga
la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini,
iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la
Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Waadventisa Wasabato
wakichangia ujenzi wa Kibweta kama alama ya shukrani kwa Mungu kwa kulivusha
Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa
amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa
Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt. Mch. Godwin Lekundayo,,
iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi
kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Mara, Mhe. Samweli Kiboye akitoa salamu katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la
Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini,
iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba
05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa
kanisa hilo hapa nchini.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Mhe. Juliana Mahongo katika
ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa
katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika salama hapa
nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo
Kuu la Kaskazin kwa amani i mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo,
iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi
kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakishiriki
maombi katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la
Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini,
iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba
05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa
kanisa hilo hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akivishwa skafu na vijana watengeneza njia katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo, viongozi wa Serikali na viongozi wa Chama, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la
Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(Kulia) akiagana na
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa
waSimiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha
Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa
amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika
Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo
hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment