Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kisiasa
kushirikiana pamoja na viongozi serikali na wadau wengine wa elimu katika
kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika mapema, lengo likiwa kuhakikisha
wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wanapata madarasa ya kusomea.
Mtaka ameyasema hayo Desemba
12,2020 kwenye kikao kazi cha mkoa cha kujadili uelekeo wa mkoa wa Simiyu
katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2020/2025 ) katika masuala
mbalimbali ikiwemo afya,elimu,kilimo,viwanda na ajira kwa vijana, ambacho
kimewashirikisha viongozi wa chama na serikali, ,wafanyabiashara ,viongozi wa
dini ,taasisi za umma na binafsi na wadau wa maendeleo wa Mkoa, kilichofanyika
Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
“Simiyu kipaumbele chetu cha kwanza ni elimu, nimekuwa
nikiwaambia watu wa Simiyu tukitaka kushindana tusomeshe watoto, malizieni
maboma ya madarasa watoto wapate mahali pa kusomea, kila mmoja abebe kwa
uchungu jambo hili kuona madarasa yanakamilika lakini mkienda kwenye mabaraza mkaanza kubishana
hamtawasaidia wananchi,” alisema Mtaka
Aidha Mtaka ameongeza kuwa kwa maeneo ambayo yana madini pamoja
na maeneo yanayonufaika na uhifadhii kama vile vijiji vya Makao, Mwangudo na
vingine Wilayani Meatu, wananchi wasichangishwe badala yake asilimia zinazotolewa
kwa ajili ya vijiji zielekezwe kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Ameongeza kuwa mkoa huwa umejiwekea malengo ya kuongoza katika
mitihani yote ya Taifa ambapo amewataka viongozi wa Serikali kuendelea kutoa
motisha kwa walimu ikiwa ni pamoja na kuacha kutoa lugha za kuwaudhi na
kuwakera walimu ili waendelee kufanya kazi kwa moyo.
Sambamba na hili Mtaka ametoa rai kwa Madiwani wote wa Mkoa huo
kuacha tabia ya kuazimia watumishi wao kwa kuwa hali hiyo inawavunja moyo
watumishi badala yake waweke mazingira ya watumishi kupenda kazi na ikiwa watumishi
watafanya jambo lisilotakiwa wawasiliane na mamlaka nyingine ili waweze
kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu.
Katika hatua nyingine Mtaka amesema Simiyu Imejipanga kuanzisha
utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo nafuu itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya
ndani inayotolewa kwa vijana wanawake na walemavu, akibainisha kuwa fedha hizo zitatangazwa
na kushindaniwa; ambapo vikundi havitapewa fedha badala yake Halmashauri zitalipia
teknolojia zinazohitajika kupitia SIDO na sehemu ya fedha inayobaki itatumika
kuwajengea uwezo wahusika wa vikundi hivyo.
Awali akitoa taarifa ya elimu mkoani hapo kwa niaba ya afisa
elimu mkoa wa Simiyu , Jusline Bandiko amesema mkoa huo una mahitaji ya vyumba
vya madarasa 565 ,vilivyopo ni 419 huku upungufu ukiwa vyumba 155 ambavyo
vinatakiwa kukamilika kwa ajili ya kidato cha kwanza 2021.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simyu, Mhe. Enock Yakobo ametoa wito
kwa viongozi kuona umuhimu wa kuanzisha mfuko wa elimu wa mkoa na kuwahamasisha
wananchi kuchangia mfuko huo ili uweze kusaidia katika ujenzi wa vyumba vya
madarasa, nyumba za walimu na ununuzi wa viti na madawati.
Miriam Mmbaga ni Katibu Tawala wa Mkoa huo ametoa wito kwa
viongozi wa Umma mkoani Simiyu kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo, sheria na
taratibu na kwa uadilifu mkubwa wakijiepusha na masuala ya migongano ya maslahi
katika maeneo yao, huku akisisitiza wafanye maamuzi sahihi kwa wakati sahihi
kwa maslahi ya wananchi wanaowaongoza.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) Taifa, Kheri James ambaye pia ni Mlezi wa CCM kwa mikoa ya Simiyu na
Mara amesema jamii inahitaji mageuzi ili kufikia mageuzi hayo inapaswa
kuwa na viongozi wenye uthubutu na ujasiri, huku akitoa wito kwa viongozi wa
Mkoa wa Simiyu kufanya kazi kwa ushirikiano na kutumia vizuri madaraka, mamlaka
na ushawishi walio nao kwa manufaa ya wananchi wanaowaongoza.
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa wa Chama
na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa
taasisi za Umma na binafsi pamoja
na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu kwenye kikao kazi cha
kujadili mwelekeo wa Mkoa katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025)
katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na
ajira kwa vijana, kilichofanyika
Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James akizungumza na wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu kwenye kikao kazi cha kujadili mwelekeo wa Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.
Mbunge
wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika kikao kazi cha Mkoa wa
Simiyu kilichowahusisha viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha,
viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa
Mkoa wa Simiyu kilicholenga kujadili mwelekeo wa Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano
ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira,
kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini
Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James wakati wa kikao kazi cha Mkoa
kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha,
viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa
Mkoa wa Simiyu, kilicholenga kujadili mwelekeo wa Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano
ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira,
kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini
Bariadi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiwasilisha mada katika
kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali,
viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma
na binafsi pamoja na wadau
mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu, kilicholenga kujadili mwelekeo wa Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano
ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira,
kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini
Bariadi.
Baadhi
ya viongozi wakifuatilia kikao cha kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi
wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini,
viongozi wa taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa
Mkoa wa Simiyu, kilicholenga kujadili mwelekeo wa Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano
ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira,
kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini
Bariadi.
Baadhi
ya viongozi wakifuatilia kikao cha kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi
wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini,
viongozi wa taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa
Mkoa wa Simiyu, kilicholenga kujadili mwelekeo wa Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano
ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira,
kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini
Bariadi.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na wa Chama na
Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi
za Umma na binafsi pamoja na wadau
mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu kwenye kikao kazi cha kujadili
mwelekeo wa Mkoa katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika
masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa
vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) na Mwenyekiti wa UVCCM
Taifa, Mhe. Kheri James wakifurahia jambo wakati wa kikao kazi cha Mkoa
kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha,
viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa
Mkoa wa Simiyu, kilicholenga kujadili mwelekeo wa Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano
ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira,
kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini
Bariadi.
Baadhi
ya viongozi wakifuatilia kikao cha kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi
wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini,
viongozi wa taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa
Mkoa wa Simiyu, kilicholenga kujadili mwelekeo wa Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano
ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira,
kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini
Bariadi. TAZAMA PICHA NYINGINE KATIKA KIKOA KAZI HIKI CHA MKOA
0 comments:
Post a Comment