Katibu
Tawala wa Mkoawa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga ametoa wito kwa viongozi, walimu,
wazazi na wadau wote wa elimu mkoani hapa kushiriki kikamilifu katika
kutekeleza na kuwezesha azma ya mkoa ya kuwa nafasi ya kwanza katika mitihani
yote ya Taifa.
Mmbaga ameyasema hayo
Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi wakati akifungua kikao cha viongozi, watendaji
na wadau wa elimu mkoa cha kutangaza Mkakati wa Mkoa wa kuboresha taaluma kwa
mwaka 2021 ambapo alibainisha kuwa endapo kila mdau atatimiza wajibu wake Simiyu
itakuwa mkoa bora katika elimu.
“Mkoa wetu kushika
nafasi ya kwanza inawezekana kabisa, kama tuliweza kutoka nafasi za mwishoni
kabisha tukaingia, kumi bora, sasa hivi tuka katika tatu bora, naamini kwa
uweza wa Mwenyezi Mungu tunaweza kushika
nafasi ya kwanza katika mitihani yote ya Taifa,” alisema Mmbaga.
Aidha, Mmbaga amewataka
viongozi wa idara ya elimu kuepuka kutumia kauli chafu kwa walimu kwa kuwa
zinawakatisha tamaa na kupunguza tija na ari katika utendaji kazi wao badal
yake watumie mbinu sahihi za kiuongozi kutatua changamoto wanazoziona kwa
walimu.
Naye Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.
Ernest Hinju amesema ushirikiano, mawasiliano na mahusiano mazuri baina ya
walimu, viongozi na wadau wote wa elimu yanasaidia muda mwingi kutumika
kufundisha na kusimamiana badala ya kutumika kuzozana, kugoma na kusuluhishana.
Baadhi ya walimu na
Maafisa Elimu wa Kata na Halmashauti wamesema wameupokea mkakati huo na kuahidi
kutimiza wajjibu wao ili kuweza kufikia malengo ya mkoa na kuboresha taaluma na
elimu mkoani Simiyu huku wakitoa maoni mbalimbali namna ya kuboresha zaidi
utekeelzaji wa mkakati huo.
“Nashauri mkoa uanzishe
mitihani ya pamoja ya madarasa tarajiwa yaani darasa la tatu, darasa la sita,
kidato cha kwanza na kidato cha tatu, mitihani hii itusaidia kujua shule zipi
zina changamoto gani na itasaidia kuweka mikakati ya kuziwezesha kufanya vizuri
kwa kuwa walimu na viongozi wengine watakuwa na mwaka mzima wa kuyaandaa
madarasa hayo kabla ya mtihani wa Taifa,” alisema Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi
Lagangabilili Itilima, Mwede Hongoa.
“Tunaomba Serikali
iboreshe makazi ya walimu, walimu wengi hawana nyumba za kuishi maeneo ya shule
wengi wanatoka mbali na Shule hivyo wakati tunapohitaji kuwasaidia wanafunzi
hasa nyakati za usiku inakuwa vigumu kwao kushiriki kikamilifu,” alisema
Mwalimu Flora Shimbi Mkuu wa Shule Itilima Sekondari.
“Serikali ya Mkoa
imetoa motisha kwa walimu hasa wanaofanya vizuri na walimu wa mkoa wa Simiyu
wamehamasika sana na wanajituma katika kazi yao, tunaomba serikali iendelee
kuboresha miundombinu ikiwemo vyumba vya madarasa, madawati na viti ili
mazingira yao ya kufundishia yawe bora zaidi,” alisema Mwalimu Oscar Nsolo Mkuu
wa Shule Sapiwi Sekondari.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ameshauri mkoa wa Simiyu
kuwa na mfuko wa elimu wa mkoa, ili mfuko huo uweze kusaidia katika ujenzi wa
miundombinu ya elimu huku akitoa wito kwa wazazi na wadau wote wa elimu kuona umuhimu
wa kuuchangia mfuko huo.
Mkakati
wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021 umejumuisha mambo muhimu
ikiwa ni pamoja na Uwezo wa kujituma kwa viongozi wa elimu, uungwaji mkono na
viongozi wa juu,uwajibikaji wa maafisa elimukata na mfumo wa utawala, huduma
bora na mawasiliano kwa walimu/wadau wa elimu, utoaji wa motisha na zawadi,
ufatiliaji kabambe wa ufundishaji na ujifunzaji, mafunzo kazini,upimaji, miundombinu
na samani, kambi za kitaaluma, matumizi ya mitandao ya TEHAMA.
MWISHO
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza
mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba
09, 2020 Mjini Bariadi kikiwashirikisha walimu, viongozi wa Chama na Serikali,
viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani hapa.
Baadhi ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani Simiyu, katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi.
Mmoja
wa walimu akichangia hoja katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha
taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini
Bariadi.
Baadhi
ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu
mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi.
Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa
wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi
Baadhi
ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu
mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi.
Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa
wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi
Baadhi
ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu
mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi.
Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa
wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi
0 comments:
Post a Comment