Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesitisha
matumizi ya leseni 18 za uchimbaji madini katika mgodi wa Dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani
mwa wilaya ya Bariadi na Busega, mpaka pale zitakapotolewa ufafanuzi na Waziri
mwenye dhamana ya madini juu ya uhalali wake katika uendeshaji wa shughuli za
madini.
Mtaka ametoa uamuzi huo katika mkutano wa hadhara ambao
umefanyika eneo la mgodi Desemba 17, 2020 akiwa amefuatana na viongozi
mbalimbali wa Chama na Serikali kwa ajili ya kwenda kusikiliza kero za
wachimbaji wadogo mgodini hapo na kuzitafutia ufumbuzi.
“Sisi kama viongozi wa mkoa tunasitisha matumizi ya leseni za
eneo lote hili, mpaka pale waziri mwenye dhamana atakapokuja kutoa ufafanuzi
kwa wananchi, kwa sababu sheria inamtamka waziri kwenye kufuta leseni lakini
sisi mkoa kwa tuliyoyaona hapa tunasitisha; kwa sasa mgodi utaendelea kuwa chini ya usimamizi wa
maelekezo ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa,” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amesema Maafisa kutoka katika Ofisi zote
zinazopaswa kutoa huduma kwa wachimbaji hao ikiwa ni pamoja na maafisa wa Soko
la Madini kuanzia Desemba 18, 2020 watakuwa katika eneo la mgodi ili
kuwapunguzia wachimbaji hao adha ya kufuata huduma mbali na eneo hilo huku
akisisitiza wachimbaji hao wauze dhahabu kwa bei iliyopo sokoni.
Mtaka pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya
Bariadi na Busega kufanya tathmini ya mashamba yaliyoharibiwa na shughuli zinazoendelea
katika eneo la mgodi ili wakulima hao waweze kulipwa fidia, huku akiwataka
Wakurugenzi hao pia kuhakikisha
wanasimamia ujenzi wa matundu ya vyoo yasiyopungua 12 kuimarisha hali ya usafi
mgodini.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa onyo kwa wachimbaji na
watu wote wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji madini kujiepusha na
utoroshaji wa dhahabu, kwamba
watakapobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni
pamoja na kutaifisha dhahabu hiyo.
Awali wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba na wamiliki wa
maduara waliwasilisha changamoto
mbalimbali zinazowakabili kwenye mgodi huo ambazo baadhi zilipatiwa ufumbuzi na uongozi wa mkoa na baadhi zitashughulikiwa
na Waziri mwenye dhamana ya madini.
“Usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwenye mgodi huu
uimarishwe zaidi, ili Serikali ipate sehemu yake, wachimbaji na sisi tupate
sehemu yetu na kila tozo au ushuru wanaotutoza wahakikishe wanatoa risiti za
kielektriniki,” alisema Flugence Ekondo mchimbaji mdogo.
“Katika ugunduzi wa mgodi huu mke wangu alikuwa anapalilia
mahindi akaokota jiwe, alivyolileta tulikuwa na wasiwasi nalo tukalipeleka
mgodi wa Gasuma tukaambiwa ni dhahabu, hiyo ilikuwa tarehe 05/11/2020 kesho
yake wachimbaji wakaanza kuchimba na mgao ukafanyika; binafsi nilijua hiyo
itakuwa rashi itakayotunufaisha wachimbaji wadogo na jamii inayotuzunguka,lakini
baadaye tukasikia kuna leseni tunaomba tusaidiwe na sisi tupate haki yetu
kwenye mgao,” Ntimba Masalu mwakilishi wa wenye mashamba
Akitoa ufafanuzi kuhusu mgao, Afisa madini Mkazi wa Mkoa, Mhandisi.
Oscar Kalowa amesema “katika mifuko 100 asilimia saba ni fedha ya serikali,
wamiliki wa mashamba asilimia 15, msimamizi/mmiliki wa leseni asilimia 15 na
mwenye duara husika anapata asilimia zinazobaki na huu ndiyo utaratibu
unaohusika.”
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka amesitisha matumizi ya leseni 18 za uchimbaji madini katika
mgodi wa Lubaga uliopo mpakani mwa wilaya ya Bariadi na Busega, mpaka pale
zitakapotolewa ufafanuzi na Waziri mwenye dhamana ya madini juu ya uhalali wake
katika uendeshaji wa shughuli za madini. Baadhi ya wachimbaji
wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipotembelea mgodi
huo akiwa na viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo Desemba 17, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia walioketi) akiwa na baadhi viongozi wa Chama
na Serikali mkoani humo katika mkutano wake na wachimbaji wadogo (waliosimama)
katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17,
2020.
Kutoka kulia Mwenyekiti
wa CCM Mkoa, Mhe. Enock Yakobo, Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi.
Miriam Mmbaga wakiteta jambo kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya
Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.
:-Afisa Madini Mkazi
mkoa wa Simiyu, Oscar Kalowa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya
Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.
Mwenyekiti wa Kijiji
cha Majengo kilichopo Kata ya Dutwa wilayani Bariadi akizungumza kwa niaba ya
wananchi wa kijiji hicho kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa
dhahabu wa Lubaga uliopo katika eneo la
mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine wakielekea
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
eneo la Mgodi wa dhahabu wa Lubaga
uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.
Debora John mmoja wa
wachimbaji wadogo kwenye Mgodi wa
dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa
Wilaya ya Bariadi na Busega katika mktano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo
hilo, Desemba 17, 2020.
Mmoja wa wachimbaji
wadogo kwenye Mgodi wa dhahabu wa
Lubaga uliopo mpakani mwa Wilaya ya
Bariadi na Busega katika mktano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo hilo,
Desemba 17, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi.
Miriam Mmbaga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa
Lubaga uliopo katika eneo la mpaka wa
Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe. Tano Mwera akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya
Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe.Festo Kiswaga akitoa
ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo
katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020
Baadhi ya wachimbaji
wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipotembelea mgodi
huo akiwa na viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo Desemba 17, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine wakielekea
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
eneo la Mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo
mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.
0 comments:
Post a Comment