Rai imetolewa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote
mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa wanakamilisha zoezi la utoaji wa vitambulisho
vya matibabu kwa wazee kufikia mwezi Juni 2021, ili wazee waweze kupata huduma
za matibabu katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya kama Serikali
ilivyodhamiria.
Rai
hiyo imetolewa Novemba 4, 2020 Mjini Bariadi na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
katika uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Simiyu..
“Mkoa
kupitia Halmashauri umefanya utambuzi wa jumla ya wazee 68,175 kwa lengo la
kuhakikisha kuwa wanapatiwa huduma muhimu, hadi sasa jumla ya mabaraza 770 ya wazee yameundwa katika ngazi zote ; kuhusu
upatikanaji wa vitambulisho vya matibabu bure, jumla ya wazee 18, 911
wamepatiwa vitambulisho hivyo ndani ya mkoa sawa na asilimia 28,’ alisema
Kiswaga.
Mabaraza
si ya kiitikadi hivyo kila mtu mwenye umri wa miaka sitini na kuendelea ana
haki ya kujiunga na kuwa mjumbe wa Baraza la Wazee mahali alipo, huku akiahidi
kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Wazee na kukukutana na wazee mara kwa
mara ili kuhakikisha kuwa inawasilikiza na mahitaji yao muhimu yanapatikana.
Mwakilishi
wa Katibu Tawala wa Mkoa, Bibi.Mwanahamisi Kawega amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
itahakikisha inasimamia utekelezaji wa suala la ugawaji wa vitambulisho vya
matibabu kwa wazee katika Halmashauri zote ili wazee wote waweze kuvipata kwa
wakati.
Aidha
Kawega ameongeza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu itawaelekeza Wakurugenzi
wa Halmashauri kuwaalika viongozi wa mabaraza ya wazee kualikwa katika mabaraza
ya madiwani ili waweze kuwasilisha kero zao na kupatiwa ufumbuzi.
Naye Meneja
Mradi kutoka Shirika la NABROHO SOCIETY FOR THE AGED linalojihusisha na utetezi
wa haki za wazee , Bw. Kubini Nkondo ameipongeza Serikali kwa namna
inavyotoa kipaumbele kwa wazee na namna ilivyokomesha mauaji ya wazee.
"Wazee
wamepitia changamoto nyingi ukizungumzia hata suala la mauaji ya wazee,
takwimu awali zilikuwa juu sana lakini katika utawala huu tunazungumzia mauaji
hayo kupungua mpaka kufikia 'digit' (tarakimu) moja, Mkoa wa Simiyu ambao
ulikuwa ukitajwa katika Mkoa 10 inayoongoza kwa mauaji ya wazee sasa hivi
haitajwi hata tena katika mikoa inayoongoza kwa mauaji hayo," alisema
Nkondo.
Mwenyekiti
wa Baraza la Ushauri la Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo amesema Baraza hilo
litaendelea kushirikiana na Serikali katika kushughulikia haki mbalimbali za
wazee huku akiomba Serikali kuitungia sheria Sera ya wazee ya mwaka 2003
ili iweze kutumika katika kuwaongoza pamoja na miongozo iliyopo.
Afisa
Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Daniel Mapunda amesema Mkoa wa
Simiyu una takribani wazee 68,175, hivyo kwa mujibu wa Sera ya Wazee ya mwaka
2003 Baraza la Wazee la Mkoa litakuwa ni chombo maalum cha kuwasemea wazee na
kushiriki katika maeneo mbalimbali ya kimaamuzi.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa pili
kushoto) akimkabidhi nyaraka mbalimbali Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la
Wazee Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo mara baada ya kuzindua baraza hilo
Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka.
Meneja Mradi wa Taasisi
isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na utetezi wa Haki za Wazee mkoani
Simiyu, Bw. Kubini Nkondo Kubin akizungumza na viongozi wa mabaraza ya Ushauri ya Wilaya katika kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020
Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la
Mkoa na kuzindua baraza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, viongozi wa Baraza la Ushauri la Wazee la
Mkoa, Viongozi wa mabaraza ya wilaya (waliosimama) wakiongozwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Mkoa, Bw. Lameck Sendo(wa pili kulia walioketi), baada ya kuzindua
baraza hilo Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, viongozi wa Baraza la Ushauri la Wazee la
Mkoa, Viongozi wa mabaraza ya wilaya (waliosimama) wakiongozwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Mkoa, Bw. Lameck Sendo(wa pili kulia walioketi), baada ya kuzindua
baraza hilo Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mwenyekiti wa Baraza la
Ushauri la Wazee Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo akitoa maelezo ya agenda kumi
zinazowahusu wazee katika kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi,
kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza hilo na kuzindua kazi iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kuzindua
baraza hilo, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Maafisa Ustawi wa Jamii na kiongozi wa
dini (waliosimama) na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa, Bw.
Lameck Sendo(wa pili kulia walioketi), baada ya kuzindua baraza hilo Desemba
04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba
akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa Baadhi ya viongozi wa Mabaraza ya
Ushauri ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika Desemba 04,
2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Mkoa
na kuzinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, akimwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Baadhi ya viongozi wa
Mabaraza ya Ushauri ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kikao
kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa
Baraza la Usahauri la Wazee la Mkoa na kuzindua baraza hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la
ushauri la Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, akipokea nyaraka za utendaji kazi
wa baraza hilo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada
ya kuzinduliwa kwa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa, Desemba 04, 2020 Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Maafisa Usatawi wa Jamii na kiongozi wa
dini (waliosimama) na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa, Bw.
Lameck Sendo(wa pili kulia walioketi), baada ya kuzindua baraza hilo Desemba
04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka.
Baadhi ya Viongozi wa
Baraza la Ushauri la Mkoa wa Simiyu
Mwakilishi wa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Daniel Mapunda na Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba
wakiteta jambo kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo
la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa na kuzindua baraza
hilo.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na baadhi ya viongozi wa mabaraza ya
ushauri ya wilaya za mkoa wa Simiyu kabla ya kuzindua Baraza la ushauri la Mkoa
kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
0 comments:
Post a Comment