Shirika la Kikristo la Life Ministry limekabidhi
Zahanati kwa Uongozi wa Mkoa wa Simiyu ambayo imejengwa katika Kijiji cha
Itubukilo wilayani Bariadi.
Akisoma taarifa ya makabidhiano ya
zahanati hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkurugenzi
wa Life Ministry Tanzania, Bw. Dismas Shekalaghe amesema shirika hilo lilipokea
zahanati hiyo kutoka kwa wananchi ambao walianza kujenga kwa nguvu zao na
kuifikisha hatua ya renta, hadi kufikia hatua za ukamilishaji wa zahanati hiyo
Shirika la Life Ministry limetoa kiasi cha Shilingi milioni 71.
Amesema pamoja na zahanati hiyo, shirika
hilo limefanya mengi mkoani Simiyu ikiwa ni apamoja na kutoa vifaa tiba
Hospitali Teule ya Mkoa vyenye thamani ya shilingi milioni 40, huduma za macho
na kutoa miwani bure, kutoa baiskeli zaidi ya 20 kwa walemavu, kugawa vifaa
mbalimbali kwa makundi mbalimbali wakiwemo watoto wenye ualbino, kuwezesha
vikundi vya bustani zaidi ya 40 katika kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya
matone na kuchimba visima virefu 12 vyenye thamani ya shilingi milioni 300.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano
hayo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Life Ministry kwa
msaada wa zahanati hiyo na kuwahakikishia kuwa mara tu itakapokamilika Serikali
itahakikisha Zahanati hiyo inafanya kazi na itapeleka watoa huduma za afya ili
wananchi waanze kupata huduma.
"Niwakikishie tu kuwa Serikali
itahakikisha Zahanati hii inafanya kazi kwa kuleta wataalam na bahati nzuri
Serikali imekubali kuajiri watu wa Sekta ya Afya" alisema Mtaka.
Mtaka amesema Taasisi za Dini zimekuwa
zikiunga mkono kazi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuwaletea
wananchi maendeleo na akaiomba Life Ministry kuendelea kusaidia katika ujenzi
wa Vituo vya kutolea huduma za Afya, ili kusaidia uboreshaji wa huduma za Afya
mkoani Simiyu, kwa kuwa mkoa huo una uhitaji mkubwa wa vituo vya afya.
" Mkoa wetu tuna asilimia chini ya
40 ya vituo vya Afya, Kama ni jambo ambalo litakuwa ndani ya uwezo wa Taasisi
ningeomba muendelee kutusaidia kwenye sekta ya Afya; zipo juhudi za Serikali
katika uimarishaji wa sekta ya Afya hususani kwenye ujenzi wa Zahanati, Vituo
vya Afya na Hospitali lakini washirika kama Taasisi za Dini bado tunawahitaji
kwa kuwa mmekuwa mkono wa pili kwenye kuunga mkono juhudi za Serikali"
alisisitiza.
Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa
Itubukilo, Diwani wa Kata ya Itubukilo Mhe. Mayanda Makenzi akiishuku Life
Ministry kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo amesema itawaondolea
adha wananchi wake kutembea mwendo mrefu kufuata huduma za Afya.
Naye Diwani wa Viti Maalum Mhe. Juliana
Lucas amesema ukamilishaji wa zahanati hiyo utawasaidia sana wananchi kupata
huduma karibu hususani wanawake ambao watapata huduma za afya ya uzazi na
kupata msaada wa karibu wakati wa kujifungua na hivyo kupunguza vifo vya wakina
mama na watoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bariadi, Bw. Abdallah Malela amesema Zahanati hiyo ya Itubukilo
itafunguliwa rasmi na kuanza kutoa huduma Julai Mosi, 2018.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria kupokea Zahanati iliyojengwa na Shirika
la Life Ministry katika Kijiji cha Itubukilo Wilayani Bariadi ambayo ilikabidhiwa rasmi kwa Serikali na Shirika
hilo Juni 03, 2018.
Mkuu wa Mkoawa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akifurahia jambo na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi, Viongozi wa Life Ministry naViongozi wa madhehebu ya Kikristo baada ya
makabidhiano ya Zahanati ya Itubukilo kati ya Serikali na Shirika la Life
Ministry ambayo imejengwa na Shilika hilo, Juni 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Life Ministry Tanzania,
Bw. Dismas Shekalaghe(kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Life Ministry Tanzania,
Mhandisi. Kapuulya Musomba (katikati) wakati wa hafla ya makabidhiano ya
Zahanati iliyojengwa na Shirika hilo katika Kijiji cha Itubukilo wilayani
Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini ya Kikristo
wakitoka kukagua jengo la Zahanati iliyojengwa na Shirika la Life Ministry
Tanzania katika Kijiji cha Itubukilo wilayani Bariadi ambayo ilikqbidhiwarasmi
Juni 03, 2018 kwa Serikali ya Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utubukilo wilayani
Bariadi wakati wa hafla ya makabidhiano ya Zahanati iiliyojengwa na Life
Ministry Tanzania Juni 03, 2018.
Mkurugenzi wa Life
Ministry Tanzania, Bw. Dismas Shekalaghe(kushoto) akiwasilisha taarifa ya
ujenzi wa Zahanati ya Itubukilo ambayo imejengwa na shirika hilo la Kikristo na
kukabidhiwa kwa Serikali Juni 03, 2018.
Diwani wa Kata ya
Itubukilo, Mhe. Mayanda Makenzi akizungumza na wananchi Kijiji cha Utubukilo
wilayani Bariadi wakati wa hafla ya makabidhiano ya Zahanati iliyojengwa na
Life Ministry Tanzania Juni 03, 2018.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, mheAnthony Mtaka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Bariadi, Bw. Abdallah Malela na Katibu wa CCM Wilaya ya Bariadi wakiteta
jambo wakati wa makabidhiano ya Zahanati ya Itubukilo na Shrika la Life
Ministry.
Viongozi wa Shirika la Life
Ministry na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa
Simiyu wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya hafla ya makabidhiano ya
Zahanati katika Shirika Hilo na Serikali ambayo imejengwa katika Kata ya
Itubukilo Wilayani Bariadi.
Baadhi
ya viongozi wa madhehebu ya Kikristo na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Itubukilo katika hafla ya makabidhiano ya
Zahanati iliyojengwa na Shirika la Life Ministry Juni 03, 2018.
Diwani wa Viti Maalum,
Mhe. Juliana Lucas akimkabidhi Mwenyekiti
wa Bodi ya Life Ministry Tanzania, Mhandisi. Kapuulya Musomba zawadi ya Kitenge
kwa niaba ya waananchi wa Itubukilo kama ishara ya kumshukuru kwa kuruhusu
Shirika hilo Kujenga Zahanati ya Itubukilo wilayani Bariadi katika hafla ya
makabidhiano ya Zahanati hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Life Ministry Tanzania,
Bw. Dismas Shekalaghe(kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Life Ministry Tanzania,
Mhandisi. Kapuulya Musomba (katikati) baada ya hafla ya makabidhiano ya
Zahanati iliyojengwa na Shirika hilo katika Kijiji cha Itubukilo wilayani
Bariadi, Juni 03, 2018.
Diwani wa Viti Maalum,
Mhe. Juliana Lucas akimkabidhi Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu. Mhe. Anthony Mtaka zawadi
ya Kitenge kwa niaba ya wananchi wa Itubukilo kama ishara ya kumshukuru kwa
namna anavyopigania maendeleo ya wananchi wake wakati wa makabidhiano ya Zahanati ya
Itubukilo wilayani Bariadi iliyojengwa na Shirika la Kikristo la Life
Ministry.
Baadhi ya viongozi wa
madhehebu ya Kikristo, wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Wajumbe
kutoka Shirika la Life Ministry wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji chaItubukilo katika
hafla ya makabidhiano ya Zahanati iliyojengwa na Shirika la Life Ministry Juni
03, 2018.
0 comments:
Post a Comment