Monday, June 4, 2018

WAGANGA WAFAWIDHI WATAKAOSHINDWA KUSIMAMIA VITUO VYAO KUVULIWA MADARAKA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini amewaagiza Waganga Wakuu wa Wilaya kuwaondoa katika nafasi za usimamizi wa zahanati na vituo vya afya ,waganga wafawidhi watakaoshindwa kusimamia vituo vyao kufika vigezo vilivyowekwa katika utoaji huduma za afya kwa wananchi kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi (RBF).

Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao chake na Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa wilaya, Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa(RHMT), waganga wafawidhi wa zahanati na vituo vya afya lengo likiwa ni kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.

“Waganga na Wauguzi wafawidhi tumewaita hapa tunataka mabadiliko kwenye utendaji wenu, vituo vyenu wote viende kwenye Alama A, kinyume na hapo Waganga Wakuu wa Wilaya wawavue madaraka na Waganga wakuu wa Wilaya wasipofanya  hivyo Wakurugenzi washughulikieni wao” alisema Sagini.

Amesema kutotekeleza majukumu yao vizuri ikiwa ni pamoja na kushindwa kusimamia suala la ujazwaji wa  takwimu sahihi kwa wakati,  kunasababisha Vituo vyao kutopata fedha za mpango huo (RBF)  ambazo hutolewa kwa vituo vinavyofanya vizuri,  ambapo vituo hivyo vikizipata zitasaidia kuboresha miundombinu ya Afya na ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Ameongeza kuwa  Timu za Usimamizi wa Huduma za Afya Wilaya (CHMT) zinapaswa kufanya ufuatiliaji na usimamizi katika Vituo vya kutolea huduma na kuhakikisha mapungufu yote yanayojitokeza yanafanyiwa kazi ili vituo vyote vitoe huduma kwa ufanisi na kupata fedha kulingana mwongozo wa Mpango wa RBF ambazo zitasaidia kuboresha huduma kwenye vituo.

Katika hatua nyingine Sagini amewataka Waganga wakuu wa Wilaya na Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya kuwasilisha taarifa za wagonjwa wanaopata huduma kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  kwa wakati kama maelekezo yanavyowataka kufanya ili kuondoa usumbufu usio wa lazima.

Nao Wasimamizi wa Vituo baada ya maelekezo ya Katibu Tawala wa Mkoa wamekiri kuwa watabadilika na kuhakikisha vituo vyao vinafanya vizuri na kufikia alama A ili kuwawezesha kupata fedha kupitia Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) zitakazowasaidia kuboresha huduma za afya katika vituo vyao.

“ Nimesikitishwa sana na Halmashauri yetu kukosa fedha za RBF kiasi kilichotajwa na mratibu kwa sababu ya baadhi ya watendaji kutotimiza wajibu wao, mimi ninaona haya yote yako ndani ya uwezo wetu, kuanzia sasa tunapaswa kutimiza wajibu wetu na tuhakikishe taarifa zote zinazopelekwa wilayani zinajazwa kwa usahihi na kwa wakati” alisema Godfrey Pascal kutoka Zahanati ya Nkololo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw.Fabian Manoza amesema ipo haja ya kuwajengea uwezo na kutoa mafunzo ya menejimenti ya takwimu  kwa wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma za Afya, ili waweze  kukusanya takwimu zinazotakiwa kwa mujibu wa mwongozo wa Mpango wa RBF hatimaye vituo vyao vipate alama nzuri na fedha zitazowasaidia kuboresha huduma.

Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Simiyu Jarlath Mushashu ameziomba Halmashauri zote Mkoani Simiyu kulipa deni ambalo Mfuko huo unazidai lililofikia shilingi milioni 78, ili kuuwezesha mfuko huo kutoa huduma za matibabu kwa wanachama na wategemezi wao kama inavyotakiwa.

Wakati huo huo Mushashu amewaomba Wakurugenzi wa Halmashauri kuwasilisha kwa wakati michango ya watumishi ya Bima ya Afya hususani watumishi wanaolipwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri.
MWISHO
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini akifungua kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Simiyu Jarlath Mushashu akiwasilisha taarifa ya Mfuko huo katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa. 

Mratibu wa Mpango wa Malipo kwa Ufanisi, Mkoa wa Simiyu Bw.Oscar Tenganamba akiwasilisha taarifa ya mpango huo katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa. 

Katibu Tawala Mkoa akimkabidhi Muuguzi Mfawidhi wa Zahanati ya Nyangokolwa, Bi. Nuriath Mtumbi  Mjini Bariadi, fedha taslimu kiasi cha shilingi 185,000/= zilizotolewa na wajumbe wa kikao cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kumpongeza kwa usimamizi mzuri wa kituo chake.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani Simiyuwakimsikiliza Katibu Tawla wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini katika kikao kilicholenga kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa. 


Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani Simiyuwakimsikiliza Katibu Tawla wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini katika kikao kilicholenga kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Mageda Kihulya  akizungumza Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo katika kikao kilicholengakujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bw. Mariano Mwanyigu akichangia hoja katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani Simiyu chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza akichangia hoja katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani Simiyu chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa. 
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha kutolea huduma za Afya akichangia hoja katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani Simiyu chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.
 Mkaguzi Mkuu wa ndani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Mika Mollel akichangia hoja katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo, chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya akichangia hoja katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Afya Mkoani Simiyu chenye lengo la kujadili matokeo ya Mpango wa Malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kipindi cha Mwezi Januari-Machi 2018 na masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwepo Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!