Tuesday, November 15, 2016

RC SIMIYU: WAMILIKI BODABODA MADEREVA WENU WAPEWE MAFUNZOMkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wakazi wa Bariadi Mkoani humo wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka na viongoi wengine wa Mkoa huo wakipokea maandamano ya madereva na watumiaji wengine wa barabara wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Baadhi ya madereva wa bodaboda na bajaji wakiwa katika maandamano na wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani)  wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani alipotembelea banda wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Usalama barabarani alipotembelea banda la kamati hiyo wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akipata maelezo kutoka kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto alipotembelea banda la Jeshi hilo wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Waimbaji wa Kwaya ya AICT Bariadi Mjini wakiimba wimbo maalum wenye ujumbe wa Usalama Barabarani wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi SOMANDA B wakionesha igizo wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Baadhi ya wananchi wa Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka alipowahutubia wakati uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Usalama Barabarani Mkoani humo mara baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Usalama Barabarani Mkoani humo mara baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi, (wa tatu kuia) Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa Edson Mwakiaba.
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Simiyu, Edson Mwakiaba akiwasilisha taarifa ya Mkoa ya Usalama wakati uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo mara baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Usalama barabarani mara baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. AnthonyMtaka akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na Waimbaji wa kwaya ya Kanila la AICT Bariadi.

                                                     Na Stella Kalinga
Katika kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani, wamiliki wa bodaboda wametakiwa kuhakikisha madereva wanaowakabidhi pikipiki wamepata mafunzo ya uendeshaji na usalama barabarani

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka wakati wa uzinduzi wa wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani uliyofanyika kimkoa mjini Bariadi  mkoani humo.

Mtaka amesema wamiliki wa bodaboda wanapaswa kutambua kuwa hiyo ni fursa kiuchumi hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wanawakabidhi pikipiki watu wenye ujuzi ambao watazilinda dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na ajali zisizo za lazima.

“Wamiliki wa bodaboda mnawekeza fedha nyingi katika kununua bodaboda lakini wengi wenu mnawakabidhi madereva ambao  hawana mafunzo na wanakuwa sababu ya ajali za barabarani. Hakikisheni wamepewa mafunzo na ambao hawana wasaideni wapate ili kuepuka kupoteza pikipiki zenu na nguvu kazi ya Taifa kwa ajali ambazo siyo za lazima”alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amewataka madereva wanaoendesha bodaboda kuheshimu kazi hiyo kwa kuwa inawapatia kipato hivyo wanapaswa kujifunza na kuzingatia matakwa ya sheria za usalama barabarani.

Akisoma taarifa ya Hali ya Usalama Barabarani Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Simiyu, ASP.Edson Mwakihaba amesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Desemba 2016 jumla ya ajali 111 zimetokea mkoani humo ambazo zimesababisha watu 71  kupoteza maisha na wengine 39 kujeruhiwa.

 ASP Mwakihaba amesema vyanzo vya ajali hizo ni elimu duni kwa waendesha bodaboda ambao wanabeba abiria bila kupata mafunzo na kutovaa kofia ngumu, matumizi yasiyo sahihi ya vyombo vya moto katika kubeba mizigo ya hatari na kuzidisha uzito ulioruhusiwa, ubovu wa barabara na vyombo vya usafiri,ukosefu wa maegesho na makosa ya kibinadamu.

Vyanzo  vingine ni pamoja na kukosekana kwa alama za barabarani,mapungufu ya sheria ya salama barabarani ambayo makosa mengi hayaendani na viwango vya adhabu, kukosekana kwa vyuo vya kutolea elimu kwa madereva na magari mengi ya minadani kuchanganya abiria na mizigo.

Mwakihaba amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikana na wadau mbalimbali limejiwekea mikakati mbalimbali katika kukabiliana na ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watumia vyombo vya moto na wananchi kwa ujumla juu ya sheria za usalama barabarani, kukagua madereva na vyombo vya moto kabla ya safari.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka imelitaka Jeshi la Polisi Kikosi cha Barabarani kutowaruhusu madereva kuendesha magari ya abiria  wanapogundulika kuwa na kilevi pale wanapopimwa kabla ya kuendesha vyombo vyao.

Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amelitaka jeshi la Polisi Kikosi cha usalama Barabarani kuwapima madereva wa bodaboda na bajaji hususani wale walio katika miji mikuu ya wilaya badala ya kujikita kwa madereva wa magari pekee.


Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Mwaka 2016 ni“Hatutaki ajali,tunataka kuishi”  na hii ni mara ya nne tangu kwa maadhimisho haya kufanyika mkoani Simiyu tangu kuanzishwa kwake.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!