Baada ya kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wa
pamba mkoani Simiyu jumla ya makampuni 12 yamekubali kuingia sokoni kunua pamba
ya wakulima kwa bei elekezi ya shilingi 1200.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka wakati wa kufunga kikao maalum cha kujadili mstakabali wa ununuzi wa
pamba katika mkoa wa Simiyu, ambapo pia ilielekezwa kuwa makampuni yaliyokubali
kununua pamba kwa wakulima yazingatie sheria na taratibu na yawalipe wananchi fedha
zao kwa wakati.
Mtaka ameyapongeza makampuni yote yaliyokubali kuingia kununua
pamba huku akiahidi kutoa msaada kwa wafanyabiashara wanaokutana na changamoto
ya upatikanaji wa fedha kutoka katika taasisi za fedha na kuwahakikishia kuwa
kila atakayehitaji msaada atamsaidia ili apate fedha.
Aidha, Mtaka amesema yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu
katika mizani achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria huku akiutaka wakala wa
vipimo kusimamia na kuhakikisha mizani hazichezewi katika Vyama vya Ushirika
vya Msingi(AMCOS).
“ Kama kuna wakati Wakala wa Vipimo unahitaji kuwa na saa nyingi
za kufanya kazi ni sasa kama magari hayatoshi waombe tutawapa na kama watumishi
hawatoshi omba watalaam kutoka katika maeneo mengine, kama kuna mtu atakutwa
amefanya udanganyifu katika mizani kwenye vyama vya ushirika achukuliwe hatua
kwa mujibu wa sheria” alisema Mtaka.
Kwa upande wao Wanunuzi wa pamba mkoani SIMIYU wameiomba
serikali kuondoa tozo zote zilizopo kwenye utaratibu wa ununuzi wa pamba, ili
kupunguza hasara watakayopata kwa kununua pamba kwa Bei elekezi ya shilingi 1200
kwa kilo kutokana na bei ya soko la dunia kushuka, jambo ambalo lililofafanuliwa
na Katibu Tawala Mkoa, Bw.Jumanne Sagini kuwa tozo hizo ni jambo la kisera na
kisheria nchini hivyo haliweze kufanyiwa maamuzi na mkoa.
Katika hatua nyingine baadhi ya wanunuzi wa pamba wakapendekeza
kuanzishwa kwa viwanda vya nyuzi na nguo ili kuongeza thamani ya Pamba na
kuondokana na utegemezi wa bei ya soko la dunia.
“Tukisema mwaka huu tutoe tozo fulani na mwakani tutatoa
nyingine tena, hiyo haitakuwa tiba kwenye bei ya soko la dunia, Tiba pekee ya
kulinusuru zao la pamba ni kuwekeza kwenye viwanda vya nyuzi na nguo na hilo
tunaliweza, tuwekeze sisi Wanasimiyu viwanda vijengwe Simiyu” alisema Mnunuzi
wa Pamba Gungu Silanga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe, Festo Kiswaga amewataka
wanunuzi wote kuzingatia sheria wakati wakinunua pamba ya wakulima na akasisitiza
kuwa wale watakaokiuka sheria ikiwa ni pamoja na kununua pamba usiku
watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Baadhi ya Makampuni yaliyokubali kuingia kununua pamba mkoani
Simiyu ni pamoja na Alliance Ginneries Limited, NGS, MWATEX, GAKI, OLAM, SM na
Vitrex
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wadau wa zao la pamba mkoani hapa,
kilicholenga kujadili mstakabali wa ununuzi wa pamba mkoani hapa,
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wadau wa zao la pamba mkoani hapa,
kilicholenga kujadili mstakabali wa ununuzi wa pamba mkoani hapa,
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Gungu Silanga mnunuzi
wa pamba mkoani Simiyu akichangia hoja katika kikao cha wadau wa pamba mkoani
Simiyu kilicholenga kujadili mstakabali wa ununuzi wa pamba mkoani hapa,
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima Mhe. Benson Kilangi akichangia hoja katika kikao cha wadau wa pamba
mkoani Simiyu kilicholenga kujadili mstakabali wa ununuzi wa pamba mkoani hapa,
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mnunuzi wa Pamba
mkoani Simiyu, Bw. Malongo Midimu akichangia
hoja katika kikao cha wadau wa pamba mkoani Simiyu kilicholenga kujadili
mstakabali wa ununuzi wa pamba mkoani hapa, kilichofanyika Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment