Serikali mkoani Simiyu kwa kushirikiana na wadau Shirika liliso
la kiserikali la InterHelath imeanzisha huduma ya tohara kinga kwa watoto
wachanga na tayari zoezi hilo limekwishaanza wilaya ya Meatu ambapo wataalam
wanaotoa huduma hiyo wamekwishapatiwa mafunzo.
Matarajio ya serikali ni kusambaza huduma hiyo ya tohara kinga
kwa watoto wachanga kwenye wilaya zote mkoani hapo ili huduma hiyo ipatikane
kiurahisi na kwa wakati na kulifanya zoezi hili kuwa utamaduni ili jamii ione
umuhimu wake tangu mtoto akiwa mdogo .
Hayo yamesemwa na mratibu wa kudhibiti UKIMWI mkoa wa Simiyu Dkt
Khamis Kulemba Julai 12, 2019 wakati
akiongea na waandishi wa habari katika mahojiano maalum matra baada ya
kuhitimishwa kwa kikao cha wadau wa AFya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Ameongeza kuwa awali
zoezi la tohara lilikuwa la hiari kwa wanaume waliokuwa bado hawajafanyiwa
huduma hiyo ambapo amesema lilipokelewa kwa mwititiko mkubwa hivyo ikaonekana
ipo haja na umuhimu wa kutoa huduma hiyo tangu mtoto akiwa mdogo ili kuwa na
kizazi kijacho kilichopata huduma hiyo .
“kwa kipindi cha mwaka 2017/18 mpango wa tohara ya hiari kwa wanaume
ulijikita katika halmashauri ya Bariadi, halmashauri ya
Itilima na halmashauri ya Meatu kama mkoa tulikuwa tunataka tutoe
tohara kinga kwa wanaume takribani 59,129 kuanzia Oktobar 2018 na kila
halmashauri ina lengo lake kwa kwa Bariadi lengo lilikuwa
kutahiri zaidi ya wanaume 20,440 lakini tulifanikiwa kutahiri wanaume
17,165 sawasawa na 84%, alisema Dkt Kulemba na kuongeza kuwa:
“kwa wilaya ya Itilima lengo lilikuwa kuwafikia kina baba
wapatao 22,176 lakini mpaka tarehe 30 june tuliwafikia wanaume 16,621
sawasawa na asilimia 75 , kwa wilaya ya Meatu tumekwenda mbali
kidogo lengo la lilikuwa kuwafikia wanaume 16,513 na mpaka
mwisho wa mwezi wa sita tarehe 30 tumewafikia wanaume 15,165 sawasawa na
92% kwa mkoa mzima tumeshawafikia wanaume 48,951 sawa na 82%
aliongeza Dkt Kulemba”
Aidha Dkt Kulemba ameongeza kuwa kwa mujibu wa
tafiti zilizofanyika nchini Kenya ,Uganda na Afrika Kusini maeneo
mengi ambayo tohara kwa wanaume ni utamaduni wao maambukizi ya UKIMWI yapo
chini ikilinganishwa na maeneo ambayo tohara ipo chini maambukizi yapo juu.
“maeneo ambayo tohara ni culture(utamaduni) yao maambukizi
ya virusi vya ukimwi yapo chini lakini kupitia wizara ya afya kwa kushirikiana
na shirika la Interhealth hayo yote yameweza kufanyika na ndio maana tukapata
matokeo haya ” alisema Dkt Kulemba .
MWISHO.
Mratibu wa Shughuli za Kudhiti na kupambana na UKIMWI, Dkt.
Khamis Kulemba akiwasilisha mada katika kikao cha wadau wa afya, kilichofanyika
kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Baadhi ya viongozi na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga, katika kikao
cha wadau hao, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakati akifunga kikao cha wadau hao, kwa niaba ya
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI
11 na 12, 2019.
0 comments:
Post a Comment