Rita
Paulsen, Hoyce Temu (Miss Tanzania 1999) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997)
wanatarajiwa kuwa majaji wa Shindano la kumsaka Miss Simiyu 2019, litakalofanyika
kesho Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani
Simiyu.
.
Hayo
yamesemwa Julai 04, 2019 na
Mkurugenzi wa Simiyu Talent Compay Ltd, Bi. Zena Mchujuko ambalo
linaandaa shindano hilo kwa kushirikiana na Grace Entertainment, wakati
akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi
Amesema kama waandaaji wameamua
kuwaleta majaji hao ambao ni mahiri na
wenye uzoefu katika masuala ya ulimbwende ili kupata Miss Simiyu ambaye atakuwa
na uwezo kuuwakilisha mkoa katika Shindano la Miss Tanzania.
“Tumeamua kuwaleta majaji hawa kwa
sababu ya uzito wa tukio lenyewe, uzoefu na umahiri wao, lengo letu ni kutoa
Miss Simiyu atakayeweza kutuwakilisha katika Miss Tanzania na tuna uhakika kila mshiriki atapata haki
yake” alisema Mchujuko.
Aidha, Mchujuko amesema Mgeni Rasmi
katika Shindano la Miss Simiyu 2019 atakuwa ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kwa upande wa Burudani Mwanamuziki
wa Kizazi kipya Nasib Abdul alimaarufu Diamond Platinum atatumbuiza shindano
hilo.
Kwa
upande wake mwalimu wa washiriki wa Miss Simiyu 2019 Doreen Robert Pastory alibainisha kuwa
majaji hao wanastahili kuwajaji warembo hao huku akiongeza kuwa suala la
urembo linatakiwa kuchukuliwa kama ajira nyingine badala ya kuchukulia kama
jambo la kihuni ambapo alitoa rai kwa Mikoa mingine kuiga jambo hilo kwani ni
ajira kama zilivyo ajira nyingine.
Naye
mmoja wa washiriki Rebeka Manoti amesema wamefundishwa kwa kuzingatia maadili
mema, hivyo wana matarajio makubwa ya kupata mlimbwende atakayepeperusha vyema
tasnia hiyo ya urembo kimkoa ,kitaifa na kidunia.
Jumla ya warembo 15 watachuana katika shindano hilo na
kiingilio itakuwa Shilingi 10,000 (Regular),Shilingi 50,000(Corparate) na Shilingi
100,000(VIP), na Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Shilingi Milioni moja na
washiriki wengine pia watapatiwa zawadi.
MWISHO
Mkurugenzi wa Simiyu Talent Compay Ltd, Bi. Zena Mchujuko ambayo
inaandaa shindano hilo kwa kushirikiana na Grace Entertainment, akizungumza na
waandishi wa habari Julai 04, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment