Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuongeza vituo vingine vya biashara ili iweze kuongeza hali ya ukusanyaji wa
mapato.
Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo jana wakati akizungumza na
madiwani na watendaji wa Halamshauri hiyo kwenye kikao cha Baraza maalumu la
madiwani llililokuwa na agenda moja ya kujadili hoja 21 za ukaguzi
zilizoibuliwa na mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali(CAG).
“ Anzisheni vyanzo vipya vya mapato lakini pia fungueni miji
mipya ya kibiashara mfano kule Bukundi daraja limeshajengwa hatuwezi kujenga
daraja la Sabaiti halafu kukaendelea kuwa pori, ni lazima Bukundi uwe mji
mwingine wa kibiashara kama Mwandoya, Mwanhuzi na ‘centres’ nyingine na
karibisheni sekta binafsi” alisema.
Katika hatua nyingine amewakaribisha wafanyabiashara wa mabasi
kupeleka magari yao Meatu ili kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri kwenda
Makao makuu ya mkoa na kuondoa changamoto ya usafiri iliyopo ambapo ni kampuni
moja tu inayofanya kazi wilayani humo na akawaasa polisi kutojihusisha na
uonevu dhidi ya wafanyabiashara na wananchi.
Kuhusu hoja za ukaguzi zilizoibuliwa na wa Mkoa wa Simiyu
Anthony Mtaka ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Meatu kujibu hoja za ukaguzi
zilizoibuliwa na mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali
(CAG)kuhakikisha zinajibiwa kwa wakati na kwa ufasaha huku akiwataka wataalam kutoa
ushirikiano kwa mkaguzi wa ndani.
Mtaka pia amemtaka mkaguzi wa ndani wa Halmashauri hiyo kuwa
jicho ili aisaidie halmashauri hiyo wakati wakitekeleza miradi mbalimbali huku
akisisitiza hoja zijibiwe kwa wakati bila ubabaishaji zikienda sambamba
na viambatanisho vya vielelezo vinavyojitosheleza.
Fabian Manoza ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo
ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na mkuu wa mkoa huo na
kuhalikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa mkaguzi wa ndani .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Pius Machungwa
alisema kwa mwaka 2016/2017 mkaguzi na mthibiti Mkuu 10 wa hesabu za serikali aliibua hoja za
ukaguzi 91 ambapo walipata hati ya mashaka, hivyo kwa mwaka huu wametekeleza
baadhi ya mapendekezo na kuwafanya kupata hati safi.
Alisema kwa mwaka huu (2017/18) mkaguzi ameibua hoja za ukaguzi
24 na kuifanya halmashauri hiyo kupata hati safi huku akiahidi kusimamia miradi
ili waendelee kupata hati safi na pia kumtumia mkaguzi wa ndani katika
usimamizi wa miradi
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Fabian Manoza alisema hoja nyingi
zilitokana na mambo ya ndani ambayo watendaji walitakiwa kuyadhibiti hasa
yatokanayo na ukusanyaji wa mapato ambapo wameanza kukusanya mapato kwa mfumo
wa kielektroniki (EFD).
Manoza alisema watamtumia mkaguzi wa ndani wanapotekeleza miradi
ili endapo akibaini kuna mapungufu aweze kuwajulisha na wayafanyie kazi.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
akizungumza na Madiwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakati wa Kikao maalum
cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe.
Pius Machungwa akifungua Kikao maalum
cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 .
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Meatu, bw.
Fabian Manoza akiwasilisha taarifa
katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 .
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, MHE. Anthony Mtaka (hayupo pichani)
katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, MHE. Anthony Mtaka (hayupo pichani)
katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018.
Baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya
Meatu wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani)
katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018.
Baadhi ya viongozi wa Serikali(mbele) wakifuatilia
kikao maalum cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
kwa mwaka 2017/2018.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,
mhe. Juma Mpina akichangia hoja katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani
chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
kwa mwaka 2017/2018.
0 comments:
Post a Comment