Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba amesema
Serikali imekaa na wanunuzi wa pamba na kwa pamoja wamekubali kuanza rasmi
kununua pamba kwa bei elekezi ya shilingi 1200 na ikiwa kutakuwa na hasara
watakayopata kutokana na bei ya zao hilo kushuka katika soko la dunia (baada ya
Agosti 15, 2019 ) Serikali itafidia.
Mhe. Mgumba ameyasema hayo katika nyakati tofauti wakati
akiwa kwenye ziara yake ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba katika
Wilaya ya Bariadi na Maswa Mkoani Simiyu.
Amesema awali wanunuzi wengi walisita kununua pamba
kwa bei kubwa na kuuza kwa bei ndogo kutokana na kushuka kwa bei ya pamba katika
soko la dunia, lakini Serikali kwa kuwathamini wakulima, imesema pamba
itanunuliwa kwa shilingi 1200 na ikiwa kuna hasara zozote za kibiashara
watakazopata wanunuzi baada ya tarehe 15/08/2019 serikali itafidia.
“Tumekubaliana na wanunuzi kuwa waingie rasmi sokoni
wanunue kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kama kuna kushuka bei au kutakuwa na hasara yoyote hayo Serikali itabeba lakini wao waendelee
kununua pamba kupitia vyama vya ushirika, msikubali kuuza pamba yenu chini ya
bei ya shilingi 1200” alisema Mhe. Mgumba.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mhe. Festo
Kiswaga amesema tayari wanunuzi wawili ambao ni NSAGALI na NGS Company wamepeleka
fedha katika Vyama vya ushirika vya Msingi wilayani Bariadi na wanunuzi wengine
wanaendelea kwenda kununua.
Nao wakulima waliotembelewa na Mhe. Naibu Waziri wa
Kilimo wameiomba Serikali kutoa mbegu, dawa na viuatilifu kwa wakati ili waweze
kuongeza tija katika uzalishaji jambo ambalo Mhe. Mgumba alilitolea ufafanuzi
kuwa linaendelea kushughulikiwa kwa kusajili wakulima ili kujua idadi kamili ya
wakulima na kutoa pembejeo za kutosha kulingana na idadi ya wakulima.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa kilimo, Mhe.
Omary Mgumba ametoa pole kwa wakulima wa Kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani
Maswa kwa naiba ya Serikali kutokana na tatizo walilopata la kuunguliwa na
pamba yao katika ghala ya Chama cha Ushirika cha msingi na kuelezwa
kusikitishwa sana na tukio hilo.
Akitoa salamu hizo za pole kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali
imesikitishwa sana janga hilo na iko pamoja nao, huku akitoa wito kwa wanachama
wa Chama cha Ushirika cha Msingi kuchukua tahadhali ya moto katika maeneo
waliyokusanya pamba.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe
ametoa wito kwa wanachama wa vyama vya ushirika kuchagua viongozi waadilifu.
MWISHO
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge
wilayani Maswa mkoani Simiyu, alipofika kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa
pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika Chama cha Ushirika
kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wakulima wa pamba mara baada ya kufika katika Chama
cha Ushirika cha Msingi cha Nyaumata Mjini Bariadi, wakati wa ziara yake ya
kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Baadhi ya wakulima wa
pamba wakipeleka pamba yao katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Nyaumata
Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(wa tatu kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba(wa nne kushoto) azungumze na wakulima
wa pamba wa Kijiji cha Mbiti wilayani Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua
mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(wa tatu kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba(wa nne kushoto) azungumze na wakulima
wa pamba wa Kijiji cha Mbiti wilayani Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua
mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Baadhi ya wananchi wa
kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa mkoani Simiyu, wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (hayupo pichani) alipofika kijijini hapo
kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa
katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wakulima wa pamba wa Kijiji cha Mbiti wilayani
Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Baadhi ya wananchi wa
kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa mkoani Simiyu, wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (hayupo pichani) alipofika kijijini hapo
kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa
katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Shinyanga Mwenge wilayani humo, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.
Omary Mgumba kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao
iliyokuwa imekusanywa katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto
siku kadhaa zilizopita.
Mmoja wa wananchi wa
kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa mkoani Simiyu, akiwasilisha hoja
yake kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.
Omary Mgumba (hayupo pichani) alipofika kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa
pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto
siku kadhaa zilizopita.
Mwakilishi wa Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa,
wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kijijini hapo
kuwapa pole kwa niaba ya Serikali, wakulima wa pamba kutokana na pamba yao
iliyokuwa imekusanywa katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku
kadhaa zilizopita.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge
wilayani Maswa mkoani Simiyu, alipofika kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa
pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika ghala la Chama cha
Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.
0 comments:
Post a Comment