Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amesema Mikoa
ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Nanenane ya Ziwa Mashariki
imekusudia kuboresha zaidi maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 ambayo yanafanyika kwa mara ya pili sasa
katika kanda hii kwenye Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Malima ameyasema hayo jana katika kikao maalum cha
maandalizi cha Kanda hiyo kilichofanyika kwa lengo la kutathmini hali ya maandalizi
ya maonesho hayo ambayo yanatarajia kuanza tarehe 29 Julai, 2019 na
kuhitimishwa rasmi Agosti 08, 2019.
Amesema kanda imekusudia kuboresha upatikanaji wa
huduma za maji, umeme na miundombinu mingine muhimu ikiwa ni pamoja na kuongeza
majengo ya kudumu ili katika siku za usoni kanda ya Ziwa Mashariki iwe sehemu
ya kudumu ya maonesho ya Kilimo Biashara.
“Mwaka huu tumekusudia kuboresha maonesho ya
Nanenane Kitaifa kuliko mwaka jana 2018, tumekubaliana kuboresha upatikanaji wa
huduma katika maeneo ya viwanja vua maonesho na pia tunakusudia kuongeza upatikanaji wa majengo
ya kudumu kwa sababu kwa kadri tunavyokwenda
tunatarajia hapa iwe ni sehemu ya Maonesho ya Kilimo Biashara kwa kanda
hii” alisema
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
amesema Maonesho ya Nanenane mwaka 2019 yatakuwa na waoneshaji wengi wa
teknolojia za kilimo kuliko miaka
iliyopia, hivyo akawahakikishia wananchi wote kuona teknolojia
mbalimbali ikiwa ni pamoja na za upukuchuaji, utengenezaji wa chakula cha
mifugo, ukataji majani ya mifugo, uvunaji na teknolojia nyingine nyingi.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Mazao Wizara ya Kilimo, Bw. Nyasebwa Chinagu amesema moja ya jukumu la
wizara hiyo katika Maonesho haya ni kuhakikisha kuwa teknolojia sahihi zilizopo
zinaoneshwa katika Maonesho ya nanenane ili wakulima, wafugaji na wavuvi waweze
kupata maarifa na teknolojia sahihi katika kuongeza tija katika uzalishaji.
Maonesho ya haya yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na
viongozi wengine wa Kitaifa watakuwepo katika siku maalum, akiwepo Waziri Mkuu
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo
Pinda na mgeni rasmi katika kilele cha maonesho haya anatarajiwa kuwa Rais wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanafanyika kwa mara ya
pili sasa mkoani Simiyu chini ya kauli Mbiu:-“KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KATIKA UKUAJI WA
UCHUMI WA NCHI” tangu Kanda ya Ziwa ilipogawanywa katika kanda mbili
yaani, Kanda ya Ziwa Mashariki(Simiyu, Mara na Shinyanga) na Kanda ya Ziwa
Magharibi(Mwanza, Geita na Kagera).
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Mhe. Adam Kighoma Malima akizungumza katika kikao cha Kamati ya maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, kilichofanyika Julai
23, 2019 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Kighoma Malima
wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha katika kikao cha
Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya NanenaneKitaifa 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, kilichofanyika Julai
23, 2019 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Kutoka kulia Mkuu wa
Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Kighoma
Malima wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka katika kikao cha Kamati
ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane 2019 yanayofanyika Kanda ya Ziwa
Mashariki, kilichofanyika Julai 23, 2019 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa
kikao cha Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019
yanayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki, kilichofanyika Julai 23, 2019 katika
Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya maandalizi ya Maonesho
ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki,
klichofanyika Julai 23, 2019 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Mhe. Adam Kighoma Malima(kulia) akizungumza katika kikao cha Kamati ya
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, kilichofanyika
Julai 23, 2019 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi, (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Baadhi
ya vipando vya mazao ya kilimo vilivyopo katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi
Simiyu
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akipewa maelezo ya ufugaji wa samaki katika banda la maonesho
la JKT katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
0 comments:
Post a Comment