Tume ya
Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la
kudumu la wapiga kura mkoani Simiyu kuanzia Julai 31, 2019 hadi Agosti 06, 2019 ambapo
zoezi hilo kitaifa lilizinduliwa rasmi Julai 18, 2019.
Akifungua
mkutano wa wadau wa Uchaguzi mkoani Simiyu, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema
Tume imekamilisha maandalizi ya uboreshaji daftari ambayo ni pamoja na kuhakiki
vituo vya kujiandikisha, uandikishaji wa majaribio, maandalizi ya vifaa vya
uboreshaji daftari, mkakati wa elimu kwa mpiga kura na uzinduzi wa uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Amesema
uboreshaji huu hautawahusisha wapiga kura wote walioandikishwa kwenye daftari
la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 bali utawahusu wapiga kura wapya ambao
wametimiza miaka 18, wale ambao watatimmiza.umri wa miaka 18 siku ya uchaguzi
Mkuu mwaka 2020, ambao wamehama katika maeneo ya awali ya uchaguzi na wale
ambao kadi zao zimeharibika
Katika
hatua nyingine Jaji Kaijage ametoa rai kwa wananchi wote wenye sifa kujitokeza
kwa wingi ili kuboresha taarifa zao, huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya
siasa, kuzingatia sheria za uchaguzi na kanuni zake katika zoezi hili la
uboreshaji na maelekezo kwa Vyama vya Siasa kuhusu uboreshaji.
Kwa upande
wake Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Frank Mhando
amesema Tume imefanya uhakiki wa vituo vya uandikishaji ambavyo vimeongezeka kutoka
36,549 mwaka 2015 hadi 37,407 mwaka 2018 (Tanzania Bara), upande wa Tanzania
Zanzibar vimeongezeka kutoka 380 mwaka 2015 hadi 407 mwaka 2018; huku
akifafanua kuwa katika uandishaji huu kila Kijiji au Mtaa utakuwa na angalau
Kituo kimoja cha kujiandikisha.
Naye
Mratibu wa Zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani
Simiyu, Bw. Maganga Simon amesema mkoa umejiandaa vizuri ili kufanikisha zoezi ambapo
wananchi wenye sifa zaidi ya 700,000 wanatarajia kuandikishwa katika daftari hilo
huku akiwasisitiza viongozi wote mkoani hapo kuwahamasisha wananchi wenye
sifa kujitokeza kujiandikisha.
“Mkoa wetu
ni mwenyeji wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka2019, tutatumia fursa hiyo
kuhamasisha, kutakuwa na bango kubwa litakaloonesha kuwa kuanza Julai 31
hadi Agosti 6 2019 mkoa wetu utashiriki kikamilifu kwenye zoezi la
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na Simiyu tumejipanga
kufanikisha zoezi hili ambalo linasimamiwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi”
alisema
Akizungumza
kwa niaba ya watu wenye ulemavu, Katibu
wa Chama cha Viziwi (CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Alex Benson amewaomba viongozi wa
vyama vya siasa kuwapa fursa watu wenye ulemavu kuwania nafasi mbalimbali, huku
akisisitiza wasimamizi kupewa mafunzo ya lugha ya alama ili kurahisisha mawasiliano na watu wenye ulemavu pindi wanapoenda kujiandikisha
na kupiga kura.
Naye Dora
Stephano kutoka katika ASASI za kiraia amesema Tume ione uwezekano wa kuongeza
ushirikishwaji wa asasi za kiraia nyingi zaidi, ili kuongeza wigo wa kutoa elimu
kwa wapiga kura juu ya masuala mbalimbali ya uandikishaji na uchaguzi.
Mkutano wa
wadau wa uchaguzi mkoani Simiyu, umewahusisha Mratibu wa Uandikishaji wa
Mkoa, Viongozi wa Vyama vya siasa Viongozi wa dini, wawakilishi wa watu wenye
ulemavu, wawakilishi wa vijana, wawakilishi wa wanawake, wawakilishi wa asasi
za kiraia, watendaji wa Tume na waandishi wa habari.
MWISHO
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi
Mkoani Simiyu, uliofanyika julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Bw. Frank Mhando akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoani
Simiyu, uliofanyika julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa
dini, , viongozi wa asasi zisizosa Kiserikali na wawakilishi wa vijna ,
wanawake na watu wenye ulemavu wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(hayupo
pichani) wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, Julai 20,
2019 Mjini Bariadi.

Vyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano
wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa
TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Frank Mhando
akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoani Simiyu,
uliofanyika julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi
Mkoani Simiyu, uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini Bariadi,(kulia) Mratibu wa Zoezi
la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Simiyu, Bw. Maganga
Simon.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(katikati walioketi) akiwa katika picha
ya pamoja viongozi wa dini mkoani Simiyu mara baada ya kufungua Mkutano wa
wadau wa Uchaguzi Mkoani humo, uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(katikati walioketi) akiwa katika picha
ya pamoja viongozi asasi mbalimbali za kiraia mkoani Simiyu mara baada ya kufungua
Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani humo, uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini
Bariadi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(katikati walioketi) akiwa katika picha
ya pamoja waandishi wa habari mkoani Simiyu mara baada ya kufungua Mkutano wa
wadau wa Uchaguzi Mkoani humo, uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa
Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(katikati walioketi) akiwa katika picha
ya pamoja Viongozi wa Vyama vya siasa mkoani Simiyu mara baada ya kufungua
Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani humo, uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa
Vyama vya siasana asasi za kiraia wakifuatilia
hotuba ya Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles
Kaijage(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani
Simiyu, Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg.
Mayunga George akichangia hoja katika Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani
Simiyu, uliofanyika julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Bi, Dora Stephano kutoka katika Asasi za Kiraia akichangia
hoja katika Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, uliofanyika Julai 20,
2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment