Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba
ametembelea Viwanja vya Nyakabindi kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yatakatofanyika kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019
katika Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu, ambapo ameridhishwa na
maaandalizi hayo ambayo amesema kwa sasa yamefikia zaidi ya asilimia 75.
Amesema maandalizi ya mwaka huu ni tofauti na mwaka
jana kutokana na mwaka jana kwa sababu mwaka jana yalikuwa ya dharura lakini
mwaka huu taasisi zimejipanga na baadhi
ya zimeanza kujenga majengo ya kudumu katika Viwanja vya Maonesho.
“ Maandalizi ya mwaka huu ni tofauti na mwaka jana
kwa sababu mwaka jana yalikuwa ni ya dharura lakini kwa udharura ule ule
tulifanikiwa kufanya vizuri lakini mwaka huu, maandalizi yamekuwa tofauti kwa
sababu majengo ya kudumu yameongezeka na niwahakikishie watu wote watakaokuja
kwenye maonesho mwaka huu kupata vitu vizuri” alisema Mgumba.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito
kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wadua wengine kushiriki katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2019 huku akiwahakikishia kuwa maonesho hayo yatakuwa
makubwa sana hivyo wategemee matokeo makubwa pia.
Kwa upande wake Mratibu wa Nanenane kutoka Wizara ya
Kilimo, Dkt. Kissa Kajigili amesema barabara zinazozunguka uwanja zenye urefu
wa kilometa sita zimeshachongwa na visima vinne vya maji vinachimbwa kuongeza
idadi ya viwili vilivyopo ili kuboresha huduma ya maji katika viwanja vya Nyakabindi.
Ameongeza kuwa Halmashauri zote 21 za Mikoa ya
Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Nanenane ya Ziwa Mashariki na
taasisi nyingine zimepanda vipando vya mazao mbalimbali kwa ajili ya
kuwaelimisha wakaulima, wafugaji na wavuvi ambavyo vinaendelea vizuri.
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yataanza
tarehe 28 Julai, 2018 na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan Agosti 01, 2019 na kufungwa Agosti 08, 2019 na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
MWISHO
Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba (wa pili
kushoto) akikagua vipando vya mazao ya kilimo ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa
maandalizi ya maoensho ya nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika
viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti
08, 2019..
Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba (wa pili kushoto) akipewa maelezo kuhusu vipando vya mazao ya kilimo ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa maandalizi ya maoensho ya nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba (wa nne
kulia) akiwa na baadhi ya viongozi na
wataalam wa Mkoa wa Simiyu na Wizara ya kilimo
katika ukaguzi wa maandalizi ya
maoensho ya nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya
Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019..
Naibu Waziri wa kilimo,
Mhe. Omary Mgumba kushoto akiangalia baadhi ya mazao yliyopandwa katika Kitalu
nyumba kilichopo Nyakabindi wakati wa
ziara yake ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019
yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia
Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimuongoza Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary
Mgumba kwenye moja ya majengo ya kudumu yanayojengwa na Jeshi la kujenga
Taifa(JKT) katika Viwanja vya Nanenane Nyakabindi Bariadi, wakati wa ziara yake
ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019
yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia
Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Mmoja wa Maafisa wa
JKT(wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba
alipotembekea moja ya majengo ya kudumu yanayojengwa na Jeshi hilo katika Viwanja vya Nanenane Nyakabindi
Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani
Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Moja ya majengo ya
kudumu yanayojengwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) katika Viwanja vya Nanenane
Nyakabindi Bariadi, ambalo litatumika katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka
2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu
kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Baadhi ya mazao yaliyo
kwenye vipando ambayo yameandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa
mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu
kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akimuonesha kitu Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary
Mgumba(kulia)wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani
Simiyu kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
Baadhi ya mazao yaliyo
kwenye vipando ambayo yameandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa
mwaka 2019 yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu
kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019.
0 comments:
Post a Comment