Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameitaka Halmashauri
ya wilaya ya Itilima kuhakikisha inawalipa madiwani wake malimbikizo ya madeni
kupitia fedha za makusanyo ya pamba mwaka huu ili kuondoa usumbufu ambao
unaweza kujitokeza pindi watakapokuwa wamemaliza muda wao.
Mtaka ameyasema hayo Julai 02, 2019 wakati akizungumza kwenye
kikao cha Baraza maalumu la madiwani llililokuwa na agenda moja ya
kujadili hoja 39 za ukaguzi zilizoibuliwa na mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu
za serikali ( CAG).
“ni vyema madeni ya
waheshimiwa madiwani yakalipwa kwa wakati ni ngumu kujadili vitu
vya kimaendeleo wakati wao wanadai, huwezi kushugulikia ya wengine wakati
yako hayako vizuri, ikumbukwe
wamebakiza muda mfupi baraza livunjwe …si vyema wakatoka madarakani huku
wakiwa wanadai”alisema Mtaka na kuongeza kuwa .
“Mkurugenzi hakikisha kipaumbele kwenye makusanyo ya pamba
unalipa madeni ya waheshimiwa hawa (madiwani) hakikisha unahuisha bima
zao, lakini kingine hakikisha unatenga fedha kwa ajili ya uchaguzi ” aliongeza.
Awali akisoma taarifa ya ripoti ya mkaguzi na mthibiti mkuu wa
hesabu za serikali (CAG ) mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Elizabeth
Gumbo alisema kwa mwaka wa fedha 2018/19 hoja zilizoibuliwa ni 39 na kuongeza
kuwa hoja 24 kati ya 39 zilizoibuliwa zilitolewa mapendekezo na kuwasilishwa
kwa mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali kwa ajili ya uhakiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mhe. Daudi Nyalamu
amesema madiwani wanadai zaidi ya shilingi milioni 360 huku akiongeza
tayari halmashauri imaishajipanga kulipa madeni yote kabla ya kuvunjwa kwa
baraza hilo.
Nao baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa kata ya Lugulu Robert
Jongela na gertuda ngokolo diwani wa viti maalum kutoka kata ya
ikindilo wamesema madeni yao ni ya muda mrefu tangu mwaka 2016 hadi 2019 hivyo
kupitia kauli ya mkuu wa mkoa huo imewapa faraja na hatua
hiyo imetoa tumain jipya la kupata stahiki zao,
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Madiwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
wakati wa Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2,
2019
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mhe. Daudi Nyalamu akifungua Kikao maalum cha
Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo akiwasilisha taarifa
katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2,
2019
Katibu Tawala wa mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza kabla ya kumkaribish Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani Halamshauri ya Wilaya ya Itilima chenye lengo
la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka
2017/2018 Julai 2, 2019.
Baadhi ya madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, MHE.
Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani
chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019
Baadhi ya madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, MHE.
Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani
chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019
Baadhi ya wakuu wa
idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
MHE. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani
chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019
0 comments:
Post a Comment