Wednesday, July 31, 2019

RAIS MAGUFULI KUZINDUA KAZI DATA YA WAKULIMA NANENANE KITAIFA SIMIYU: WAZIRI HASUNGA

Waziri wa Kilimo, Mhe.  Japhet Hasunga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Agosti 8, 2019 ,anatarajiwa kuzindua kanzi data ya usajili wa wakulima kupitia mazao nane ya kimkakati, itakayosaidia kujua idadi ya wakulima sambamba na wakulima  kujua takwimu za mazao na upatikanaji wa masoko kwa urahisi kupitia njia ya mtandao .


Mhe. Hasunga ameyasema hayo Julai 30, 2019 wkati akikagua maendeleo ya maandalizi ya maonesho ya Nanenane Kitaifa Mkoani Simiyu, ambapo amesema pamoja na kuzindua kanzi data ya wakulima Mhe. Rais Magufuli anatarajiwa pia kuzindua mfumo wa kielectroniki utakaosaidia kujua idadi ya wakulima, mahali walipo,mazao wanayolima na ukubwa wa maeneo wanayolima.

“Tunataka kili Mtanzania popote alipo akitaka takwimu sahihi awe anaweza kuingia kwenye mfumo na akaziona,  ukitaka wakulima wa pamba wa pamba waonekane, tukakitaka wakulima wa mkonge waonekane, tunataka tuwe na uwezo wa kuwaona wakulima wakubwa, wa kati na wadogo na mahali walipo” alisema Mhe. Hasunga.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa tarehe hiyo pia  Rais Dkt Magufuli atafungua soko la bidhaa ambalo litawawezesha  wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi ambayo itasaidia kupata uhakika wa bei na  kuepuka madalali na kuleta uwazi ili kila mkulima /mdau yoyote  aweze kuona na kujua  bei  sambamba na kufahamiana .

Waziri Hasunga amesema  kwa upande wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan , wakati  akizindua  maonesho ya nane nane Agosti  Mosi, 2019, anatarajiwa kuzungumzia masuala ya mazinigira  ambapo atazindua mkakati wa kuthibiti upotevu wa mazao utakao wezesha kujua hasara anazozipata mkulima hatua itakayopelekea kukabiliana nazo kwa wakati.

Aidha waziri Hasunga ameongeza kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa atazindua bima ya mazao ambayo itasaidia kukabiliana na vihatarishi vya mazao mfano ukame na mafuriko sambamba na kuona maendeleo ya ushirika nchini na nafasi ya ushirika na namna ambavyo unawaunganisha wakulima ,wafugaji na wavuvi.

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amemtembelea mmoja wa wajasiriamali kutoka wilaya ya Meatu  Deke Ndabuli Maige anayetengeneza mashine za kupukuchua mahindi ambapo mjasiriamali hiyo amesema kuwa alianza kutengeneza mashine hizo tangu mwaka 2014 na  hadi sasa ameshatengeneza mashine 10 na tayari ameshauza mashine 7.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa mashine hizo zinauwezo wa kupukuchua magunia 150 kwa siku huku akitumia lita saba za mafuta ya kuendeshea mashine hiyo kwa siku.

MWISHO


Waziri wa Kilimo, Mhe.  Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akipokea maelezo juu ya teknolojia rahisi ya upandaji wa mazao ya mbogamboga katika Vipando vya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.


Waziri wa Kilimo, Mhe.  Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akipokea maelezo juu matumizi ya zana za kisasa za kilimo katika Banda la Jeshi la kujenga Taifa(JKT), wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe.  Japhet Hasunga(kushoto), kuhusu jengo la Maonesho la Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga (aliyeyoosha mkono)akiangalia mbegu ya ulezi, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga (mbele)akiangalia vipando vya nyanya vya Jeshi la kujenga Taifa(JKT), wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani(kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(mwenye suti) juu ya mashine iliyotengnezwa na mjasiriamali  Deke Ndabuli Maige kutoka Meatu(wa pili kushoto)yenye uwezo wa kupukuchua gunia 150 kwa siku.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akimuonesha jambo Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga (wa pili kushoto) wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wakipewa elimu juu ya namna ya kutambua noti bandia katika banda la Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ikiwa ni maandalizi ya  Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Moja ya zana za kisasa zinazopaswa kutumiwa na wakulima ili kuongeza tija ya uzalishaji zilizopo katika Banda la Jeshi la kujenga Taifa(JKT), litakalooneshwa katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu..
Viatu vya ngozi vilivyotenegenezwa na Shirika la Uzalishaji Mali la SUMA JKT, ambavyo vitapatikana Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu

Baadhi ya kuku walio katika Banda la JKT katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu

Mtaalam wa JKT (kulia) akitoa maelezo juu ya namna ya kufuga asmaki kwenye matanki kwa Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga (wa nne kulia) katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu

Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga akiangalia  asali inayotoka mkoani Mra, mara baada ya kutembelea mabanda ya mkoa wa Mara, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Baadhi ya mabanda ya maonesho yakiwa yamekamilika ikiwa ni hatua za mwisho za maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Kitalu nyumba cha Halmashauri ya Manispaa ya Musoma

Baadhi ya bidhaa za JKT zinazouzwa kwenye banda lao katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga akipewa maelezo kuhusu mbegu za zao la mtama, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga akiangalia zao la mbogamboga aina ya kabichi katika vipando cya jeshi la Magereza, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!