Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Jambo Food Produsts Company,
Mhe. Salum Khamis na wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini Tamasha la
Simiyu Jambo Festival kuliendeleza tamasha hilo kwa lengo la kuwasaidia
wananchi wa mkoa wa Simiyu kuendeleza vipaji vyao katika sanaa, utamaduni na
michezo.
Mtaka ameyasema hayo
wakati akifunga Tamasha hilo Juni 30, 2019 Mjini Bariadi ambalo lilihusisha mashindano ya
ngoma za asili (Mbina Wagika na Wagalu), mashindano ya baiskeli kwa wanawake na
wanaume, mashindano ya mdahalo kwa wanafunzi wa shule za sekondari na mbio
fupi(fun run).
“ Namshukuru sana Mkurugenzi wa Jambo
Food Products Company Salum Khamis ambaye amekuwa mdhamini kwa miaka mitatu
mfululizo kwenye tamasha hili, nimuombe
yeye na kampuni yake waendelee kuunga mkono juhudi hizi kwenye eneo la michezo
na burudani, sisi ni viongozi leo tupo kesho hatupo, ni vizuri jambo hili ambalo
tumelianzisha kampuni yake iendelee kulimiliki kama makampuni mengine ya
vinywaji yanavyofanya” alisema ikaliendeleza.
Akizungumzia Kauli Mbiu ya Simiyu Jambo
Festival: WEZESHA MTOTO WA KIKE
ATIMIZE NDOTO ZAKE, INAWEZEKANA KUZUIA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO; Mtaka amesema ni vema watoto wa kike walindwe
ili waweze kuepuka mimba za utotoni na kufikia ndoto zao.
Akizungumza na wananchi wakati wa Tamasha la Simiyu Festival Mdhamini
Mkuu wa Tamasha hilo Mkurugenzi
wa Jambo Food Products Company Salum Khamis amesema Kampuni yake itaendelea
kudhamni tukio hilo na kuahidi kuendeleza tamasha hilo.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) mkoani Simiyu, Dkt. Amir
Batenga amesema moja ya ahadi za shirika
hilo ni kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao hivyo kupitia kauli mbiu ya tamasha hilo shirika hilo
lilifikisha ujumbe kwa vijana na wanaamini kila kijana anaweza kutimiza ndoto
zake.
Katika tamasha hilo washiriki zaidi ya
150 walishiriki mbio za baiskeli na mshindi wa kwanza kilometa 150 wanaume alijinyakulia kitita cha
shilingi 1,000,000/=, kilometa 80 wanawake shilingi 700,000 na walemavu kilometa
tano shilingi 500,000/=, huku ngoma za asili Wagika na Wagalu kila kikundi
kilijipatia shilingi 1,000,000/=
Simiyu
Jambo Festival mwaka 2019 imedhaminiwa na Jambo Food Products Company, Shirika la
Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani-UNFPA, NGM Gold Mine
Limited, NGS Petroleum, Alliance Ginneries Limited, Busega Mazao Limited, Maswa
Standard Chalk, Ms Hotel, Vetreces
Company Limited na NHIF.
MWISHO
Baadhi ya washiriki wa
mashindano ya baiskeli wakianza mashindano hayo katika Eneo la Salunda Mjini
Bariadi wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Juni 30, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (mwenye namba 0413) akiwaongoza baadhi ya viongozi na
wananchi katika mbio fupi za kilometa tano wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo
Festival liliofanyika Juni 30, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Jambo
Food Products Company, Salum Khamis akimkabidhi zawadi ya shilingi milioni moja
kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya mbio za baiskeli kilometa 150 wanaume
katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto )na viongozi wengine wakifurahia jambo katika
Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Msanii wa Kundi la
BASEKI Mjini Bariadi akionesha umahiri wake wa kucheza na nyoka aina ya chat, katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival
lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Washindi wa tatu wa mashindano
ya baiskeli kilometa 150 wanaume wakisubiri kupokea zawadi zao, wakati wa Tamasha
la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (mwenye fulana iliyoandikwa Jambo kifuani ) akicheza pamoja
na viongozi na wananchi wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival
lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (mwenye fulana iliyoandikwa Jambo kifuani ) akicheza pamoja
na viongozi na wananchi wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival
lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
kwa naiba ya wadhamni wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival wanaotoka Bariadi
katika tamasha hilo lililofanyika Juni 30, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Kampuni ya NGM Gold
Mine Ltd, Bw. Gungu Silanga kama ishara
ya shukrani kwa kukubali kudhamini Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika
Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi chetI cha shukrani Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) mkoani Simiyu, Dkt. Amir Batenga
kwa niaba ya shirika hilo kwa kukubali
kudhamini Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(mwenye kipaza sauti) na viongozi wengine wakiwa katika picha
ya pamoja na washindi wa mbio za baiskeli kwa watu wenye ulemavu, katika Tamasha
la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) mkoani
Simiyu, Dkt. Amir Batenga akizungumza na
wananchi wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika
Juni 30, 2019 Mjini Bariadi ambapo Shirika hilo lilikuwa moja ya wadhamini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi chetI cha shukrani Mwakilishi wa Shirika la Friedkin Conservation Fund Ltd kwa niaba ya shirika
hilo kwa kukubali kudhamini Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni
30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakiwa wameshika baadhi ya baiskeli zilizotolewa na Wheelchair
Foundation wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30,
2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (mwenye namba 0413 ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya viongozi mkoani hapa na washiriki wa mashindano yam bio za baiskeli walemavu
kilometa tano, wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni
30, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment