Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 2.2
kwa ajili ya kujenga jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Simiyu, ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma za kulaza wanawake na
watoto.
Waziri Ummy ameyasema hayo Julai 16, 2019 wakati
akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la maabara, jengo la
upasuaji ambalo pia litakuwa na huduma za mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Simiyu Mjini Bariadi.
Amesema wagonjwa wengi ni wanawake na watoto wadogo
hivyo ni vema wakajengewa wodi huku
akibainisha pia kuwa Serikali imeshatoa shilingi bilioni 5.7 kwa ajili ya
ujenzi wa jengo la maabara na jengo la upasuaji ambalo pia litakuwa na huduma
za mionzi unaotarajia kukamilika mwezi Oktoba 2019.
“Tulianza na ujenzi wa jengo la OPD, na awamu ya
pili namshukuru Mhe. Rais ametoa shilingi bilioni 5.7 kwa Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara, jengo la upasuaji ambalo
pia litakuwa na huduma za mionzi”
“Sasa hivi tuna shilingi bilioni 2.2 kwenye akaunti
ya Hospitali na tutaanza kujenga jengo la mama na mtoto, ili tuanze kulaza wagonjwa
maana hata ukiangalia wagonjwa wengi ni
wanawake na watoto wadogo, hili la wodi za watu wengine nalo pia tunalibeba”
alisema Waziri Ummy.
Aidha, Mhe. Waziri amepongeza wakala wa Majengo TBA
mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa huku
akimtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kurejesha fedha zilizokatwa
kodi(withholding tax) wakati akilipa TBA gharama za ujenzi, ili zifanye kazi ya
ujenzi maana TBA kama Taasisi ya Umma haipaswi kukatwa fedha hizo.
Naye Meneja wa TBA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.
Likimaitare Naunga amesema ikiwa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 204
zilizokatwa kama kodi “Withholding Tax” zikirejeshwa zitasaidia kununua vifaa
vya kukamilishia majengo hayo.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony
Mtaka ameishukuru Serikali kwa kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa
majengo hayo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, ambayo yataendelea
kuboresha huduma kwa wananchi, ambapo pia ameishukuru wizara ya afya kwa
kuendelea kusimamia kwa karibu ujenzi wa majengo hayo.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock
Yakobo amesema CCM kama wasimamizi wa utekelezaji wa Ilani wanashukuru kwa
namna Serikali inavyotekeleza ilani katika kuboresha huduma za afya Mkoani
Simiyu na ameahidi kuwa wataendela kufuatilia na kusimamia
kwa karibu ili kuhakikisha huduma bora zinatolewa.
MWISHO
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa
pili kulia) akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara ya
kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA
Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Likimaitare
Naunga (katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) kuhusu Ujenzi wa
Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Simiyu wakati wa ziara ya Waziri huyo
yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo, Julai 16, 2019
Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili
kushoto) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakioneshwa ramani ya jengo la Upasuaji
wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara,
upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019
Mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya(kushoto) ) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia mbele)
kuhusu Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara
ya Waziri huyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo,
Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Sehemu ya mbele ya
Jengo la Upasuajia ambalo sehemu itatumika kama Jengo la Mionzi ambalo
linaendelea kujengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Sehemu ya mbele ya
Jengo la Maabara ambalo linaendelea kujengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Simiyu.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia)
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiangalia kitu kwa makini katika Jengo la Upasuajia
ambalo sehemu itatumika kama Jengo la Mionzi ambalo linaendelea kujengwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Mwakilishi wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya(wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia
mbele) kuhusu Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu wakati wa
ziara ya Waziri huyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa
majengo hayo, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia)
na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakikagua jengo la Upasuaji wakati alipofanya
ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia)
na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakielekea kukagua jengo la Upasuaji wakati
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji
na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini
Bariadi.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia)
akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) kuhusu Ujenzi wa
jengo la upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu wakati
wa ziara ya Waziri huyo yenye lengo la
kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili
kushoto) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakioneshwa ramani ya jengo la Upasuaji
wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara,
upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019
Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati)
akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment