Tuesday, July 2, 2019

WHEELCHAIR FOUNDATION YAKABIDHI BAISKELI 48 ZA WALEMAVU MKOANI SIMIYU

Mwakilishi wa Wheelchair Foundation ya nchini Marekani Charli Butterfield amekabidhi baiskeli 48 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya watu wenye ulemavu mkoani hapa.


Awali akipokea baiskeli hizo  Mtaka ameishukuru taasisi hiyo kwa msada huuo na  kutambua mahitaji ya watu wenye ulemavu ambao wanakabiliwa changamoto ya vifaa saidizi, huku akibainisha kuwwa mkoa utaendeleza uhusiano na shirika hilo..

Kwa upande wake mwakilishi wa Taasisi ya Wheelchair Foundation Charli amesema utoaji wa vifaa saidizi vya walemavu ni endelevu na shirika hilo limetoa zaidi ya baiskeli 4000 katika nchi mbalimbali Barani Afrika.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Enock Yakobo  ameshukuru shirika la Wheelchair Foundation kwa msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu na kubainisha kuwa jamii ya wana Simiyu itaendelea kuwakumbuka.

Mmoja wa watu wenye ulemavu aliyenufaika na baiskeli akishukuru  kwa niaba ya wenzake amesema baiskeli hizo zitawasaidia sana kama kifaa saidizi kwao maana awali ilikuwa inawalazimu kujongea kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa shida.
MWISHO




Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na watu wenye ulemavu mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) mara baada kupokea msaada wa baiskeli 48 kwa ajili ya watu wenye ulemavu kutoka Taasisi ya Wheelchair Foundation ya nchini Marekani Juni 30, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akishukuru mara baada msaada wa baiskeli 48 kutoka Taasisi ya Wheelchair Foundation ya nchini Marekani Juni 30, 2019 kushoto ni mwakilishi wa Taasisi hiyo Charli Butterfield.

Mwakilishi wa Wheelchair Foundation ya nchini Marekani Charli Butterfield(kushoto) akimkabidhi kitabu kilichoandikwa na mwasisi wa Taasisi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada makabidhiano ya msaada wa baiskeli 48 kwa ajili ya watu wenye ulemavu
Baadhi ya baiskeli zilizotolewa kwa ajili ya watu wenye ulemavu mkoani Simiyu na Taasisi ya Wheelchair Foundation ya nchini Marekani Juni 30, 2019
Mwakilishi wa Wheelchair Foundation ya nchini Marekani Charli Butterfield (katikati) akimuonesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kupitia simu yake, mara baada ya makabidhiano ya baiskeli 48 kwa ajili ya watu wenye ulemavu, kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye fulana ya Jambo) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mkoani Simiyu na baadhi ya watu kutoka Taasisi ya Wheelchair Foundation walipomtembelea ofisini kwake Juni 30, 2019.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!