Wednesday, September 6, 2017

RAS SAGINI ATOA SALAMU KWA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WANAOANZA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA LEO

Ninafahamu kuwa leo tarehe 06/09/2017 vijana wetu walioanza darasa la Saba wanaanza mitihani yao ya siku 2 ikiwa ni hatua muhimu ya kuhitimu Elimu ya msingi.

Najua kwamba walimu, wazazi, walezi na viongozi wa ngazi zote wametimiza wajibu wao na wanafunzi pia wamejiandaa vizuri. Nachukua nafasi hii kuwaombea ufanisi vijana wetu wote wanaofanya mitihani  kesho na keshokutwa.

Nawatakia heri watoto wote wa Mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla. Nawaombea utulivu wa akili na umahiri katika kujibu maswali yote ili wapate ufaulu ulio bora na hivyo kuanza vema safari yao ya kitaaluma.

Aidha, wasimamizi wote wafanye kazi hiyo kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuwa na matokeo yanayoaminika. Baraka za Mungu ziwe kwenu nyote.


Jumanne Abdallah Sagini
Katibu Tawala Mkoa Simiyu
06/09/2017

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Abdallah  Sagini

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!