Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ametoa wito kwa viongozi wa dini na waganga wa tiba asili mkoani Simiyu kushirikiana na Serikali katika juhudi mbalimbali za kupunguza vifo vya wakina mama wajawazito na watoto vitokanavyo na uzazi.
Mmbaga
ameyasema hayo katika kikao chake na viongozi wa dini na waganga wa tiba asili
wilayani Itilima, kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya
wilaya hiyo Lagangabilili.
“Sisi
kama mkoa tunasema hatutaki kuona mwanamke yeyote anapoteza maisha wakati
akijifungua na mtoto akipoteza maisha wakati anazaliwa tunasema waliokufa sasa
basi, ni muhimu viongozi wa dini na waganga wa jadi wakashirikiana na Serikali
katika kueleimisha jamii juu ya umuhimu wanawake wajawazito kupata huduma stahiki za afya kwa wakati, tunajua haya makundi yanakutana na
yanawahudumia watu wengi,” alisema Mmbaga.
Aidha,
Mmbaga amesema Serikali inatambua mchango na kazi nzuri inayofanywa na viongozi
wa dini kupitia kamati za amani huku akisisitiza kamati hizo ziendelee
kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto
mbalimbali zinazokutana na taasisi wanazozisimamia (madhehebu ya dini).
Wakati
huo huo Mmbaga ametoa rai kwa waganga wa tiba asili mkoani Simiyu kuchagua
viongozi waadilifu watakaowaunganisha pamoja na kuwa msaada kwao katika kutatua
changamoto mbalimbali zinazowakabili ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia sheria, miongozo, kanuni na taratibu za nchi zilizowekwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amewapongeza waganga wa tiba asili
kwa kuwa wadau muhimu wa maendeleo katika wilaya hiyo kwa kuchangia ujenzi wa
vyumba vya madarasa, kutoa chakula kwa ajili ya wanafunzi wanaokuwa katika
kambi za kitaaluma; huku akiwaomba waimarishe umoja wao na kuwa na uongozi
imara ili waweze kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.
Mchungaji
wa Kanisa la EAGT Lagangabilili ameomba Serikali ione uwezekano wa kuunda
chombo kitakachowasaidia viongozi wa dini na waganga wa tiba asili ili makundi
hayo yaweze kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya sheria, kanuni, taratibu na
miongozo inayotolewa na serikali, huku Padri Ivo Komba akitoa wito kwa viongozi
wa dini kuwaongoza waumini wao katika imani ya kweli iliyo thabiti mbele za
Mwenyezi Mungu.
Kwa
upande wake Bw. Tandala Shuri Mganga wa asili kutoka kata ya Nkoma ameomba
waganga wa tiba asili washirikiane na viongozi wa dini kufanya kazi kwa kufuata
taratibu huku akieleza kuwa baadhi ya waganga wa tiba asili siyo waaminifu
wamekuwa wakikiuka taratibu zilizowekwa hivyo akaiomba serikali isisite
kuwachukulia hatua waganga wote watakaokwenda kinyume cha sheria zilizopo.
“Tunaomba
serikali ishughulike na waganga wahalifu na sisi waganga ndiyo tuwe mstari wa
mbele kuwafichua wahalifu hao ili uhalifua wao usituchafue waganga wote,
tufuate utaratibu unatakiwa na serikali katika kufanya kazi zetu tusitafute kugombana
na serikali,” alisema Tandala Shauri.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Dkt. Anold Musiba amesema waganga wote wanapaswa kuomba leseni za kuendesha shughuli zao ili waweze kutambulika kisheria ambapo mpaka sasa jumla ya waganga wa tiba asili 1387 wametambuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Aidha, Dkt. Musiba ametumia fursa hiyo kuwaomba
waganga hao kuwaelekeza wakina mama wajawazito, wakina mama wenye watoto wenye
utapiamlo mkali na matatizo yote ya lishe kufika katika vituo vya kutolea
huduma za afya mapema.
MWISHO
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya viongozi
wa dini na waganga wa tiba asili wa
wilaya ya Itilima, katika kikao kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika
makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Baadhi ya viongozi wa
dini na waganga wa tiba asili wa wilaya
ya Itilima, wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga, kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo
Lagangabilili.
Baadhi ya viongozi wa
dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima, wakiwa katika kikao na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) , kilichofanyika
jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe. Benson Kilangi akizungumza katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba
asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika
jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Tandala Shauri Mmoja wa
waganga wa tiba asili akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba
asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao
makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Mchungaji wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Lagangabilili Itilima
akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba asili wa wilaya ya
Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo
Lagangabilili.
Mbunge wa Jimbo la
Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba
asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao
makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Itilima, Dkt. Anold Musiba akifafanua jambo katika kikao cha Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga
wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika
makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Paroko wa Kanisa
Katoliki Parokia ya Kilulu wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na
waganga wa tiba asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26,
2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Mmoja wa Waganga wa
tiba asili wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba
asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao
makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Mmoja wa Waganga wa
tiba asili wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa tiba
asili wa wilaya ya Itilima kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao
makuu ya Wilaya hiyo Lagangabilili.
Baadhi ya viongozi wa
dini na waganga wa tiba asili wa wilaya
ya Itilima, wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga, kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo
Lagangabilili.
Baadhi ya viongozi wa
dini na waganga wa tiba asili wa wilaya
ya Itilima, wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga, kilichofanyika jana Februari 26, 2021 katika makao makuu ya Wilaya hiyo
Lagangabilili.
0 comments:
Post a Comment