Saturday, February 27, 2021

KILA MTUMISHI ITILIMA ASHIRIKI KIKAMILIFU UKUSANYAJI WA MAPATO: RAS SIMIYU

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu kuwa sehemu ya Halmashauri hiyo katika ukusanyaji wa mapato ili Halmashauri hiyo iweze kupanda katika ukusanyaji mapato na  kupata uwezo wa kujiendesha.

Mmbaga ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

‘Halmashauri yetu haifanyi vizuri katika ukusanyaji wa mapato, kutokana na hali hii ya ukusanyaji baadi ya masuala yenu muhimu kama watumishi mnaweza msiyapate kwa wakati hivyo kila mtumishi ajulikane kama afisa mapato wa halmashauri, hili si jukumu la Mkurugenzi na Mtunza Hazina wa Halmashauri pekee, wote mshirikiane kukusanaya mapato kwa uadilifu,” alisema Mmbaga.

Aidha, Mmbaga amewataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kuwa waangalifu katika matumizi ya mapato yanayokusanywa kwa kuhakikisha wanawekeza katika maeneo yenye tija na matokeo.

Sambamba na hilo Mmbaga amewataka watumishi hao kuziba mianya yote ya ubadhilifu na kumwataka viongozi kuwachukulia hatua watumishi watakaothibitika pasipo shaka kuwa wamefanya ubadhilifu wa mali za umma na katu wasiwafumbie macho.

Kwa upande wao watumishi wa lioshiriki katika kikao hicho walipata fursa fursa ya kuwasilisha changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuomba Katibu Tawala wa Mkoa kama Mkuu wa Utumishi wa Umma ndani ya Mkoa aweze kuzipatia ufumbuzi ambazo ni kulipwa stahiki zao ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara, madai ya fedha za kujikimu na nauli kwa watumishi wapya, upandishwaji wa madaraja na suala la uhamisho.

Katika kuyapatia ufumbuzi masuala haya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema ni vema wakuu wa taasisi wapewe taarifa sahihi juu ya upandishwaji wa madaraja na uhamisho wa watumishi ili waweze kuwaelimisha na kuwapa taarifa sahihi za masuala hayo watumishi walio chini yao.

Aidha, Mmbaga amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya itilima kuweka mpango mkakati wa kulipa madai mbalimbali ya watumishi ikiwa ni pamoja na nauli na fedha za kujikimu ili waweze kulipwa kulingana na halmashauri itakavyopata fedha.

Naye Afisa Utumishi wa Halmashauri amesema suala la kupandishwa madaraja kwa watumishi walioajiriwa kuanzia mwaka 2014 halijafanyika kwa nchi nzima si kwa Itilima peke yake hivyo amewasihi watumishi hao kuendelea kuwa watulivu mpaka yatakapotolewa maelekezo na Ofisi ya Rais Utumishi juu ya upandishaji wa vyeo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo amewataka wakuu wa shule na wakuu wa Vituo vya kutolea huduma za afya wilayani humo kuyawekea mipaka asili maeneo yaliyo chini yao ili kuepusha maeneo hayo kuvamiwa na wananchi ambapo uvamizi huo unaweza kuleta migogoro katika jamii inayozunguka taasisi hizo.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akiwa katika kikao pamoja nao wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo akifafanua jambo katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya watumishi wa  tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji, Bi. Kija Kayenze akifafanua jambo katika katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya watumishi wa  tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Upendo Haule akifafanua jambo katika katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya watumishi wa  tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akiwa katika kikao pamoja nao wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

Mmoja wa watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!