WIZARA
YA ELIMU YAAHIDI KUTOA FEDHA UJENZI WA CHUO VETA SIMIYU
Na Stella Kalinga,
Simiyu RS
Naibu waziri wa Elimu, sayansi na teknolojia, Mhe.Omary Kipanga amesema Wizara hiyo itahakikisha inatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA cha mkoa wa Simiyu ili kutimiza azma ya serikali ya kila mkoa na wilaya kuwa na chuo cha Mafunzo ya ufundi stadi (VETA).
Kipanga ameyasema hayo
Februari 16, 2021 wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi
wa vyuo vya VETA ambapo kwa mkoa wa Simiyu alipata fursa ya kutembelea eneo
lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA cha mkoa katika Mtaa wa
Bunamhala Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Naibu waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omari Juma Kipanga (katikati) akizungumza jambo na
baadhi ya viongozi wakati alipotembelea Chuo cha Maendelea ya Jamii Bariadi
kilichopo Mtaa wa Bunamhala Februari 16, 2021 wakati wa ziara yake ya siku moja
mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment