Tuesday, September 5, 2017

RC MTAKA APIGA MARUFUKU USHURU WA BIASHARA NDOGONDOGO MAARUFU KAMA MATANDIKO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amepiga marufuku Halmashauri zote Mkoani humo kutoza ushuru wa biashara ndogondogo zinazofanywa na wananchi kwa kutandika na kupanga bidhaa zao chini au kuuzwa katika mabeseni maarufu kama matandiko.

Mtaka ametoa agizo hilo baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Igaganulwa, Mhe.Nhandi Masaka Kachala na baadhi ya wananchi kutoa malalamiko yao kuhusu ushuru huo, wakati wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi .

Amesema suala hilo lilishatolewa maelekezo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, hivyo Halmashauri zinapaswa kubuni vyanzo vipya vya mapato vyenye tija kwa Halmashauri na wananchi badala ya kutegemea kutoza ushuru unaowakwaza wananchi.

“Kama kuna Halmashauri bado inatoza ushuru wa matandiko wamechelewa sana, kuanzia kesho hamna huo ushuru, kama ninyi mnafikiri mapato ni kutoza tandiko la nyanya, dagaa, mchicha na ninyi  kama wakuu wa idara hiki ndicho chanzo mnachokifikiria kichwani hiyo kazi haiwafai, mkatafute kazi nyingine ya kufanya” alisema Mtaka.

 “Halmashauri lazima ibuni chanzo cha mapato chenye tija kwenye Halmashauri na watu. Sasa mtu anahangaika na beseni lake la nyanya wewe unamtoza ushuru, umechangia nini, beseni si lako nyanya si zako” alisema Mtaka.

Aidha, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  kuhakikisha kuwa inarejesha asilimia Kumi ya mapato yanayokusanywa inayokusanywa kutoka katika vijiji vyote kwenye kila robo mwaka ili Vijiji hivyo viweze kutekeleza mipango ya maendeleo iliyowekwa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewahamasisha wananchi kuendelea kulima pamba kwa kuwa Serikali imekusudia kujenga kiwanda cha bidhaa ya Afya zitokanazo na zao la pamba mkoani humo na wataalam wanaofanya upembuzi yakinifu wanatarajia kufika Mkoani Simiyu Septemba 20 mwaka huu kuja kuona eneo kitakapojengwa kiwanda.

Amesema wananchi wasikate tamaa kulima pamba kwa sababu ya matatizo ya kihistoria na kuwaeleza kuwa, Serikali ya Mkoa imepanga mikakati madhubuti ya kuirudisha pamba kuwa dhahabu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata mbegu bora, dawa, pembejeo zote na suala la bei ya pamba itaanza kujadiliwa mapema.

Ameongeza kuwa wananchi wasiache kulima mazao jamii ya mikunde hususani choroko na dengu kwa kuwa Serikali inashughulikia suala la upatikanaji wa soko la uhakiki pamoja na kupunguza au kuondoa kabisa  madalali katika biashara ya mazao hayo ili wananchi wanufaike kupitia kilimo.

Akitolea ufafanuzi hoja ya Diwani wa Kata ya Ikungulyabashashi Mhe.Bupi Maduhu Litunga ya kupimiwa maeneo, Mkuu wa Mkoa huyo wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi kupitia Idara ya Ardhi, kuitisha mikutano katika Vijiji vyote ambavyo wananchi wanahitaji  kupimiwa maeneo na baadae awasilishe mihutasari ya vikao hivyo Ofisini kwake tarehe 13/09/2017.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amekamilisha ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambapo amesikiliza na kutatua kero za wananchi katika sekta ya Elimu,Afya, Kilimo, Mifugo, Ardhi, Ujenzi, Biashara na Uchumi pamoja na suala la utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA) ambazo amezitolea maelekezo na ameahidi kufuatilia utekelezaji wake.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa(hawapo pichani) Wilayani Bariadi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa  wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga  akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa  wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  aliyofanya  Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Diwani wa Kata ya Dutwa Wilayani Bariadi, Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa akizungumza na wananchi wa Kata hiyo (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa  wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  aliyofanya  Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na  wajumbe wa Serikali ya Kijiji  cha Igaganulwa Kata ya Dutwa (hawapo pichani) Wilayani Bariadi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kijijini hapo  wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Diwani wa Kata ya Sapiwi, Mhe. James Kibuga Wilayani Bariadi akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa  wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  aliyofanya  Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi akifafanua jambo katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa  wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  aliyofanya  Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Mkoa wa Simiyu, Jarlath Mushashu akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa juu ya umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka  aliyofanya  Wilayani Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Dutwa wakimsikiliza wilayani Bariadi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mpina Nkwabi Mkazi wa Dutwa Wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ziara yake wilayani humo yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthoy Mtaka akiwaonesha Kadi ya matibabu kwa Wazee inayotolewa kwa wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuwasihi wazee ambao hawajaajiandikisha wajiandikishe wakati wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthoy Mtaka akiwaonesha Kadi ya matibabu kwa Wazee inayotolewa kwa wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuwasihi wazee ambao hawajaajiandikisha wajiandikishe wakati wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya Viongozi na Wataalam kutoka Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Bariadi wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wananchi wa Kata ya Dutwa katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa  wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  aliyofanya  Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Sunday, September 3, 2017

ASKOFU SANGU AWATAKA VIJANA WASIKUBALI KUTUMIWA KULETA CHUKI, FITINA NA MAFARAKANO

Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu amewataka Vijana kutokubali kutumiwa kuleta vurugu, chuki na mafarakano hapa nchini.

Askofu Sangu ametoa wito huo wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

“......Maandiko Matakatifu yanasema Vijana wana nguvu;  kwa hiyo nawasihi vijana popote pale mlipo muwe chimbuko la Upendo, furaha na amani; watu wengine wasitumie nguvu zenu vijana kuleta chuki, fitina na mafarakano, muwe macho” alisema Askofu Sangu.

Askofu Sangu amewaasa waumini wa Kanisa hilo kuishi maisha mema ambayo hayatakuwa chanzo cha mateso kwa watu wengine katika familia, jumuiya , jamii wanaoishi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, amewataka Watanzania wote kupinga na kukemea mauaji ya watu wenye ualbino kwa kuwa wanayo haki ya kuishi kama watu wengine na watu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa Kanisa kuwa na mtazamo wa  kuisaidia nchi katika kupambana na tatizo la ajira hususani  kwa vijana.

Ameongeza kuwa ni vema Kanisa liyavae maneno ya Mhe.Rais kuhusu Ujenzi wa Tanzania ya Uchumi wa Kati na kuona namna linavyoweza kushiriki katika kufikia Tanzania Mpya, kwa kuimarisha  Idara za Kanisa na Vyama vya Kitume na kuzijenga idara na vyama hivyo katika  mtazamo wa Kiujasiriamali.

“Kanisa lione namna gani WAWATA tulionao wanakuwa WAWATA wa miradi, VIWAWA wanakuwa wa miradi, TYCS wa miradi, lakini sasa Vyama vyetu vya Kitume navyo pia vianze kujielekeza kusaidia Kanisa kwenye eneo la miradi”amesema Mtaka.

Mtaka amesema upo umuhimu wa kufanya semina za Ujasiriamali kwa vijana, wanawake na Vyama vya Kitume katika Kanisa  na waumini wote kwa ujumla ili kuwa na waumini waliojengwa kiuchumi na wanaoendana na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati.
Akiwa katika Ziara yake Mkoani Simiyu, Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu , Jumamosi Septemba 02 alizindua Parokia mpya ya Mtakatifu Luka iliyopo  Mjini BARIADI,  sambamba na kutoa kipaimara na leo ametoa kipaimara kwa vijana 164, katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyoongozwa na Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwapaka mafuta vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika  katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwabariki vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika  katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Baadhi ya Vijana waliopata Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiimba katika ibada .
Kwaya ya Shirikisho ikiimba  katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika  katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu  akiingia katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi ambapo aliongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (mwenye shati jeupe) na Mkewe Neema Mbiha(kulia) wakifuatilia mahubiri wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi iliyoongozwa na Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
Vijana wa Kipaimara (wenye sare ya rangi nyekundu) katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiingia  Kanisani kwa ajili ya ibada ya Sakramenti hiyo, ambayo iliongozwa Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu  akizindua Kitabu cha “MWANZO WA KUWA TAJIRI” wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi, kilichoandikwa na Muumini wa Kanisa hilo Ndg.Vincent Mabula Jilala.
Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu (katikati), Paroko wa Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi Padre Kizito(kulia) Nyanga na Mapadri wengine wakifuatilia Ujumbe wa Mkuu wa Mkoa wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John wakiwa katikaIbada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyoongozwa na Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu (hayupo pichani)

Friday, September 1, 2017

WANANCHI WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi Wilayani Bariadi mkoani humo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).

Mtaka ametoa wito huo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Amesema azma ya Serikali ni kuwa ifikapo mwaka 2020 Watanzania wote wawe wamejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) au Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), hivyo akawahamasisha wananchi ambao bado hawajajiunga na CHF kujiunga kwa kuwa gharama yake ni nafuu.

“Watu wa Ngulyati ni wafanyabiashara wazuri, wafanyakazi wazuri, wakulima wazuri ningetamani kuwaona wote hapa mnakuwa na kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii ambazo zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000, hii ni sawa na kuku mmoja tu mnapata matibabu watu sita  kwa maana ya baba, mama na watoto wa nne” amesema.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya ili wananchi waweze kupata huduma bora, ambapo Serikali kupitia Mradi wa RBF(Result Based Financing/Kulipa kulingana na Matokeo) imetoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma.

Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela amesema, kupitia mradi wa RBF Halmashauri hiyo imepokea shilingi milioni 260, zilizogawanywa katika vituo vilivyopo 26 vya kutolea huduma za afya ambapo kila kituo kimepokea shilingi Milioni 10 ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga kufuatilia na kuhakikisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi anawasilisha kwake taarifa ya fedha za Mradi wa RBF alizopokea na kazi zilizofanyika katika vituo vya kutolea huduma.

“Mhe. DC umesikia hapa hawa watu wamepokea fedha toka mwezi saba mwaka huu na leo ndio wamekaa kikao cha mpango,  maana yake ni kwamba mwezi wa nane wananchi hawajapata huduma zilizokusudiwa na Wizara ya Afya, na naamini yanayofanyika kwenye kituo hiki yapo katika vituo vyako vyote, sasa nimuombe Mkurugenzi wa Mji Jumatatu atuletee taarifa ya  mpango uliotekelezeka” amesema Mtaka.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuwa atalifuatilia suala hilo pamoja na kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa katika ziara hiyo na ameahidi kuwachukulia hatua watumishi watakaoshindwa kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wananchi.

Kuhusu suala la taratibu za uwekaji wa umeme wa REA awamu ya III kwa wananchi na Taasisi za Umma ambalo liliwasilishwa na wananchi akiwemo Mwl. Daudi Jackson, Mkuu wa Mkoa, Mhe.Anthony Mtaka amesema atakutana na Meneja wa TANESCO Mkoa siku ya Jumatatu Septemba 04, ili wajadili namna na kushughulikia suala hilo.

Katika hatua nyingine Mtaka  amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuhakikisha Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri anafika eneo la ujenzi wa Soko la Ngulyati Jumatatu tarehe 04 Septemba kukutana na viongozi wa Kijiji na Kata, kwa ajili ya kuanza mpango wa ujenzi wa soko hilo ili kutatua kero ya ukosefu wa soko na kuwawezesha wananchi kupata sehemu ya kuuzia bidhaa zao.


Wakati huo huo Mtaka amewataka wananchi kutumia vizuri msimu wa kilimo, kulima mazao yanayostahimili ukame na akawasisitiza kutunza chakula walichokipata katika msimu uliopita kwasababu Serikali haitakuwa na chakula cha msaada.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizugumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi katika Mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Mchungaji Nicholuos Chimbu mkazi wa Kijiji cha Ngulyati(kulia) wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Kata ya Ngulyati aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Minza Maduhu mkazi wa Kijiji cha Ngulyati wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi.
Eliasi Hopi mkazi wa Kijiji cha Nyasosi Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi aliwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi.
Afisa Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Simiyu akitolea ufafanuzi suala la utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini REA Awamu ya III ambalo liliulizwa na wananchi wa Kata ya Ngulyati wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyoifanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Bariadi wakisikiliza kwa makini kero mbalimbali zilizokuwa zikiwasilshwa na wananchi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyoifanya katika kata ya Ngulyati wilayani Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyoifanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Afya yaliyoulizwa na wananchi wa Kata ya Ngulyati wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyoifanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Diwani wa Kata ya Ngulyati Mhe.Mganga Ndamo Kanagana akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyoifanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Bariadi wakisikiliza kwa makini ufafanuzi na maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) juu ya kero na hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Ngulyati wilayani Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kikundi cha Burudani cha Msanii Polepole kutoka Ngulyati kikitoa burudani ka wananchi na viongozi katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) aliyoifanya katika kata ya Ngulyati wilayani Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mablimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Thursday, August 31, 2017

RC MTAKA: ZOEZI LA KUONDOA MIFUGO KWENYE MAENEO YA HIFADHI LIFANYIKE KWA WELEDI, HAKI NA UADILIFU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Meatu mkoani humo, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Dkt. Joseph Chilongani kutekeleza kwa weledi, uadilifu na haki zoezi la kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi litakaloanza September 04, 2017.

Mtaka ametoa kauli hiyo mara baada ya viongozi wa Serikali na Chama Mkoa na Wilaya, Wataalam, wafugaji na wadau wa uhifadhi na Utalii kukutana na kujadili suala la uondoaji mifugo katika Maeneo ya Hifadhi, yakiwemo ya  Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao wilayani Meatu.

“Mkafanye zoezi hili kwa weledi mkubwa na haki, lisije likawa zoezi la kuwaonea watu, kufanya utapeli kwa kujifanya mnachukua ng’ombe kwa ajili ya kutaifisha halafu mkagawana; viongozi na wote mtakaohusika mkalisimamie kwa makini sana suala hili” alisisitiza Mtaka
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe.Joseph Chilongani amesema baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi, wafugaji na wadau wa uhifadhi na utalii ametoa muda wa siku nne na kufikia Septemba 04 mwaka huu, wafugaji wawe wametoa mifugo katika maeneo ya hifadhi kwa hiari.

Dkt.Chilongani amebainisha kuwa Viongozi wa Wilaya ya Meatu walikutana na wafugaji katika maeneo yao na kuwatahadhalisha juu ya uingizwaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi, ili kuwasaidia waepuke adhabu ya kifungo na mifugo yao kutaifishwa kwa kuwa kuingiza mifugo hifadhini ni makosa kwa mujibu wa sheria.

“Maandalizi yote yako tayari, timu za kutekeleza zoezi hili zote zipo, nitoe muda wa siku hizi zilizobaki ili kufikia Jumatatu ya tarehe 04 zoezi la kuondoa mifugo kwenye Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na WMA ya Makao lianze, tulishawapa wafugaji muda wa kutosha tulipokuwa tukipita kwenye vijiji kuzungumza nao juu ya madhara ya  kuingiza mifugo hifadhini” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba la Maswa Lasato Masinde amezitaja baadhi ya changamoto za kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi kuwa ni ushindani wa malisho na maji kati ya wanyamapori na wafugwao,ongezeko la ujangili, kuuwawa kwa wanyamapori hasa walao nyama, magonjwa na mmonyoko wa udongo kutokana na wafugaji kukata miti.

Aidha, Masinde amefafanua kuwa suala la uingizwaji wa mifugo katika hifadhi linachangiwa pia na baadhi ya viongozi wa vijiji wasiokuwa waadilifu ambao hupokea fedha kwa wafugaji na kuwaruhusu kuingiza mifugo yao, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Meatu kuwachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wafugaji kupima maeneo yao wanayomiliki na kuyawekea miundombinu ya mifugo kama vile visima vya maji na mabwawa, majosho na mashamba ya malisho ili waweze kufuga kisasa na kuondokana na adha ya kuhangaika kutafuta maji na malisho.

Katika kikao hicho wafugaji kwa pamoja wamekubali kutoa mifugo katika maeneo ya  hifadhi na kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wa kupima maeneo yao na kuweka miundombinu, hivyo wameomba watalaam wa Ardhi na Mifugo waweze kuwasaidia namna wanavyoweza kutumia maeneo yao kufuga kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani humo.
Baadhi ya viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Meneja wa Pori la Akiba la Maswa, Lusato Masinde akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.

Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanayamapori ya Makao, Robert Simon akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mhifadhi kutoka Ranchi ya MWIBA, Julius Makaroti  akiwasilisha taarifa ya ranchi hiyo kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donald Magesa akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mmoja wa wafugaji wa Wilaya ya Meatu akichangia hoja katika kikao kilichofanyika wilayani Meatu kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe.Pius Machungwa akichangia hoja katika kikao kilichofanyika wilayani Meatu kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao wilayani Meatu na ambaye pia ni mfugaji, Anthony Philipo akichangia hoja katika kikao kilichofanyika wilayani Meatu kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,Said Samba akifafanua jambo katika kikao kilichofanyika Mjini Mwanhuzi  kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mhifadhi kutoka Shirika la Frankfoot, Sylevester Bwasama akifafanua jambo katika kikao kilichofanyika Mjini Mwanhuzi  kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!