Friday, May 3, 2019

VIONGOZI WA DINI, SIASA NA KIMILA WASHIRIKISHWE KUELIMISHA JAMII KUZUIA VIFO VITOKANAVO NA UZAZI-RC MTAKA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa Serikali mkoani hapa kuona umuhimu wa kuwashirikisha viongozi wa dini, siasa na wa kimila katika utoaji wa elimu kwa jamii na kuwahamasisha wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi..

Mtaka ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
“ Ni vizuri tukaongeza wigo wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa mama wajawazito  kuhudhuria kliniki kipindi cha ujauzito na kuhakiksha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya; viongozi wa dini,siasa na wa kimila wana nafasi kubwa kwenye jambo hili muone namna ya kuwashirikisha “ alisema  Mtaka.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) imeboresha vituo vya kutolea huduma, hivyo ni vema jamii ikaelimishwa umuhimu wa kutumia huduma za afya ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Katika hatua nyingine Mtaka ameishukuru UNFPA kwa namna ilivyosaidia katika ujenzi wa miundombinu ya afya,vifaa na vitendea kazi kama magari ya kubeba wagonjwa huku akisisitiza viongozi na watendaji walioshiriki katika uzinduzi wa kampeni hii kutoka na dhamira ya kuwavusha salama akina mama wajawazito na watoto na kupinga vifo vitokanavyo na uzazi..
Mwakilishi wa  Ofisi  ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dinna  Atinda ameusisitiza uongozi wa mkoa  kusimamia vituo vinavyotoa huduma za afya za msingi na dharura kuhakikisha vinatoa huduma bora kwa wananchi.
Naye Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Salome Mwijuma  ametoa wito  kwa jamii kuendelea kuwasaidia wanawake wajawazito waweze kuhudhuria kliniki muda wote, wapate lishe bora na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ili wajifungue salama.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Mageda  Kihulya amesema mwaka 2015 watoto 680 walifariki na mwaka 2018 watoto 640 walifariki,  wakati kwa upande wa akina mama wanaojifungua vifo vimepungua kutoka 48 mwaka 2015 na kufikia 40 mwaka 2018,  jambo ambalo linaonesha kuwa nguvu ya ziada kutoka wadau mbalimbali inahitajika kumaliza tatizo hili.
Dkt. Mageda amesema sababu zinazosababisha vifo vingi vya akina mama wajawazito kama vile kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua na mkingamo wa uzazi zinaweza kuzuilika, hivyo akatoa wito kwa wakina mama kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma kuzuia vifo hivyo, huku akisisitiza watoto chini ya miaka mitano nao wapewe chanjo kuzuia vifo..
Makamu Mwakilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, Dkt. Hashina Begum amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika jitihada mbalimbali za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, uliofanyika  Tuwavushe Salama, Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wadau wa afya  baada ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, DKT. Hashina Begum  na Mratibu wa UNFPA Mkoa wa Simiyu, Dt. Amir Batenga wakiteta jambo wakati wa hafla ya  Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, DKT. Hashina Begum akizungumza na viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu,wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.



Baadhi ya viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi. 
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dinna Atinda akizungumza na viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu,wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mageda Kihulya akiwasilisha taarifa ya hali ya vifo vya wanawake na  watoto, wakati wa hafla ya  Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akizungumza na viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu,wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  (kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dinna Atinda wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Mji wa Bariadi akichangia  jambo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia  jambo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo pichani), wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, DKT. Hashina Begum(katikati walioketi) akiwa katika piccha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wataalam na wadau wa afya,  baada ya wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, DKT. Hashina Begum(katikati walioketi) akiwa katika piccha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wataalam na wadau wa afya,  baada ya wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe Tano Mwera(kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, DKT. Hashina Begum(katikati walioketi) akiwa katika piccha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wataalam na wadau wa afya,  baada ya wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.




NAIBU WAZIRI MADINI ATOA SIKU MOJA KWA MAKANDARASI KUKAMILISHA JENGO LA SOKO LA MADINI SIMIYU


Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo ametoa muda wa siku moja kwa Mkandarasi  SUMA JKT anayejenga Jengo la Kituo cha Umahiri Simiyu kuamilisha sehemu ya Jengo hilo iliyopangwa kutumika kama Soko la Madini la Mkoa.

Nyongo ameyasema hayo Mei  02, 2019 wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambalo sehemu litatumika kama kituo cha umahiri na sehemu kama Soko la Madini la Mkoa.

“ Kwa  mkoa wa Simiyu tumeona hapa tunaweza kupatumia kwa kuanzia kwenye soko la madini, nimeshatoa maagizo kuwa jengo hili walimalizie mara moja, ili waweze kutoa sehemu ambayo itatumika kwa ajili ya soko la madini na kufikia kesho jioni tunataka jengo hili lianze kutumika kama soko la Madini “ amesema Nyongo.

Aidha, Nyongo amesema anatumia  fursa hiyo kuwajulisha wachimbaji  wadogo wadogo wa madini kuwa Simiyu kutakuwa na jengo ambalo litatumika kununua na kuuza madini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kama mkoa wamejipanga vizuri katika soko la madini, huku akiwakaribisha wafanyabiashara wa madini kutoka mkoa wa Simiyu  na mikoa jirani kufika katika kituo hicho ambacho amesema kitakuwa kituo bora chenye uhakika wa kufanya biashara hapa nchini.

Mtaka ameongeza kuwa kituo hicho ambacho kitafunguliwa rasmi wiki ijayo kitatoa fursa kwa Watanzania kuanza kuangalia ufanyaji wa biashara katika eneo la madini kwa njia ambazo ni halali, akatoa wito kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Simiyu pamoja na kuwekeza biashara katika kilimo, mifugo na viwanda wawekeze pia katika biashara ya madini.

Naye Sajenti Emmanuel Igogo kutoka SUMA JKT amesema agizo la Naibu Waziri la kukamilisha sehemu ya Jengo la Kituo ca Umahiri ambayo itatumika kama soko la madini (Kituo cha kuuzia madini) litatekelezwa kama lilivyoagizwa.

“ Tutatekeleza agizo la Mhe. Naibu Waziri tutaanza leo kulifanyika kazi na kwa kuwa kazi hii haikuwepo kwenye mkataba wetu wa awali nitawasiliana na viongozi wangu na tutakamilisha” alisema Sajenti Igogo.
MWISHO



Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo( wa pili kushoto)  akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea Kituo cha Umahiri kilichopo Nyaumata Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la Madini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( watatu kushoto) akichangia jambo kwenye mazungumzo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo( wa pili kushoto)  alipotembelea Kituo cha Umahiri kilichopo Nyaumata Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la Madini.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo( wa pili kulia)  akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea Kituo cha Umahiri kilichopo Nyaumata Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la Madini.
Jengo la Kituo cha Umahiri Simiyu kilichopo Nyaumata Bariadi, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la Madini.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent (kushoto) akizugumza na baadhi ya viongozi wakati wa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo( wa pili kushoto)  alipotembelea Kituo cha Umahiri Simiyu kilichopo Nyaumata Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la Madini.
Fundi akiendelea kupaka rangi  katika hatua za ukamilishaji kwenye Jengo la Kituo cha Umahiri Simiyu Simiyu kilichopo Nyaumata Bariadi, ambacho kimeamriwa kuwa sehemu ya jengo hilo ikamilike haraka na ianze kutumika kama Soko la Madini.

Wednesday, May 1, 2019

RC MTAKA: SIMIYU TUTAENDELEA KUFANYA KAZI KWA KUHESHIMIANA NA KUSIKILIZANA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema  Viongozi  Mkoani Simiyu wataendelea  kufanya kazi  na kuwahudumia wananchi  kwa kuzingatia utawala bora, utawala unaofuata sheria na uongozi wa kuheshimiana na kusikilizana.

Mtaka ameyasema hayo Mei Mosi, 2019 wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi na wananchi mkoani humo katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Kimkoa, yaliyofanyika katika Uwanja wa Nguzonane Wilayani Maswa.

“Tungependa tujenge utumishi ambao ni wa kipekee sana kwenye mkoa na kila mtumishi aliye kwenye mkoa huu ajisikie fahari kufanya kazi Simiyu; ahadi yangu kwenu ni kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa kuheshimiana,kusikilizana na kutiana moyo katikati ya changamoto ambazo watumishi wanazipitia” alisema

Aidha, amewashukuru wafanyakazi kwa namna walivyojitoa kwa hali na mali  kuhakikisha kwamba malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yanatekelezeka  na kusisitiza kuwa mkoa utaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Vyama vyote vya wafanyakazi na kuwataka waajiri wote wathamini vipaji vya watumishi wao.
Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Said Mselem ameomba Serikali kushughulikia suala la upandaji wa mishahara na madaraja kwa watumishi ili kuwaongezea ari na motisha katika kazi.
Katika hatua nyingine Mselem ameiomba Serikali kuu kuona uwezekano wa kuwabadilishia mfumo wa malipo ya mshahara watumishi wanaolipwa kupitia mapato ya ndani na kuanza kuwalipa kupitia HAZINA, ili wawe na uhakika wa kupata mishahara yao na michango yao ya mifuko ya hifadhi ya jamii iwasilishwe kwa wakati.
Nao baadhi ya wafanyakazi  kutoka vyama tofauti vya wafanyakazi wamesema Wafanyakazi Mkoani Simiyu wanapenda kazi zao na wanafanya kazi kwa uadilifu, hivyo wameiomba  Serikali iendelee kuboresha mazingira na kuwasaidia kutatua changamtozao ili waweze kufanya kazi wa uhuru na kujituma zaidi.
‘Watumishi tunapenda kazi zetu na tunafanya kwa bidii na uadilifu, tunajua wapo wachache wanaotuangusha lakini tunaendelea kuwahimiza wawajibike kutimiza azma ya kuwatumikia wananchi, ombi letu kwa Serikali itukumbuke kwenye kupanda madaraja wapo ambao hawajapanda toka mwaka 2015” alisema Mwenyekiti CWT Itilima Mwl. Rehema Shalali.
“Watumishi wanaolipwa kwa mapato ya ndani wanakutana na changamoto ya mafao yao wanapostaafu, mafao hayaendi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuwa wakati maana hawalipwi mishahara kwa wakati tunamwomba Mhe. Rais aliangalie hili, ili watumishi hao nao waweze kulipwa na HAZINA moja kwa moja” alisema Sara Kiyuga Mjumbe wa Baraza Kuu TALGWU Taifa.
Maadhimisho ya Mei Mosi kwa mwaka 2019 yamebebwa na Kauli Mbiu “ TANZANIA YA UCHUMI WA KATI INAWEZEKANA, WAKATI WA MISHAHARA NA MASLAHI BORA KWA WAFANYAKAZI NI SASA”  ambapo yamefanyika kwa mara ya saba sasa Kimkoa tangu mkoa wa Simiyu kuanziswa mwezi Machi, 2012.
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiimba wimbo wa mshikamano daima wa Wafanyakazi na baadhi ya viongozi wa Serikali na Vyama vya Wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani,  Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akipokea Maandamano ya Wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakiwa kwenye maandamano, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani  Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa mkoa huo Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Said Mselem akitambulisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Said Mselem akisoma risala ya wafanyakazi wa mkoa wa Simiyu kwa Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Simiyu,, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka aweze kuzungumza na wafanyakazi wa mkoa huo Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.



 Kwaya ya walimu wilayani Maswa wakitoa burudani ya wimbo katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya za Mkoa huo, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslous Nyongo akiwasalimia wafanyakazi na wananchi kwa ujumla, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.


 Baadhi ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.


Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari Dereva wake Bw.Viecent Mtebe, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari Mtunza Kumbukumbu wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega Bi. Laurencia katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari Mfamasia wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Oscar Tenganamba katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.

RAS SIMIYU ASAINI MKATABA NA SUMA JKT UJENZI WA JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesaini Mkataba wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Msimamizi Mkuu wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa, Kapteni Fabian Buberwa.
Mkataba huo umesainiwa Aprili 30, 2019 mbele ya Wataalam wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na SUMA JKT katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini ambaye aliwataka SUMA JKT kujenga jengo hilo kwa viwango na kuhakikisha linakamilika kwa wakati.
“SUMA JKT mmepewa heshima kubwa na Serikai yetu na viongozi wetu pia tunaomba muendelee kufanya vizuri ili kulinda heshima yenu; tunaomba mfanye kazi usiku na mchana jengo hili likamilike mapema na ka viwango” alisema Sagini.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa, Kapteni Fabian Buberwa amemhakikishia Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini kuwa wakipata fedha watahakikisha wanakamilisha jengo hilo kwa wakati na kwa viwango vya juu, ili kuendellea kulinda heshima waliyopewa na Serikali

Naye Mhandisi wa Ujenzi wa Mkoa wa Simiyu, mashaka Luhamaba amesema Jengo hilo litakalojengwa eneo la Nyaumata Mjini Bariadi, litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 5, 718, 387,926.20

Jengo hili linatarajiwa kuanza kujengwa mwezi Mei, 2019 na kukamilika baada ya miezi 18.
MWISHO.




Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto)  na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.

Mkuu wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi, Bi. Vivian Watugulu akiwaonesha jambo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto)  na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa katika Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.
Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) kabla ya viongozi hao kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019(kulia) Mhandisi wa Ujenzi wa Mkoa wa Simiyu, Mashaka Luhamba.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Wataalam kutoka SUMA JKT na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  ,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  ) kabla ya viongozi hao kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Wataalam kutoka SUMA JKT na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa  ,inayotajarajiwa  kujengwa katika eneo la Nyaumata Mjini Bariadi kuanzia mwezi Mei, 2019.
Msimamizi wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni. Fabian Buberwa(katikati) akioneshwa ramani ya Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wakala wa Ujenzi (TBA) Simiyu, wakati aliopofika 

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!