Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB)
imeuhakikishia uongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa itafanya kazi kwa karibu katika
kutoa fursa ya mikopo itakayowasaidia wakulima mkoani humo kulima kilimo
chenye tija..
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka pamoja na Wakurugenzi na Wataalam kilimo
na umwagiliaji, ushirika na mifugo kutoka Halmashauri zote za Simiyu,Kaimu
Mkurugenzi wa Banki hiyo Francis Assenga amesema wapo tayari kukopesha na
kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu kutokana na utayari wao na uwepo wa mwongozo
elekezi wa shughuli za kilimo
zilizofanyiwa utafiti.
Amesema
Benki hiyo ambayo ina lengo la kuleta
mapinduzi ya kilimo Tanzania imeridhia kutoa mikopo katika miradi ya kilimo kwa wakulima, vikundi
vilivyosajiliwa, vyama vya ushirika na kupitia Benki na taasisi nyingine za
kifedha ambazo zinaweza kuwakopesha wakulima, ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa wakulima mkoani humo.
Ameongeza kuwa ili kufanikisha azma ya Mkoa wa Simiyu ya kukifanya kilimo kuwa ni biashara na kukuza uchumi wa wakulima wake , Benki ya TADB itasaidia kutoa mikopo itakayoambatana na mafunzo ya kuwajengea uwezo wakopaji hususani wanawake na vijana.
Ameeleza kuwa benki yake imekwisha tenga kiasi cha shilingi milioni 650 kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo na Bil 42 za mkopo kwa wanawake na vijana, hivyo amezisisitiza Halmashauri za Mkoa wa Simiyu kuwahamasisha vikundi vya wakulima vilivyosajiliwa kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo yenye riba ndogo na masharti nafuu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu uko tayari kufanya kazi na Benki ya TADB kupitia vikundi vya uzalishaji, Halmashauri na Miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani humo, ikiwa ni pamoja na miradi ya umwagiliaji ya Mwamanyili Wilayani Busega ulio katika hatua ya upembuzi yakinifu na Mwasubuya wilayani Bariadi ambao uko katika hatua ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.

“Tungehitaji
kuwa Mkoa ambao kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo tungetengeneza namna
ambayo ingewasaidia wakulima na ikasaidia mikoa mingine kuja kuona maendeleo ya
kilimo ambayo ni matokeo ya Serikali
kuwekeza katika Benki ya Kilimo” amesema Mtaka.
"Sisi
kama Mkoa tumejipanga ,tumetoa Elimu ya utayari na namna ya utekelezaji wa shughuli zote kwa
wataalam wetu pamoja na wananchi na isitoshe tayari tumeshafanya utafiti na kuandaa
mwongozo wa uwekezaji ndani ya mkoa, hivyo tunawakaribisha kuwekeza” Amesema
Mtaka
Aidha
Mtaka ameongeza kuwa Mkoa wa Simiyu unatekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda chini
ya Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” ambapo hadi sasa
kuna kiwanda cha chaki na maziwa na miradi mingine minne ya viwanda iko katika
upembuzi yakinifu, hivyo benki inaweza kuwekeza katika miradi hii kwa
kuwawezesha wakulima na wafugaji kuzalisha malighafi ya Viwanda hivyo au kuwa
mdau katika viwanda hivyo.
Naye Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB Augustino Matutu Chacha amesema wamefurahishwa na utayari wa Mkoa wa Simiyu juu ya kuwawezesha wakulima na Benki hiyo iko tayari kutoa mikopo pia kwa wakulima wa zao la pamba ambao wanazalisha zaidi ya asilimia 60 ya pamba yote nchini ili izalishwe kwa wingi zaidi na katika ubora wa hali ya juu.

Chacha
amesema wataalam wa kilimo wa Mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana
na wataalam wa benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) watakutana ili
kuona namna watakavyofanya kazi kwa pamoja ili mikopo itakayotolewa iweze kuwa
wa manufaa kwa wakulima na nchi kwa ujumla.
Aidha amewaeleza Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuwa, Halmashauri zinaweza kupatiwa mikopo ili ziweze kuendesha miradi ya kilimo itakayoweza kuwa vyanzo vipya vya mapato kwa Halmashauri zao.
Aidha amewaeleza Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuwa, Halmashauri zinaweza kupatiwa mikopo ili ziweze kuendesha miradi ya kilimo itakayoweza kuwa vyanzo vipya vya mapato kwa Halmashauri zao.
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB), Francis Assenga
akizungumza na Uongozi wa Mkoa wa Simiyu pamoja na wataalam wa Kilimo, ushirika
na Mifugo (hawapo pichani) Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kati ya
uongozi wa Mkoa huo, wataalam wa kilimo, mifugo na ushirika na Uongozi wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania.
Mkurugenzi
wa Biashara na Mikopo, Augustino Matutu Chacha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania(TADB), akizungumza na Uongozi wa Mkoa wa Simiyu pamoja na wataalam wa
Kilimo, ushirika na Mifugo (hawapo pichani) Mjini Bariadi.
Mkuu wa Idara ya kilimo
wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Juma Chacha akichangia katika kikao
kilichofanyika katika uongozi wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu na Benki ya Maendeleo
ya Kilimo Tanzania(TADB) Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wataalam
wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa katika kikao
kilichofanyika Mjini Bariadi kati ya Uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB).
Mkuu wa Idara ya Kilimo wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Wilbert Siogopi akichangia katika kikao
kilichofanyika kati ya Uongozi wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu na Benki ya Maendeleo
ya Kilimo Tanzania(TADB) Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wataalam
wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa katika kikao
kilichofanyika Mjini Bariadi kati ya Uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB).
Baadhi ya Wataalam
wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa katika kikao
kilichofanyika Mjini Bariadi kati ya Uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB).
0 comments:
Post a Comment