Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini Inspekta Generali Simon Sirro amesema Makamanda wa Polisi wa Mikoa
wataendelea kubaki katika vituo vyao vya kazi endapo watatimiza wajibu wao na kupunguza
uhalifu katika mikoa yao.
IGP Sirro
ameyasema hayo wakati wa ziara
yake Mkoani Simiyu katika mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya
kamaliza mazungumzo yake na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa yaliyofanyika
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
IGP Sirro amesema
Makamanda wa Polisi Mikoa wanapaswa kutimiza wajibu wao katika kujali na kusimamia suala la Ulinzi na
Usalama katika mikoa yao ili wananchi wakae kwa amani na mali zao ziwe salama.
“ Moja ya lengo la
ziara yangu ni kuwakumbusha askari wa jeshi la polisi uwajibikaji na kuwajibika
ni pamoja na kulinda watu na mali zao, makamanda wa polisi mikoa nimewaambia kamanda
ataendelea kukaa kwenye mkoa ule kama uhalifu utakuwa umepungua kwa kiasi
kikubwa” amesema Sirro
Inspekta Sirro amesema
ziara yake pia imelenga kuwakumbusha askari majukumu yao katika kuhakikisha
wanawajibika kutimiza kiapo chao na kutenda haki ili wananchi waendelee
kuliamini Jeshi la Polisi.
Kiongozi huyo pia
ameelekeza viongozi wa jeshi la polisi wasiwanyime haki ya dhamana watu wenye makosa ya kawaida ambayo
yana dhamana isipokuwa kwa makosa
makubwa yakiwepo ya mauaji, kughushi na mengine yanayohitaji upelelezi.
Kuhusu suala la kuwepo
kwa mahusiano mabaya kati ya baadhi ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa na
Waandishi wa habari, Inspekta Sirro amefafanua kuwa Makamanda wa Polisi wa
Mikoa watimize wajibu wao kama watumishi wa Umma kwa kuwajali waandishi kama
wanavyowajali wateja wengine kwa kufuata sheria na akawataka waandishi wa
habari wafuate sheria, kanuni na taratibu pasipo kuvuka mipaka.
Akakimkaribisha Mkuu
huyo wa Jeshi la Polisi nchini, katika Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Mkoa huo,
Mhe.Anthony Mtaka amemshukuru Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Boniventure
Mshongi na Jeshi la Polisi kwa ujumla kwa namna wanavyoshirikiana katika suala
la ulinzi na usalama.
Aidha, amemuomba Mkuu
huyo wa Jeshi la Polisi nchini kuona uwezekano wa kusaidia kujenga majengo ya
Ofisi na nyumba za makazi kwa ajili ya Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.
Inspekta Simon Sirro amewasili Mkoani Simiyu akitokea Mkoani Mara akiwa
katika ziara yake ya kikazi ambapo pamoja na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Wilaya ambao pni Wenyeviti wa Kamati za
Ulinzi na Usalama za wilaya, pia amezungumza na viongozi na askari wa Jeshi la
Polisi mkoani humo.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili
ya ziara yake ya kikazi Mkoani Simiyu
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini, IGP Simon Sirro (kulia) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) wakati wa ziara yake mkoani humo,
(kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akifuaahia jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
IGP Simon Sirro mara baada ya kumaliza mahojiano na waandishi wa habari wakati
wa ziara yake mkoani Simiyu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini, IGP Simon Sirro akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara ya
kikazi mkoani Simiyu.
Wajumbe wa Kamati za
Ulinzi na Usalama Mkoa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu za Mkoa wa Simiyu
wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro(hayupo pichani)
katika kikao alichofanya akiwa ziarani mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP
Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya
kikazi mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Mkuu wa Jeshi
la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (kulia) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa huo wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini, IGP Simon Sirro (kulia) akizungumza na Kamati ya Ulizi na Usalama ya
Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani humo,(baadhi ya wajumbe hawapo
pichani).
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza katika kikao cha Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini, IGP Simon Sirro (hayupo pichani) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
huo wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini, IGP Simon Sirro akisalimiana na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya
Utawala na Rasilimaliwatu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele
Ndaki mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi
mkoani Simiyu
Kaimu Katibu Tawala
Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji,katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Dkt.Gamitwe Mahaza (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP
Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi
mkoani Simiyu.
Kaimu Mkuu wa Jeshi la
Magereza Mkoa wa Simiyu(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya
kikazi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Msaidizi
Sehemu ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Ndg.Simon Maganga(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP
Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya
kikazi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamaliza mazungumzo yake
na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu
Afisa Ardhi Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi.Grace Mgombera (kulia)akisalimiana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi
kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment